Flower
Flower

Thursday, February 6, 2020

Ufeministi ni nini


Suala la kumtambua mwanamke kuwa hana akili lina historia ndefu katika maandiko ya kifalsafa. Aristotle, wanafikra wa karne za kati na wanafalsafa wapya wa kiliberali wakiwemo Hume, Rousseau, Kant na Hegel wote walikuwa na shaka kuhusu suala kuwa mwanamke ana akili. Kwa msingi huo mafeministi wa kiliberali walitilia mkazo mitazamo yao ya kiliberali na kutetea wanawake katika suala la kutambua haki za kisiasa za watu kwa mujibu wa kiwango chao cha akili wakisema kuwa kubakia nyuma wanawake katika uwanja huo wa kisiasa ukilinganisha na wanaume, ni matokeo ya kunyimwa haki ya kupata suhula na fursa sawa na za wanaume. Dukuduku kubwa zaidi la mafeminsiti wa kiliberali lilikuwa haki zao za kisiasa na kisheria. Hivyo mapambano yao ya karne ya 19 hususan katika wimbi la kwanza la ufeministi yalifanyika kwa shabaha ya kurejesha haki za kumiliki wanawake walioolewa. Mafeministi wa kiliberali walitilia mkazo ubinadamu wa mwanamke na kutaka apewe nafasi sawa na ya mwanaume. Kwa msingi huo walitaka kuwepo usawa baina ya wanawake na wanaume katika fursa za kazi na kutaja kufanya kazi za nyumbani kuwa ni dhulma kwa mwanamke. Vilevile nafasi ya mama ni miongoni mwa mambo yaliyozusha mjadala mkubwa zaidi kati ya mitazamo ya mafeministi wa kiliberali ambao walitambua suala la kutoa mimba kuwa ni miongoni mwa haki za kimsingi za mwanamke (Wamitila, 2003).
Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza katika Ulaya wakati haki za binadamu zilipoanza kutangazwa, ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee. Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kampeni ya awali kuanzia karne ya 19.

Uhakiki wa kifeministi ulishika kasi miaka ya 1960 na kuendelea kukua na kuishia kuwa muhimu katika miaka ya hivi karibuni. Zipo kazi kadhaa zilizoandikwa kabla na kuhimulika suala hili kwa namna moja ama nyingine. Kazi kuu mbili za “A Room of One’s Own” ya Virginia Woolf na “A virdiction of the Right of women “ya Mery Wollsto Necraft. Zimechangia sana katika kutilia mkazo nadharia ya Ufeministi.

Williady (2015) anasema kwamba nadharia hii inahistoria ndefu duniani, akimaanisha ni moja ya nadharia zilizopata kutokea miongo mingi iliyopita. chanzo cha kuibuka kwa nadharia hii ni vuguvugu la kutaka kufuta kabisa uonevu wa mwanaume kwa mwanamke. Nadharia hii inadai kuwa chimbuko la uonevu na ukandamizaji unaofanywa na wanaume kwa wanawake ni uroho wa mwanaume katika kumtawala mwanamke. Kwa ufupi, ajaenda kuu ya ufeministi na mafeministi ni kumaliza kabisa utawala wa mwanaume kwa mwanamke.

Mmoja kati ya wadau waliochangia sana kuendelea kwa nadharia hii kwa kasi ni Adrew Dworkin mwaka 1976 akiwa katika mji mkuu wa Uingereza; London, alitoa mapendekezo makali katika kukomesha utawala wa mwanaume kwa mwanamke, Dworkin anasema: Ili kufanikisha, tunahitaji kubomoa kabisa muundo wa mihimili ya utamaduni wa jamii kama vile sanaa, kanisa, sheria, kaya zinazodhibitiwa na baba, jamii na taswira zote za asasi, mila, desturi ambazo zinamwona mwanamke kuwa mtu ovyo.

Hata hivyo, kazi iliyoishia kuwa na mchango mkubwa katika kuuweka msingi wa uhakiki wa ufeministi ni kazi maarufu ya mwandishi wa Kifaransa, Simone de Beauvoir iitwayo, “The Second sex,” ya mwaka 1952. Katika kitabu hiki, mwandishi huyu anachukuwa mkabala wa kiharakati kwa kushambulia na kukosoa baadhi ya asasi zinazochangia katika kumdhalilisha au kumdunisha mwanamke. Asasi kuu anazozishambulia ni ndoa, dini na utamaduni. Hata hivyo, nadharia ya ufeministi ilichimbuka huko Marekani katika harakati za kukomesha biashara ya utumwa mwaka 1830 ambapo wanawake walianzisha harakati za kupigania haki za mwanamke.

Malenya (2012) anaeleza kuwa dhana ya ufeministi ilianza kujitokezaa kwa mara ya kwanza baada ya Simone De Beauvoi aliyezaliwa huko Ufaransa akiwa ni mtoto wa kike na wa kipekee katika familia yao na ambaye alionekana kama muhamasishaji wa kwanza juu ya Ufeministi. Hii ilitokana na uwezo mwingi aliokuwa nao katika kufikiri, hekima na bidii katika kazi vilivyosababisha kusifiwa daima na baba yake. Hali hii ilianza kuibua mtazamo hasi dhidi ya wanawake baada ya baba yake kudai kuwa, uwezo wa akili alionao unafanana na wake na wala sio kama wa mama yake. Hali hii ilimfanya Simone De Beauvoi kujenga dhana ya unyanyasaji wa wanawake na hata kumfanya asifikilie kuolewa bali ajikite na harakati za ukombozi kwa wanawake. Kupitia harakati zake aliamsha hisia na hari kwa wanawake kutaka kujikomboa. Baadhi ya nyanja zilizoonekana kumkandamiza mwanamke ni pamoja na asasi za kijamii kama vile dini, tamaduni na uandishi mbalimbali wa kazi za fasihi.
Malengo ya Nadharia ya Ufeministi
Wamitila (2006:160-161) na Ntarangwi (2004:52-56) wamebainisha malengo mbalimbali ya ufeministi. Ni kweli kwamba kuna baadhi ya malengo ya ufeministi yanakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika lakini baadhi ya malengo hayo yanasawiri maisha halisi ya mwanamke wa kiafrika.
Nadharia ya ufeministi ina lengo la kuondoa unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa mwanamke. Hivyo basi, malengo ya ufeministi yalijikita katika kumnasua mwanamke kutoka katika pingu za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Malengo haya ndiyo yanayoleta ukinzani wa maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika. Hali hii imeleta mabadiliko katika maisha ya wanawake wa kiafrika, kama vile kutaka haki ya elimu, kumiliki mali, kurithi mali, kutaka nafasi za uongozi, pia kuwa na maamuzi ya kifamilia au kiukoo, katika kupingana na pingu za maisha.


 Dhana ya Ufeministi

Ufeministi (kutoka mzizi wa Kilatinifemina,’ yaani wa ‘kike’; au mwanamke. Kwa lugha ya kifaransa féminisme linamaanisha harakati ya ukombozi wa wanawake‎) ni jina linalojumlisha aina nyingi za misimamo, itikadi na matapo tofautitofauti yanayochangia lengo kuu la kutetea haki za wanawake dhidi ya ubaguzi wa jinsia uliotawala dunia kwa muda mrefu sana upande wa siasa, uchumi, utamaduni, dini na jamii kwa jumla (Luvenduski & Randall, 1993).

Nadharia ya Ufeministi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama vile: Wamitila (2003:253) anayesema kuwa hii ni nadharia ambayo imewekewa msingi na msukumo mkubwa pamoja na nia ya kupigania ukombozi wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kidini, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Aidha, anaongeza kuwa ufeministi ni nadharia ambayo inasaili na kudadisi itikadi ya kiume ambayo imekuwepo katika jamii kwa kipindi kirefu. Kudadisi pia fasiri za kiume za fasihi pamoja na mikabala ya kiubabedume.

Ntarangwi (2004:45) anadai kuwa Ufeministi ni nadharia ambayo inajaribu kukiuka mitazamo ya kiume ambayo yaelekea inatumiwa sana katika jamii. Anaendelea kusema kuwa nadharia ya ufeministi imetokana na mkondo na harakati za kutetea haki za wanawake ulimwenguni na imejikita katika imani ya usawa wa kijinsia, kijamii, kisiasa na kiuchumi. 

Williady (2015) anasema kwamba ufeministi ni ninadharia iliyojaribu kuvunja mwiko wa mfumo dume hapa dunia kwa kuanzisha mapambano ya usawa wa kijinsia, bilashaka majaribio haya bado hayajafanikiwa. Anaongeza kwamba hayajafanikiwa kwa sababu jamii inachukua muda kubadilika hivyo matarajio ya wanawake yatafikiwa tu kwa kuwa hawakata tamaa.

Waandishi wengine wanaendelea kuufafanua ufeministi kama istilahi inayotumiwa kueleza nadharia ambayo imewekewa misingi na msukumo mkubwa pamoja na nia ya kupigania ukombozi wa wanawake kutokana na pingu za kiutamaduni na kidini zilizomfunga kwa muda Mrefu (Malenya, 2012).
Irib (2014) anaongeza kuwa ufeministi ni harakati za ukombozi zilizoanzishwa na wanawake ili kupinga mfumo dume ambao unawakandamiza wanawake katika nyanja mbalimbali. Anaendelea kuunga mkono tafsiri ya Wamitilia kwamba, ufeministi ni nadharia inayopinga asasi zote za kijamii zinazochangia katika kudhulumiwa kwa mwanamke katika Nyanja mbalimbali.
Kwa jumla, mwandishi anaiona nadharia ya ufeministi kama nadharia iliyojikita katika kupinga ukandamizaji wa mwanamke unaofanywa na mwanaume katika jamii hususan katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni. Hivyo basi, ufeministi ni harakati zinazofanywa na wanawake kujikomboa katika Nyanja mbalimbali za: kifikra, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni kutoka katika mifumo ya ukandamizwaji.  

Aina za Ufeministi na Mikondo yake
Mgawanyiko umeanza kujitokeza kati ya wale wanaotaka wanawake wafanane kabisa na wanaume na wale wanaoona umuhimu wa kutunza upekee wa mwanamke katika uhusiano wa kukamilishana na mwanamume. Kwa mfano: wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani hoja ya jadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa: wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki katika shughuli zote sawasawa. Wengine hukubali kwamba kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakini tofauti hizo zisiruhusiwe kuwapa wanaume kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa, lakini wasilazimishwe kufanya hivyo, nao wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hiyo ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka waliyoitumia kwa kazi ya nyumbani. Wengine husema jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenzi ya wanaume, hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapinduzi katika jamii. Na kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume, na ni muhimu watoe mchango wao wa pekee (Gabriel, 2010).
Malenya (2012) anaibuka na kuugawa Ufeministi katika makundi mbalimbali yakiwemo ya kiuharakati, kiutamaduni, kiuyakinifu na kadharika.
Ufeministi wa Kiharakati
Ufeministi wa Kiharakati; huu ni ukombozi unaotambua kuwa mwanamke ananyanyaswa na kukandamizwa na mwanaume hivyo kuona umuhimu wa kuwaelimisha wanawake kukataa unyanyaswaji na ukandamizwaji dhidi yao. Aina hii inamwona mwanamme kama mkandamizaji wa kwanza wa uhuru na haki za mwanamke. Hivyo basi, mwanamke anahamasishwa kuanza harakati za ukombozi dhidi ya minyororo.
Ufeministi wa Kiutamaduni
Ufeministi wa kiutamaduni; hii ni aina ya ufeministi ambayo inautizama utamaduni kama nyenzo kubwa katika kumdhalilisha na kumfanya mwanamke aamini kuwa anapaswa kuwa na hali aliyonayo mfano; kukandamizwa, kudhalilishwa na kukosa uhuru wa kutoa maoni. Ufeministi unaotoa wito kwa kila mwanamke kuona umuhimu na wajibu wa kushiriki katika ukombozi wa mwanamke. Tamaduni mbalimbali hasa za kiafrika zimekuwa zikimgandamiza mwanamke katika mambo mbalimbali kwa mfano; wanawake katika jamii ya Wahaya (kabila linalopatikana Bukoba mkoani Kagera) hawakuruhisiwa kula nyama ya kuku au kula senene.
Ufeministi Huru
Hutetea usawa kati ya wanawake na wanaume katika ngazi zote za maisha. Mkondo huu hushikilia kwamba maadamu wanadamu wote ni sawa, wote wake kwa waume wanapaswa kuwa huru katika kutekeleza malengo na majukumu yao ya kila siku.
Ufeministi wa Kiuyakinifu
Ufeministi wa Kiuyakinifu; ni aina ya ufeministi ambao unamkomboa mwanamke katika misingi ya kijinsia hususani katika utekelezajii wa majukumu mbalimbali ya kijamii ikimaanisha kuwa mwanamke huchukuliwa kama mtu asiyeweza kusimamia na kufanya baadhi ya majukumu au kazi kama ilivyo kwa mwanaume. Kwa mfano utabibu, ualimu, uadhili, uongozi, ujenzi pamoja na upendeleo katika uelimishaji wa watoto wa kike ambapo wavulana hupewa kipaumbele zaidi.

Ufeministi wa Kidhahania
Ufeministi wa Kidhahania; ni aina ya ufeministi ambao unamwonesha mwanamke kama kiumbe huru mwenye uwezo wa kuteua, kujilinda na kujitazama atakavyo mwenyewe.
Aidha, mwanamke anaona kuwa hakuna haja ya mawazo yake kuamuliwa na mwanaume au mtu yeyote katika jamii. Kutokana na dhana hii, jamii imeanza kuwapata wanawake wanajeshi, wazalishaji mali, walimu na matabibu.
Ufeministi wa Kimaksi
Ufeministi wa kimaksi pia ni miongoni mwa mielekeo ya ufeministi. Kundi hili liliamini kuwa chanzo dhulma dhidi ya mwanamke ni kukandamizwa kwao kiuchumi, kijamii na kisheria akilinganishwa na mwanaume na linasema dhulma hiyo itakomeshwa kwa kubadilishwa haki za kijamii na kiuchumi. Mafeministi wa kimaksi wanamtambua mwanawake kuwa ni mithili ya vibarua katika makucha ya wanyonyaji na wanatumikia maslahi ya mfumo wa ubepari. Wanaamini kuwa wawekezaji wanatumia nguvu rahisi ya wanawake na watoto kwa shabaha ya kupunguza gharama za uzalishaji. Kwa msingi huo mafeministi wa kimaksi wanasisitiza juu ya udharura wa kufutwa mfumo wa kibepari na kukomeshwa dhulma dhidi ya wanawake. Kundi hili la mafeministi pia linashabihisha kazi ya kuzaa na kujifungua mwanamke na mwenendo wa wananyama na si kitendo cha kibinadamu.
Karl Marx na Engels wakinukuliwa na Malenya (2012), walikuwa wakiamini kwamba familia ndiyo taasisi ya kwanza ya kijamii ambako hakuna usawa katika kugawa kazi baina ya mwanamke na mwanaume na kwamba mfumo huo wa familia unapaswa kuangamizwa na badala yake kuanzishwe taasisi za ushirika au ujima ili kazi za nyumbani, kulea watoto na kadhalika zifanywe na jinsia mbili kwa usawa. Fikra hizi za kimaksi zilivuruga mipaka ya kifamilia na kupuuza uhakika wa kijamii. Vilevile mafeministi wa kimaksi waliamini kuwa, dhulma dhidi ya wanawake zinatokana na mfumo dume na ubepari, wakati hakuna mfungamano wa aina yoyote baina ya viwili hivyo.
Ufeministi wa Kisoshalisti
Ufeministi wa kisoshalisti ni katika milengo ya harakati ya ufeministi. Mlengo huu pia unasema kuwa uhusiano baina ya wanawake na wanaume unatokana na muundo wa kijamii na kiuchumi na mageuzi makubwa au mapinduzi ya kijamii, na kwamba kuwepo haki sawa kati ya wanawake na wanaume kumo katika usawa wa kijamii na kufutwa kabisa dhulma ya kijinsia na kitabaka. Mafeministi wa kisoshalisti wanasema mfumo wa kugawa kazi kwa mujibu wa jinsia ya mtu na kubana sehemu za kazi za wanawake ndani ya nyumba na kazi za mama ulibuniwa kwa ajili ya kudhamini maslahi ya kiuchumi ya ubepari. Mafenisti hawa wa kisoshalisti wanakubaliana na uchambuzi wa wenzao wa kimaksi kuhusu uhusiano wa kitabaka wa ubepari, kwa msingi huo wanasisitiza kuwa ili kupatikana usawa na kubadili hali ya sasa kuna ulazima kuwepo mapambano dhidi ya mfumo dume na ubepari. Wanasema mapambano hayo yanapaswa kupanuliwa zaidi kuanzia maeneo ya viwandani hadi kazi zote za umma na za binafsi ambako wanawake wanabaguliwa (Gabriel, 2010). Moja ya matatizo makubwa ya mtazamo huu ni kwamba unayafanya maisha ya mwanaume na mwanamke kuwa uwanja wa vita na mpambano baina ya jinsia hizo mbili ilhali, kimaumbile, kila mmoja kati ya wawili hao ana nakisi na mapungufu ambayo hayawezi kuondolewa isipokuwa kwa ushirikiano na maelewano baina yao.

Ufeministi wa Kuchupa Mipaka (radical feminism)
Mlengo mwingine wa ufeministi ni ule wenye misimamo mikali ya kuchupa mipaka (radical feminism). Mafeministi hawa wenye misimamo mikali wanadai kuwa, dhulma zinazofanyika kwa msingi wa jinsia ndizo kubwa zaidi ya zote na kwamba zinatokana na mfumo dume (Patriarchy). Wanasisitiza kuwa wanaume au kwa ujumla mfumo dume ndiyo sababu kuu ya dhulma zinazowasibu wanawake na kwamba sheria zisizo za kiadilifu zinachangia pia katika mfumo kandamizi unaompa mwanaume mamlaka kamili kuanzia katika familia hadi katika taasisi za kisiasa. Mafeministi hawa wenye misimamo mikali wanasema wanaume wote ni wakatili na wadhalimu dhidi ya wanawake na kwamba kunahitajika mapinduzi makubwa ya kuondoa hali hiyo na si kubadili sheria za kisiasa na kijamii tu (Gabriel, 2015). Mafeministi hawa wanafikia kiwango cha kutoa wito wa kuuawa na kufutwa kabisa wanaume! Misimamo ya kupindukia mipaka ya mafeninisti hawa sambamba na mitazamo yao kama ile ya kupuuza tofauti za kimaumbile kati ya mwanamke na mwanaume, kupuuzwa haki za wanawake kama wale wenye asili ya Afrika au weusi na kumtwisha mwanamke majukumu mazito ya kimaisha, ilikabiliwa na malalamiko na upinzani mkubwa hata ndani ya jamii ya wanawake. Kwa msingi huo katika wimbi la tatu la ufeministi kulitolewa wito wa kutazamwa upya na kufanyika mabadiliko katika mitazamo ya ufeministi.

Misingi ya Nadharia ya Ufeministi
Mchango mkubwa katika kuweka msingi wa uhakiki wa ufeministi ni kazi maarufu ya mwandishi wa Kifaransa, Simone de Beauvoir iitwayo, “The Second sex,” ya mwaka 1952. Katika kitabu hiki, mwandishi huyu anachukuwa mkabala wa kiharakati kwa kushambulia na kukosoa baadhi ya asasi zinazochangia katika kumdhalilisha au kumdunisha mwanamke. Asasi kuu anazozishambulia ni ndoa, dini na utamaduni. Miongoni mwa misingi ya kifikra ya ufeministi ni pamoja na:
·         kupinga na kutupilia mbali mafundisho ya dini. Mafemenisti wanayaona mafundisho ya dini kuwa yanachangia katika kuimarisha utamaduni wa mfumo dume, kwa msingi huo wanaamini na kufuata thamani za kimaada na kupinga thamani za kidini. Wanasema thamani na mafundisho ya dini ndiyo kizuizi kikuu katika njia ya kufikiwa malengo yao kwani wanaamini kuwa dini za Mwenyezi Mungu zinathamini na kutukuza sana familia na nafasi ya mama, na ili kulinda nafasi hiyo zinamzuia mwanamke kushiriki katika baadhi ya mambo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kadhalika. Vilevile wanasema dini zinashajiisha na kuhamasisha uzazi na kuzaa, na zinakataza kuavya mimba na kuwalazimisha watu kuzilinda na kulitambua suala hilo kuwa ni sawa na kulinda nafsi ya mwanadamu mzima. Hivyo basi kuna haja ya kufanyika jitihada za kujiweka mbali na thamani na mafundisho ya dini!

·         Nadharia hii inatumika fasihi kama jukwaa la kueleza kwa uyakinifu hali aliyonayo mwanamke ili kumsaidia kumwzwsha mtu yeyote kuielewa hali hiyo na kisha kumsaidia mwanamke. Fsihi imekuwa ikitumiwa na Waandishi mbalimbali katika kazi zao kumwelezea mwanamke na adha anayoipata katika jamii yake.

·         Nadharia hii inanuia kuwasawazisha wanadamu kwa upande wa utamaduni na uana. Inapigania jamii mpya yenye msingi katika amali za kibinadamu. Baadhi ya amali hizo ni zile za kike na za kijadi na ambazo zinadharauliwa katika jamii ya sasa.

·         Mitazamo huu Vilevile unajaribu kuhamasisha utungaji wa kazi za sanaa zenye wahusika wa kike wanaoweza kuhigwa (kuwa mfano), wanawake ambao hawategemei wanaume ili wajitambulishe. Kazi hii yaweza kufanywa na wanaume ili kuonyesha ya kwamba wanakubaliana na uwezo wa mwanamke kusimama peke yake na kujitambilisha katika Nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

·         Inaendeleza na kukuza hisia za umoja wa wanawake kama Kundi linalodhulumiwa. Hii itasaidia kuzindua na kuleta mwamko kwa upande wanawake jinsi wanavyojiona na uhusiano wao na watu wengine.

·         Nadharia hii inadhamilia kuvumbua na kuziweka wazi kazi za kifasihi zilizotungwa na wanawake na ambazo zimepuuzwa kwa sababu ya utamaduni unaopendelea wanaume. Kisha kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi katika utunzi wa kazi za kifasihi ili kuptia humo waweze kupaza sauti zao.

Wafeministi wanaamini kuwa mtazamo jumla wa jamii nyingi unawadunisha wanawake na kuwafanya watu wa daraja la pili. Kwa msingi huo wanasisitiza juu ya kubadilishwa mtazamo wa jamii kuhusu wanawake na kufutwa ubaguzi unaolenga jamii hiyo. Hapa inatupasa kusema kuwa, kila mtu mwenye insafu anajua kwamba, mijadala inayohusiana na haki za wanawake na mafeministi na wito wa kufanyika mabadiliko katika mtazamo unaowaona wanawake kuwa ni wanadamu wa daraja la pili katika nchi za Magharibi na vilevile juhudi za mafeministi za kupigania haki zao za kisiasa, kijamii na kichumi vimepelekea kupatikana baadhi ya mafanikio kwa maslahi ya wanawake hususan katika nchi za Magharibi. Hata hivyo suala la kupigania haki za wanawake na kupambana na ubaguzi halipasi kuwa kisingizio cha kutokomeza na kuua maana ya maisha, kumdunisha mwanaume katika jamii na kulazimisha haki na majukumu sawa na yanazofanana licha ya tofauti za kimaumbile baina ya jinsia mbili za wanadamu (Irib, 2014).

Uislamu sio pekee wenye itikadi ya kuwatukuza wanaume bali watu mbalimbali toka katika dini za Uyahudi (agano la kale), Ukristo na Uislamu pia katika Quran. Dini zote zinawatukuza wanaume kwa sababu zimeanzishwa kutokana na misingi ya jamii zenye kutukuza wanaume. Mtafiti anasema kuwa hata hijabu kwa wanawake sio tu kwa waislamu pekee, ni kwa utamaduni wa kale uliorithiwa na wenye kufanana na dini ya kisita (utawa) (Nyangasa, 2016).
Katika andiko la the Global and mail octoba 4, 1994, mwanafunzi msichana wa Kiislam avaae kitambaa cha kufunika kichwa alinyimwa haki yake ya kupata elimu nchini Ufaransa. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba; je dini za Uislam, Ukristo na Uyahudi zinafanana juu ya wanawake? Au dini za Ki-risto huwatendea vyema wanawake kuliko Waislam?. Nafasi ya mwanamke katika dini hizi tatu inatokana na ushahidi wa maandiko ya vitabu vitakatifu vya Quran, Hadithi za mtume (S.A.W), Biblia, Talmudi (Kitabu cha Wayahudi) (Yangasa, 2016).
Kosa la Hawa (Eva)
Dini hizi tatu zinakubaliana ya kwamba wanawake na wanaume wote wameumbwa na Mungu. Lakini tofauti zinaanzia pale tu mwanaume alipoumbwa wa kwanza na mwanamke kutokea ubavuni mwa mwanaume (Mwanzo, 2:4-3:24). Lakini Mungu aliwakataza wote wawili wasile matunda ya mti uliokatazwa katika bustani walimoishi. Nyoka alimshawisi Hawa ale tunda la mti huo na kisha Hawa akamshawishi Adam ale pamoja naye. Hivyo, lawama zilimwendea Hawa kwa mfano “huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja name ndiye aliyenipa matunda ya mti huo nikala (Mwanzo, 3:12) na katika (Mwanzo 3:16) “…akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa Watoto; na tama yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Katika Quran takatifu uumbaji unazungumziwa katika sehemu nyingi mfano “kisha Mungu akasema akimwambia nabii Adam..Nawe Adam! Kaa peponi pamoja na meko, na kuleni mnapopenda, lakini msiukalibie mti huu msije kuwa miongoni mwa waliodhurumu nafsi zao. …Mola wenu hakuwakataza mti huu (kwa sababu hii) msije mkawa Malaika au kuwa miongoni mwa wakaao milele (Quran 7:19-23). Mitazamo yakinifu toka vitabu hivi viwili inatoa lawama kwa watu wote wawili (Adam na Hawa). Lakini katika Quran hakuna kipengele hata kimoja kinacho eleza kuwa Hawa ndiye alimshawishi Adam kula tunda au kwamba Hawa ndiye alikula tunda wa kwanza au Hawa ndiye alimpelekea Adam. Kwa mantiki hii Quran haimwiti Hawa mshawishi wa Adam kula tunda na Hawa si mlaghai wa mdanganyifu.
 Urithi wa Hawa
Taswira ya kuwa Hawa ni mshawishi iliyo ndani ya Biblia imeleta matokeo ya athari mbaya kwa kiasi kikubwa kwa wanawake katika mafundisho ya Uyahudi-Ukristo. Wanawake wote waliaminiwa kuwa wamerithi kutoka kwa mama yao Hawa wa Kibiblia mambo mawili: zambi zake na hila zake. Kwa hiyo, wanawake wote wakawa hawaaminiwi, madhaifu, uadlifu, na waovu. Kupatwa na hedhi, mimba, na kuzaa; vitu hivi vilizingatiwa kuwa ni adhabu ya uadilifu kwa dhambi ya milele ya kulaaniwa kwa jinsi ya kike.
Ili tufahamu vizuri ni naman gani mkanganyiko mbaya juu ya Hawa wa Ki-biblia ulivyokuwa kwa vijukuu vyake vya kike vyote tunalazimika kutazama maandiko ya baadhi ya Wayahudi na Wakristo muhimu sana wa kila zama. Tazama Agano la Kale na tuone dondoo kutoka katika kile kiitwacho Maandiko ya Busara ambayo kwayo tunakuta: “Naona uchungu sana kuliko uchungu wa kifo mwanamke ambaye ni ghiliba, ambaye moyo wake ni mtego na mikono yake ni minyororo. Mwanamume anayempendeza Mungu atamuepuka mwanamke huyo, lakini muovu atatekwa na mwanamke huyo… Wakati nilipokuwa naendelea kutafuta bila kupata, nilipata mwanamume mmoja wa kuaminika miongoni mwa maelfu, lakini sijapata hata mwanamke mmoja wa kuaminika miongoni mwa wanawake wote’’. (Ecclesiastes 7:26-28). Katika sehemu nyingine ya maandiko ya Kiyahudi ambayo yanapatikana katika Biblia ya Kikatoliki tunasoma: “Hakuna uovu unaotokea sehemu yeyote unaokaribiana na uovu wa mwanamke…. Dhambi huanza kwa mwanamke na tunamshukuru mwanamke kwa kuwa sote lazima tufe’’; (Ecclesiasticus 25:19-24).
Wataalamu wa dini ya Kiyahudi wameorodhesha laana tisa zinazowatesa wanawake ikiwa ni matokeo ya Kuporomoka: “Yeye ametoa laana tisa na kifo kwa mwanamke: Mzigo wa damu ya hedhi na damu ya bikra; mzigo wa kubeba mimba; mzigo wa kuzaa; mzigo wa kulea watoto; kichwa chake kinafunikwa kama vile mtu yupo katika maombolezo; mwanamke anatoboa masikio yake kama vile mtumwa wa kudumu au mjakazi ambaye anamtumikia bwana wake; mwanamke asiaminiwe kuwa ni shahidi; na baada ya yote hayo… kifo.”  Wayahudi wakiume wa Kiorthodoksi katika sala zao za kila siku asubuhi wanakariri “Baraka ni za Mungu mfalme wa ulimwengu wote kwa kuwa hajaniumba mwanamke”; Wanawake, kwa upande mwingine, wanakariri “shukraniii ni za Mungu kila asubuhi kwa kuniumba kulingana na Matakwa yake (Ecclesiasticus25:19-24).”
Sala nyingine inayopatikana katika vitabu vingi vya sala za Kiyahudi ni: “Shukrani ni za Mungu kwa kuwa hajaniumba nikiwa mtu wa mataifa (mtu ambaye si Myahudi).
Leonard and Swidler (1976:115) katika kazi yao iitwayo “Women in Judaism; the Status of Women in Formative Judaism” inasema: “Shukrani ni za Mungu kwa kuwa hajaniumba mwanamke. Shukrani ni za Mungu kwa kuwa hajaniumba mjinga.” Ushahidi huu unaendelea kuweka wazi jinsi Vitabu vitakatifu vya kikristo na kiyahudi vinavyo wabeza na kuwabagua wanawake.

Hawa wa Kibiblia amechukua sehemu kubwa katika Ukristo kuliko katika Uyahudi. Dhambi yake imekuwa ni tegemeo kwa imani yote ya Kikristo kwa sababu itikadi ya Kikristo juu ya sababu za kazi ya Yesu Kristo Duniani imejengwa kutokana na maasi ya Hawa wa Biblia kwa Mungu. Hawa alifanya dhambi kisha alimshawishi Adam afuate mkumbo wake. Kwa hiyo, Mungu aliwafukuza wote wawili watoke Peponi waende ardhini, ardhi ambayo imelaaniwa kwa ajili yao. Walirithisha dhambi yao, ambayo haikusamehewa na Mungu, kuwarithisha kizazi chao chote na kwa hiyo, binadamu wote wanazaliwa wakiwa na dhambi. Ili kuwatakasa wanadamu kutoka katika “dhambi zao za asili,” Mungu alilazimika kumtoa muhanga msalabani, Yesu, ambaye anazingatiwa kuwa ni mwana wa Mungu. Kwa hiyo, Hawa anabeba kosa lake, dhambi ya mumewe, dhambi ya asili ya binadamu wote, na kifo cha Mwana wa Mungu. Kwa maneno mengine, matendo ya mwanamke mmoja kwa nafsi yake yamesababisha kuangamia kwa binadamu.
Mt. Tertullian pia alikuwa butu mno kuliko Mt. Paulo, alipokuwa akiongea na ‘watawa wake awapendao sana kiimani, alisema: Je, kuna nini kwa mabinti zake? Hao nao ni wakosaji kama yeye na wanalazimika kutendewa kama alivyotendewa yeye. Sikiliza muono wa kuhuzunisha wa mtakatifu Paulo katika Agano Jipya: “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” (1 Timotheo2:11-14).

Ruether (1987:209) katika kazi yake ya For all the sayings of the Prominent Saints, see Karen Armstrong, The Gospel According to Woman anasema kwamba “Je, hivi hamjui kuwa nyinyi nyote ni akina Hawa? Hukumu, (Maelezo) ya Mungu juu ya jinsia yenu yanaishi katika zama hizi: uovu nao lazima uwe unaishi. Nyinyi ni mlango wa Shetani: Nyinyi ndio waondoaji kizuizi cha mti ulioharamishwa: Nyinyi ndio wa mwanzo kuacha sheria takatifu: Nyinyi ndio yule mwanamke aliyemshawishi mwanamume ambaye shetani alishindwa kupata ujasiri wa kutosha kumvamia; niyinyi ndio mlioharibu kirahisi picha ya Mungu. Kwa sababu ya dhambi zenu hata Mwana wa Mungu amelazimika afe.” Mt. Augustine alikuwa ni mwaminifu kwa waliomtangulia, alimuandikia rafiki yake: “Hakuna tofauti kwa mwanamke awe mke au mama, ataendelea kuwa ni Hawa tu ambaye ni mshawishi kwa hiyo, lazima tujihadhari na mwanamke yeyote yule… Nimeshindwa kupata faida ya mwanamke kwa mwanamume, ukitoa tendo la mwanamke kuweza kuzaa watoto kadri mmewe atakavyo mzalisha.”

Baada ya karne kadhaa, Mt. Thomas Aquinas aliendelea kuamini kuwa wanawake ni wasaliti: “Kwa mintarafu ya tabia ya kimaumbile ya kila mmoja, mwanamke ni masaliti na ni mwanaharamu, kwa nguvu iliyo hai, kwa mbegu ya mwanamume inaelekea kutoa tunda lenye kufanana kikamilifu na jinsia ya kiume; huku tunda la mwanamke linakuja kutoka katika dosari ndani ya nguvu iliyohai au kutoka katika baadhi ya malighafi mbovu, au hata kutoka baadhi ya athari za nje.” Mwisho, mwanamageuzi mashuhuri Martin Luther hajaona faida yoyote kwa mwanamke ispokuwa kuleta watoto wengi duniani kwa kiasi kinachowezekana bila kujali athari mbaya zozote: “Kama watachoka au kufa, hakuna tatizo. Waache wafe kwa kuzaa, kwani hiyo ndio sababu ya kuwepo kwao.” Tena na tena wanawake wote ni wa kuadhiriwa kwa sababu ya taswira ya Hawa ambaye ni mlaghai, shukrani zende kwa fikra iliyopo katika kitabu cha Mwanzo. Kwa muhtasari, itikadi ya Kiyahudi-Kikristo juu ya Mwanamke imetiwa sumu kwa imani ya kuamini dhambi ya asili ya Hawa na watoto wake wa kike.  
Katika Quran maandiko yanasema: “Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu; na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani; na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii; na wanaume wasemao kweli, na wanawake wasemao kweli; na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri; na wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea; na wanaume wanaotoa Zaka na sadaka na wanawake wanaotoa Zaka na sadaka, na wanaume wanaofunga; na wanawake wanaofunga; na wanaume wanaojihifadhi tupu zao; na wanawake wanaojihifadhi; na wanaume wanaomtaja Mungu kwa wingi; na wanawake wanaomtaja Mwenyezi Mungu; amewaandalia msamaha na ujira mkubwa…” (Quran 33:35) “Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake ni marafiki kwani huyaamrisha yaliyo mema na huyakataza yaliyo mabaya na husimamisha sala na hutoa Zaka na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake…   Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. (Quran 9:71) “Mola wao Akawakubalia (maombi yao kwa kusema): “Hakika Mimi sitapoteza juhudi (amali) ya mfanya juhudi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, (kwani nyinyi) ni nyinyi kwa nyinyi….” (Quran 3:195). “Afanyaye ubaya hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake na afanyaye mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Mwislamu, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila hisabu.” (Quran 40:40)
 
 Mabinti Wanaotia Aibu
Kwa hakika, Biblia inaeleza juu ya unyanyasaji wa jinsia ya kike kuanza punde tu anapozaliwa mwanamke. Kwa mfano, Biblia inaeleza kuwa kipindi cha mama aliyezaa kuwa si msafi kwa mujibu wa sheria za kidini ni mara mbili ya urefu wa kawaida ikiwa mtoto atakuwa mwanamke kinyume na mwanamume. (Mambo ya Walawi 12:2-5). Biblia ya Kikatoliki inaeleza kikamilifu kuwa: “Kuzaliwa kwa binti ni hasara” (Ecclesiasticus 22:3). Kinyume cha maelezo haya yanayotia mshtuko na kupaza roho, watoto wa kiume wanapokea sifa za kipee: “Mwenamume anayemuelimisha mwanawe wa kiume atahusudiwa na maadui zake” (Ecclesiasticus 30:3).

Wanazuoni wa Kiyahudi wameamrisha Wayahudi wa kiume wazaliane watoto wengi ili waendeleze kabila la Kiyahudi. Wakati huo huo, hawafichi upendeleo wao wa wazi kwa watoto wa kiume: “Ni uzuri kwa wale wote ambao watoto wao ni wa kiume lakini ni ubaya kwa wale wote ambao watoto wao ni wanawake”, “Anapozaliwa mtoto wa kiume, watu wote wanashangilia…. na anapozaliwa mtoto wa kike watu wote wanahuzunika” na “wakati mtoto wa kiume anapokuja duniani, amani inakuja duniani…” Wakati mtoto wa kike anapokuja duniani hakuna kitu kinachokuja.

Elimu kwa Wanawake
Moyo wa Uyahudi ni Torati, ambayao ni sheria. Hata hivyo, kulingana na kitabu Talmudi, (kitabu muhimu sana kwa Waislam), kinasema: “wanawake hawaruhusiwi kujifunza Torati.” Baadhi ya wanazuoni wa Kiyahudi kwa ukali wametangaza kuwa “ni bora kuyaacha maneno ya Torati yaunguzwe moto kuliko kusomwa na mwanamke” na “Yeyote atakayemfundisha Torati binti yake amemfundisha uchafu.” “Mwenyezi Mungu amekwishasikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” (Quran 58:1). Aidha Watoto wa jamii ya kiislamu wanapaswa kujifunza elimu akhera na sio elimu dunia maana ufalme wa Alah (Mungu) si kwa mambo ya kidunia.
Mtazamo wa Mt. Paulo katika Agano jipya anasema: “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama vile inenavyo Torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa” (Wakorintho wa Kwanza 14:34-35). Vipi mwanamke ataweza kujifunza ikiwa haruhusiwi kuongea? Vipi mwanamke atakua kiakili ikiwa amelazimishwa kuwa katika hali ya utiifu kikamilifu? Vipi mwanamke ataweza kujipanua upeo wake wa kielimu ikiwa chanzo chake cha pekee cha kupata elimu ni mumewe tu akiwa nyumbani?
Mama mmoja aitwaye Khawlah akawa na wakati mgumu sana. Bibi huyo akaenda moja kwa moja hadi kwa Mtume wa Uislamu ili kutetea kesi yake. Mtume (S.A.W) alikuwa na rai ya kumtaka bibi huyo awe mtulivu kwa kuwa hakuna njia ya kutatua tatizo hilo kwa wakati huo. Khawlah akaendelea kujadiliana na Mtume (S.A.W) akijaribu kuokoa ndoa yake iliyotundikwa. Punde tu, Quran ikaingilia kati; na maombi ya Khawlah yakakubaliwa. Hukumu takatifu ikakomesha tabia hiyo mbaya sana. Sura moja kamilifu (sura ya 58) ya Quran inaitwa “Almujadilah” au “mwanamke ambaye amefanya mjadala” iliitwa hivyo kwa ajili ya tukio hilo: Mwanamke katika itikadi ya Quran anayo haki ya kupinga rai, hata kama ni rai ya Mtume wa Uislam (S.A.W). Hakuna mwenye haki ya kumnyamazisha Mwanamke. Mwanamke hayupo chini ya amri ya kumtaka mumemewe awe ndiye marejeo yake ya pekee katika masuala ya kisheria na kidini.

Mwanamke Mwenye Hedhi

Sheria na hukumu za Kiyahudi juu ya hedhi ya wanawake ni kali mno. Agano la kale linamchukulia mwanamke yeyote mwenye hedhi kuwa si msafi na ni najisi. Zaidi ya hayo unajisi wake “unaambukiza” wenginewe vile vile. Mtu yeyote au kitu chochote atakachokigusa kitanajisika kwa siku nzima: “Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni. Na kitu cho chote akilaliacho katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho akiketia kitakuwa najisi. Mtu ye yote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. Mtu yeyote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni. Kwamba, ni katika kitanda au cho chote alichokilalia huyo mwanamke atakapokigusa kitu hicho atakuwa najisi kwa wakati huo na hata jioni (Law, 15:19-23). Kwa sababu ya maumbile yake ya kutia najisi; mwanamke mwenye hedhi mara nyingine alipelekwa uhamishoni ili kuepusha uwezekano wowote wa kukutana naye. Hupelekwa nyumba maalumu ziitwazo “nyumba ya wasio wasafi” kwa kipindi chote cha hedhi yake. Zaidi ya hayo, mume wa mwanamke mwenye hedhi alizuiwa kuingia sinagogini kama atachafuliwa na mkewe tena hata kwa mavumbi yaliyo chini ya miguu yake.
Kasisi yeyote ambaye mkewe, bintiye, au mamaye ni mwenye hedhi hakuruhusiwa kuhubiri baraka sinagogini. Talmudi inamchukulia mwanake mwenye hedhi ni “mauti” hata kama hakuna mafungamano ya kimwili: “Walimu zetu wa dini ya Kiyahudi wametufunza… kama mwanamke mwenye hedhi atapita kati ya (wanaume) wawili, ikiwa ni mwanzoni mwa hedhi yake, mwanamke huyo atamnyonga mmoja wao, na kama akiwa mwishoni mwa hedhi yake, atasababisha ugomvi kati ya wanaume hao” (Bpes.111a.).

Haki ya Kutoa Ushahidi
Kadhia nyingine ambayo Quran na Biblia hazikubaliani ni kadhia ya mwanamke kutoa ushahidi. Ni kweli kuwa Quran imewafunza waumini ambao wanashughulika na mikataba ya kibiashara wawe na mashahidi wawili wa kiume au mwanamume mmoja na wanawake wawili (Quran 2:282). Hata hivyo, ni kweli kwamba Quran katika matukio mengine (baadhi) inakubali ushahidi wa mwanamke. Na kwa hakika ushahidi wa mwanamke unaweza ukawa ni bora zaidi kuliko wa mwanamume katika baadhi ya mambo.    
Kwa upande mwingine, katika jamii za kale za Kiyahudi wanawake hawakuruhusiwa kutoa ushahidi. Wanazuoni wa Kiyahudi waliwahesabu wanawake kuwa hawawezi kutoa ushahidi. Jambo hilo ni miongoni mwa laana tisa zinazowatesa wanawake wote kwa sababu ya “kuporomoka” (tazama sehemu ya Urithi wa Hawa). Katika Israeli ya leo, wanawake hawaruhusiwi kutoa ushahidi katika mahakama za kidini. Wanazuoni wanahalalisha sababu za kutoruhusiwa kwa wanawake kutoa ushahidi kwa kukariri (Mwanzo 18:9-16), pale ilipoeleza kuwa Sara mke wa Ibrahimu ameongopa. Wanazuoni wa Kiyahudi wanatumia tukio hili kama ni ushahidi wa kuwa wanawake hawana vigezo vya kuwa mashahidi. Hapa inapaswa izingatiwe kuwa, kisa hiki kilichosimuliwa na (Mwanzo 18:9-16) kimetajwa zaidi ya mara moja katika Quran bila ya kudokeza kama Sara aliongopa (Quran 11:69-74, 51:24-30). Katika Ukristo wa Kimagharibi, vyanzo viwili Ecclesiastical na sheria ya uraia viliwakataza wanawake wasitoe ushahidi hadi mwishoni mwa karne iliyopita.


Kama mwanamume atamuoa mwanamke kisha akamtuhumu kuwa si bikira, ushahidi wa mwanamke huyo hautokubaliwa. Wazazi wake watalazimika kuleta ushahidi wa ubikira wake mbele ya wazee wa mji. Na kama wazazi watashindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha utakatifu wa binti yao, binti huyo atapigwa mawe hadi afe mlangoni katika ngazi za nyumba ya babaye. Na kama Kama mwanmume atamtuhumu mkewe kwa uzinzi, ushahidi wa mwanamke huyo hautokubaliwa kabisa kabisa kwa mujibu wa Biblia. Mke anayetuhumiwa lazima akabiliwe na hukumu ya kuchunguzwa kwa kuteswa. Katika majaribio hayo, mke atakabiliwa na kanuni za kidini zikichanganyika na kufedheheshwa ambazo zitapendekezwa ili kuthibitisha uovu wake au utakatifu wake (Hesabu 5:11-31). Na kama atapatikana na hatia baada ya kuchunguzwa kimateso, mwanamke huyo atahukumiwa kifo. Na kama itagundulika si muovu, mumewe atakuwa hana hatia yoyote ya kumtendea vibaya mwanamke huyo.

“Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, kisha akimshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; angalieni amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumuacha siku zake zote. Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira, na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israel, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondo uovu katikati yako (Kumb. 22:13-21).
Uasherati
Uzinzi unazingatiwa kuwa ni dhambi katika dini zote. Biblia inatangaza adhabu ya kifo kwa wote wawili mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke (Law. 20:10). Uislam pia unatoa adhabu iliyo sawa kwa wote wawili mzinifu mwanamume na mzinifu mwanamke (Quran 24:2). Hata hivyo, ufafanuzi wa Quran juu ya uzinzi una tofauti sana na ufafanuzi wa Biblia.
Uzinzi, kwa mujibu wa Quran, ni kushiriki tendo la ngono nje ya ndoa kwa aliyeoa au aliyeolewa. Lakini Biblia inazingatia tendo la ngono nje ya ndoa kuwa ni uzinzi kwa mwanamke aliyeolewa. (Law. 20:10, Kum 22:22, Methali 6:20-7:27). “Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume alielala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli (Kum 22:22). “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa maana wametenda dhambi (Law, 20:10).

Kwa mujibu wa ufafanuzi wa Biblia, kama mwanamume aliyeoa atalala na mwanamke asiyeolewa, jambo hilo halichukuliwi kuwa ni uovu kabisa kabisa. Mwanamume aliyeoa anayefanya ngono nje ya ndoa na mwanamke asiyeolewa si mzinzi na mwanamke asiyeolewa aliezini naye, pia, si mzinzi. Uovu wa zinaa unatendeka pale tu, mwanamume aliyeoa au asiyeoa, anapolala na mwanamke aliyeolewa. Kwa hali hii mwanamume anachukuliwa kuwa ni mzinifu, hata kama hajaoa, na mwanamke anachukuliwa kuwa ni mzinifu. Kwa ufupi, uzinzi ni uovu wa kingono unaomuhusisha mwanake aliyeolewa. Matendo ya ngono nje ya ndoa yanayomuhusu mwanamume aliyeoa si uzinzi kwa mujibu wa Biblia. Je, Kwa nini huu u-ndumilakuwili?. Kwa mujibu Insaiklopidia ya Kiyahudi, mke anazingatiwa kuwa ni miliki ya mume na uzinzi unatoa madaraka ya uvunjaji wa sheria kumvunjia mume kwa haki ya kipekee aliyonayo kwa mwanamke; mke kama miliki ya mume hana haki kama hiyo kwa mumewe.

Hadi hivi leo katika nchi ya Israeli, kama mwanamume aliyeoa atajitumbukiza katika ngono nje ya ndoa na mwanamke asiyeolewa, watoto wake kwa mwanamke huyo wanazingatiwa kuwa ni watoto wa halali wa ndoa. Lakini, kama mwanamke aliyeolewa atafanya ngono nje ya ndoa na mwanamume mwingine (si mumewe) aliyeoa au asiyeoa, watoto wake kwa mwanamume huyo si wa halali tu lakini pia wanazingatiwa kuwa ni watoto wa haramu na ni haramu kwa watoto huo kuoa au kuolewa na Myahudi yeyote ispokuwa aliyeitoka dini ya Kiyahudi na watoto wa nje Hiyo ndio maana, kama mwanamume atafanya ngono na mwanamke aliyeolewa, mwanamume huyo atakuwa amevunja mali ya mwanamume mwingine na, kwa hiyo lazima aadhibiwe (Jeffrey, 1990:170-177). Katazo hili linaendelea kwa vizazi vya mtoto huyo kwa madaraja ya vizazi mpaka uvundo wa uzinzi uthibitishwe kufifia (Quran 41-42). Kwa upande mwingine,  
Kula Kiapo na Kuweka Nadhiri
Nadhiri au kiapo cha mwanamke lazima kitimizwe na baba yake, kama atakuwa anaishi kwenye nyumba ya baba yake, au atimiziwe na mumewe, akiwa ameolewa. Kama baba/mume hajaidhinisha nadhiri ama kiapo cha binti yake au mkewe, viapo, ahadi, nadhiri na dhamana zote zilizofanywa na mwanamke huyo zinakuwa ni batili na ni kazi bure: “Lakini kama huyo baba yake akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika….” Na mumewe alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri Zake zote zitathibitika na kila kifungo alichofunga kitathibitika. (Hesabu 30:5-15). Kwa nini iwe maneno ya mwanamke hayashurutishwi kwake? Jibu ni lepesi: Ni kwa sababu mwanamke anamilikiwa na baba yake, kabla ya kuolewa, au na mumewe baada ya kuolewa. Utawala wa baba kwa binti yake ulikuwa ni dhahiri kwa upeo ambao, kama atataka, anaweza kumuuza! Na jambo hilo limeonyeshwa katika maandiko ya wanazuoni wa Kiyahudi kuwa: “Mwanamume anaweza kumuuza binti yake, lakini mwanamke hawezi kumuuza binti yake, Mwanamume anaweza kumchumbia binti yake, lakini mwanamke hawezi.”
Kushindwa kutekeleza kiapo ipasavyo, kilichoapwa na mwanamume au mwanamke, ni lazima alipe fidia kama ilivyotajwa katika Quran: “Mwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakukamateni kwa viapo mlivyoapa kwa nia mliyoifunga barabara. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha katikati mnachowalisha watu wa majumbani mwenu, au kuwavisha, au kumpa uungwana mtumwa, Lakini asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu (Quran 5:89). Wafuasi wa Mtume Muhammad (S.A.W) waume kwa wake, walikuwa wakiwasilisha viapo vyao vya kumtii, wao wenyewe. Wanawake, sawa na wanaume, walikuwa wanamuendea Mtume kila mtu mwenyewe na kula viapo vyao. “Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzusha tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana ahadi nao na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu.   
Mali za Mwanamke
Mafundisho ya Kiyahudi yanalichukulia jukumu la mume kwa mkewe kuwa linaanzia kutoka katika itikadi ya kuamini kuwa mume anammiliki mke kama anavyomiliki mtumwa wake. Itikadi hii imekuwa hoja nyuma ya undumilakuwili katika sheria ya uzinzi na nyuma ya uwezo wa mwanamume wa kubatilisha viapo vya mkewe. Itikadi hii pia inahusika katika kumzuia mke asisimamie mali yake au mapato yake. Mwanamke wa Kiyahudi mara tu anapoolewa, mwanamke huyo anapoteza kabisa kabisa usimamizi wa mali zake na mapato yake, na kuchukuliwa na mumewe. Wanazuoni wa Kiyahudi wanatetea haki ya mwanamume kwa mali ya mkewe kama ni matokeo ya kummiliki kwake mke huyo: “Mtu anapokuwa mmiliki wa mwanamke je, jambo hilo halipelekei kuwa mtu huyo atakuwa mmiliki wa mali za mwanamke huyo vile vile?” na “Na mwanamume ajitwalie mwanamke je, hatajitwalia mali za mwanamke huyo vile vile? Ukweli wa mambo ni kwamba mali za mwanamke wa Kiyahudi zina maana ya kuwavutia wachumba.
Familia ya Kiyahudi inatoa fungu la binti yao katika kiwanja/shamba la baba yake litumiwe kama mahari atoayo mke ili aolewe. Mahari hiyo ndiyo sababu iliyowafanya mabinti wa Kiyahudi wewe ni balaa lisilotakiwa kwa baba zao. Baba analazimika kumlea binti yake kwa miaka mingi kisha aandae ndoa yake kwa kutoa mahari kubwa. Kwa hiyo, msichana katika familia ya Kiyahudi amekuwa ni dhima isiyo na kikomo na sio rasilimali.Kwa hiyo, ndoa imesababisha mwanamke tajiri sana awe hana kitu! Talmudi inachambua hali ya kiuchumi ya mwanamke kama ifuatavyo: “Vipi mwanamke awe na chochote; chochote ambacho ni chake kinamilikiwa na mumewe? Kwa mume kile ambacho ni chake basi hicho ni chake na kwa mwanamke kile ambacho ni chake basi hicho ni cha mwanamume vile vile. Ni lazima iongezwe kuwa mume vile vile analazimika atoe mahari kwa bibi harusi, lakini kwa mara nyingine tena mume huyo huyo ndio mmiliki halali wa zawadi hiyo kwa muda wote wa ndoa yao.

Ukristo, hadi hivi karibuni, umekuwa unafuata mafundisho yale yale ya Kiyahudi. Mamlaka za sheria za raia katika himaya ya Ukristo wa Kiroma (baada ya Constantine) zinaomba maafikiano ya mali kama ni sharti la kutambuliwa kwa ndoa. Familia zinawapa mabinti zao mahari za ziada kama matokeo ya sheria hiyo. Chini ya sheria ya urai, mke ametajwa kuwa anarudishiwa mahari yake kama ndoa imebatilishwa, ila kama mwanamke huyo ni mzinzi, katika hali hii, mwanamke huyo ananyang`anywa haki yake ya mahari ambayo imesalia kuwa mikononi mwa mumewe.24 Chini ya sheria ya kanuni na sheria ya uraia mwanamke aliyeolewa katika dini ya Ukristo wa Ulaya na Marekani ameshapoteza haki za mali zake, hali hii ilikuwa inaendelea hadi mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini. Kwa mfano, haki za wanawake chini ya sheria ya Uingereza zilizotungwa na kuchapishwa 1632. Miongoni mwa haki hizo ni: “Cha mume ni chake.  
Mke sio tu anapoteza mali zake katika ndoa, pia anapoteza utu wake. Mumewe anaweza kubatilisha uuzaji au zawadi iliyotolewa na mke kwa kuwa haina sharti lenye thamani kisheria. Mtu yeyote atakayeingia mkataba na mke wa mtu anachukuliwa kuwa ni haramia kwa kushiriki katika ulaghai. Zaidi ya hayo, mwanamke hawezi kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake mwenyewe, wala hawezi kumshitaki mumewe. Mwanamke aliyeolewa alikuwa anatendewa kama vile ni mtoto mchanga katika jicho la sheria. Kirahisi kabisa, mke alimilikiwa na mumewe na kwa hiyo anapoteza mali zake, utu wake kisheria, na jina lake la kifamilia.
 
Mali na pato la mke vipo chini ya utawala wake kikamilifu na ni kwa ajili ya matumizi yake peke yake, na mutumizi ya watoto, ni jukumu la mumewe. Quran imeelezea msimamo wake juu ya mada hii kwa uwazi kabisa: “Na wapeni wanawake mahari yao, hali ya kuwa ni hadiya (aliyowapa Mungu). (Lakini hao wake zenu) wakikupeni kwa radhi ya nafsi zao kitu katika hayo (mahari) basi kuleni kwa furaha na kunufaika. (Quran 4:4). Bila kujali huyo mke ni tajiri kiasi gani, mwanamke halazimishwi kuwa mchumiaji mwenza wa mwanamume kuihudumia familia ispokuwa kama atajitolea mwenyewe na kuamua kufanya hivyo.

Talaka
Hizi dini tatu zina tofauti zilizo wazi kimtazamo juu ya talaka ambapo Ukristo unapinga talaka moja kwa moja. Agano Jipya kwa kauli moja linapigania ndoa isiyotanguka. Inasemekana kuwa Yesu amesema: “Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe, ispokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. (Matayo 5:32). Ukamilifu huo ulio mgumu kutekelezeka na usiobadilika bila ya shaka si jambo la hakika. Jambo hilo linaibua dhana ya ukamilifu wa kimaadili ambao haufikiwi na jamii ya kibinadamu. Wakati wanandoa wanapogundua kuwa ndoa yao haiwezi kuendelea, tendo la kuharamisha talaka haliwatendei wema wowote wanandoa hao. Kuwalazimisha wanandoa wanaochukiana waishio kwa ubaya wakae pamoja kinyume na matakwa yao ni jambo lisilo na maana yeyote wala si la haki.
Si ajabu ulimwengu wa Wakristo wote unalazimisha kuruhusiwa kwa talaka. Wayahudi, kwa upande mwingine, wanaruhusu talaka hata ikiwa bila sababu. Agano la kale linampa mume haki ya kumtaliki mkewe hata kama hana kosa au kwa kuwa hampendi tu. “Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo asiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi.” (Kum 24:1-4) Aya iliyo hapo juu imesababisha mjadala mkali kwa Wanazuoni wa Kiyahudi kwa sababu ya kutokubaliana kwao juu ya tafsiri ya maneno. “Uovu, chuki, kutia aibu, tabia mbaya” na “kutopenda” yaliyotajwa katika hizo aya. Kitabu cha Talmudi kinasajili rai zao zilizotofauti tofauti: “Madhehebu ya Shamai inakamata kuwa mwanamume haruhusiwi kumwacha mkewe ila kama atampata na hatia ya uzinifu, huku madhehebu ya Hillel yanasema kuwa mwanamume anaweza kumwacha mkewe hata kama huyo mwanamke amevunja kibakuli cha mumewe. Na mwanazuoni Akiba anasema mwanamume anaweza kumwacha mke hata kama kwa sababu nyepesi ya kwamba amempata mwanamke mwingine aliyemzuri sana kuliko wa kwanza” (Gittin, 90a-b).
Agano Jipya linafuata rai ya Shamaites huku sheria ya Kiyahudi imefuata rai ya (Hillelites & Akiba, 1962). Tangu kuenea kwa rai ya Hillelites, imekuwa ni mafundisho yasiyokeukwa kwa sheria ya Wayahudi ya kuwapa uhuru wanaume wa kumuacha mkewe bila ya sababu yoyote. Agano la Kale sio tu linampa mume haki ya kumtaliki mkewe “aliyemuhuzunisha” lakini pia linazingatia kumwacha “mke muovu” ni lazima: “Mke mbaya analeta fedheha, muono wa kuhuzunisha, na maumivu ya moyo. Mgoigoi wa mkono na mdhaifu wa goti ni mwanamume ambaye mkewe ameshindwa kumfurahisha. Mwanamke ni dhambi ya asili, na kupitia kwake sote tutakufa. Usiache tangi lenye ufa kuchimba au kumruhusu mke mbaya asema atakacho. Na kama mwanamke huyo hakubali utawala wake, mwache na mfukuze.” (Ecclesiasticus 25:25). Talmudi imesajili matendo maalumu kadhaa ya wake wanaolazimika kuachwa na waume zao: “Kama mwanamke atakula mitaani, kama atakunywa kwa pupa mitaani, kama atanyonyesha mtaani, kwa matendo hayo yote mwanazuoni Meir amesema kuwa mwanamke huyo lazima aachane na mumewe” (Git. 89a). Vile vile Talmudi imefanya jambo hilo kuwa ni mamlaka ya kumuacha mwanamke mgumba (ambaye hazai kwa kipindi cha miaka kumi): “Mwanazuoni wetu ametufundisha: Kama mwanamume amejitwalia mke na kuishi nae kwa miaka kumi na mwanamke huyo hajazaa mtoto, mwanamume huyo amuache mke huyo” (Yeb. 64a).

Wake, kwa upande mwingine, hawawezi kutoa talaka chini ya ya sheria ya Kiyahudi. Mke wa Kiyahudi, hata hivyo, anaweza kuomba talaka mbele ya mahakama ya Kiyahudi huku akithibitisha sababu nzito ya kufanya hivyo. Ni nafasi ndogo sana apewayo mke ili aweze kuomba talaka. Miongoni mwa nafasi hizo ni: ikiwa mumewe ana ugonjwa mbaya au ugonjwa wa ngozi, mumewe akishindwa kutekeleza wajibu wa ndoa. Hiyo mahakama inaweza kuunga mkono madai ya mke ya kutaka talaka lakini haina uwezo wa kuvunja ndoa. Ni mume tu awezaye kuvunja ndoa kwa kumtoza mkewe faini ya talaka. Na mahakama inao uwezo wa kutoa adhabu ya viboko, faini, kifungo na kumtenga na sinagogi huyo mume ili kumlazimisha apokee malipo ya lazima ya kumtaliki mkewe. Hata hivyo, kama mume atakuwa mbishi vya kutosha, anao uwezo wa kutotoa talaka na kuendelea kubaki na mkewe bila ya mipaka. Na baya zaidi, ni kuwa, mume anao uwezo wa kumtelekeza mkewe bila ya kumpa talaka na kumuacha akiwa si mwolewa wala si mtalikiwa. Na huyo mume anaweza kuoa mke mwingine au hata kuishi na kimada bila ya ndoa na kupata watoto kwa huyo kimada, (watoto hao wanahesabiwa kuwa ni wa halali katika sheria za Kiyahudi). Mke aliyetelekezwa, kwa upande mwingine, haruhusiwi kuolewa na Myahudi mwingine, kwa kuwa yeye ni mke wa mtu kisheria na hawezi kuishi na mwanamume mwingine kwa sababu atahesabiwa kuwa ni mzinifu na watoto wake kwa huyo mwanamume mwingine pia si wa halali kwa vizazi kumi.

Mwanamke mmoja alimuendea Mtume Muhammad (S.A.W) akitaka kuvunjwa kwa ndoa yake, akamwambia Mtume kwamba yeye hana lalamiko lolote dhidi ya tabia au hali ya mumewe. Tatizo lake la pekee lilikuwa ni kuwa hampendi huyo Kama mume atavunja ndoa kwa kumtaliki mkewe, hatorudishiwa chochote miongoni mwa mahari aliyotoa kumpa mkewe. Quran imeeleza kuharamisha kwa mume aliyeacha mke asirudishiwe mahari bila kujali ughali au thamani ya mahari yenyewe: “Na kama mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, (yaani kumwoa mke mwingine na kumwacha huyo wa zamani), na hali mmoja wao (nae ndiye huyo anayemwacha) mumempa mrundi wa mali, basi msichukue chochote. Je, mnachukua kwa dhulma na kwa khatia iliyo wazi?” (Quran 4:20). Katika hali ya mke kuamua kumaliza ndoa, huyo mke anatakiwa arejeshe mahari kwa mumewe. Kurejesha mahari katika hali hii ni fidia ya uadilifu kwa mume ambaye anapendelea kuendelea na mkewe huku huyo mke anataka waachane. Quran imewafundisha waume wa Kiislamu wasichukue kitu chochote katika mahari walizowapa wake zao ispokuwa katika hali ya mke kuamua kuvunja ndoa: “…Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa (wake zenu), ispokuwa (wote wawili) wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu”.
Uislamu umempa mwanamke wa Kiislamu baadhi ya haki (chache): mwanamke anaweza kumaliza ndoa kupitia khulah na kufungua mashitaka ya kudai talaka. Mke wa Kiislamu kamwe hatokuwa mtundikwa na mume mkaidi. Na zilikuwa ni haki hizi zilizowashawishi wanawake wa Kiyahudi waliokuwa wakiishi katika jamii za Kiislamu za mwanzo za karne ya 7 C.E. watafute kupata malipo ya talaka kutoka kwa waume zao wa Kiyahudi kupitia mahakama za Kiislamu. Wanazuoni wa Kiyahudi walitangaza kuwa malipo hayo ni batili na hayafai. Ili kukomesha mwenendo huo, wanazuoni wa Kiyahudi walitoa haki mpya na marupurupu kwa wanawake wa Kiyahudi ili kujaribu kudhoofisha mvuto wa mahakama za Kiislamu. Wanawake wa Kiyahudi waishio katika nchi za Kikristo hawakupewa chochote katika marupurupu kama yale ya wenzao. Kwa kuwa sheria ya talaka ya Kirumi inayofanyakazi ilikuwa haina mvuto wa ziada kuliko sheria za Kiyahudi. Vile vile, Mtume, amesisitiza kuwa Waislamu wabora sana ni wale walio wabora kwa wake zao: Sasa, hebu acha tutazame namna Uislamu usivyopendelea talaka. Mtume wa Uislamu amewaambia waumini kuwa: “Jambo la halali linalomchukiza sana Mwenyezi Mungu ni talaka.”  
Mwanamume wa Kiislamu hatakiwi kumtaliki mkewe eti kwa kuwa hampendi. Quran inawafundisha wanaume wa Kiislamu wawe wema kwa wake zao hata katika hali ya hisia za kuvuvuwaa au hisia za kutompenda: “….Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake. (Quran 4:19) Mtume Muhammad (S.A.W) ametoa mafundisho kama hayo: “Muumini wa kiume asimchukie muumini wa kike, kama hapendi moja ya tabia zake atapendezwa na nyinginezo” (Muslim) (David, 1896:125-126). “Mkamilifu wa imani miongoni mwa waumini ni yule mbora wao kitabia na aliye mbora wenu kitabia ni yule mwenye tabia njema kwa mkewe.” (Tirmidhi) Hata hivyo, Uislamu ni dini ya vitendo na inatambua kuwa kuna wakati ndoa inakuwa ipo ukingoni karibu kuvunjika. Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni mwamuzi mmoja katika jamaa za mwanamume na mmoja katika jamaa za mwanamke. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa habari za siri na habari za dhahiri (Quran 4:34-35).
Mambo matatu ya kwanza kutajwa yajaribiwe kwanza. Na kama yameshindwa, ndipo inapotakiwa kutafutwa msaada wa familia. Ni lazima izingatiwe, kuwa aya za hapo juu zinaangaza, kuwa kumpiga mke mkaidi, ni kipimo cha muda mfupi ambacho kinakimbiliwa kikiwa ni hatua ya tatu tena katika hali ya kulazimika kufanya hivyo huku kukiwa na matarajio ya kuwa hiyo itakuwa dawa ya matendo maovu ya mke. Kama hilo litafaa, basi mume haruhusiwi kwa hali yoyote ile kuendelea kumsumbua mke kama ilivyotajwa kwa ufafanuzi katika aya hizo. Na kama njia hiyo imeshindwa, mume bado haruhusiwi kutumia tena njia hiyo na hapo ndipo njia ya mwisho ya suluhisho kwa msaada wa familia lazima iangaliwe. 
Kwa kuongezea, Mtume wa Uislamu amelaani mapigo yoyote yasiyo ya kiuadilifu. Baadhi ya wake wa Kiislamu walimshitakia Mtume (S.A.W) kuwa waume zao wamewapiga. Kwa kusikia hivyo, Mtume kwa dhahiri alisema kuwa: “Wale wafanyao hayo (kuwapiga wake zao) si wabora wenu.
Akina Mama
Agano la Kale katika sehemu nyingi linaamrisha wema na kutenda matendo ya pekee kwa wazazi na kuwalaani wale ambao hawawatendei wema. Kwa mfano, “Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa; amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.” (Mambo ya walawi 20:9) “…Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; bali mpumbavu humdharau mamaye.” (Mithali 15:20). Ingawa kumfanyia wema baba peke yake ndiko kulikotajwa katika baadhi ya sehemu; kwa mfano, “Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye; Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo” (Mithali 13:1). Mama peke yake ndiye asiyetajwa. Zaidi ya hayo, hakuna msisitizo wa kipekee juu ya kumtendea wema mama kama alama ya kufahamu vizuri tabu nyingi alizozipata wakati wa kujifungua na matatizo ya mtoto mchanga. Kando ya hayo, akina mama hawarithi kabisa kabisa chochote toka kwa watoto wao huku akina baba wanarithi mali. Huu ni uonevu na tafsiri yake ni kwamba mke hazalishi.

Mtu anaweza akadai kuwa Yesu alikuwa akijaribu kuwafundisha makutano yake somo muhimu sana ambalo ni kuwa uhusiano wa kidini si wenye umuhimu mdogo kuliko uhusiano wa kifamilia. Hata hivyo, Yesu alikuwa na uwezo wa kuwafundisha wasikilizaji wake somo hilo hilo bila ya kuonyesha huko kutomjali mama yake Ni vigumu kusema kuwa Agano Jipya ni maandiko yanayowataka watu wawafanyie wema akinamama. Kwa kulinganisha, mtu anaona kuwa Agano Jipya linahesabu kuwatendea wema akinamama kuwa ni kikwazo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa Agano Jipya, mtu hawezi kuwa Mkristo mzuri wa kutumainiwa kuwa yeye ni mfuasi wa Kristo ila amchukie mama yake. Inasemekana kuwa Yesu alisema: “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” (Luka 14:26) Kwa kuongezea, Agano Jipya linatoa picha ya Yesu kama ni mtu mwenye tofauti au asiyemuheshimu mama yake mzazi. Kwa mfano, wakati mama yake alipokwenda kumtafuta na huku Yesu akiwa anawahubiria makutano, Yesu hakujali wala hakutoka kwenda kumuona mama yake: “Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita. Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka; wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani? Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu” (Marko 3:31-35). Mwelekeo kama huo usio na heshima unatoa picha ya wakati alipokataa kuthibitisha maelezo yaliyotolewa na makutano yake ya kuibariki kazi ya mama yake ya kumzaa na kumlea: “Ikawa alipokisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisem, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika” (Luka 11:27-28). Ikiwa mama mwenye daraja ya bikira Maria ametendewa matendo yasio na heshima kiasi hicho, kama ilivyofafanuliwa na Agano Jipya, tena katendewa na mtoto mwenye daraja ya Yesu Kristo, sasa itakuwaje kwa mama wa kawaida wa Kikristo vipi atatendewa na wanawe wa Kikristo wa kawaida? Katika Uislamu, heshima, utiifu, na kutukuza kunaambatana na mfano ambao hauna kifani.

Quran inaweka umuhimu wa kuwatendea wema wazazi kuwa ni jambo la pili baada ya kumuabudu Mwenyezi Mungu Muweza: “Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa hishima (kabisa). Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme; “Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto.” (Quran 17:23-24) Quran katika sehemu kadhaa imeweka mkazo maalumu kwa kazi ya mama ya kuzaa na kulea: “Na tumemuusia mwanadamu (kuwafanyia ihsani) wazazi wake – mama yake ameichukuwa mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na (kumnyonyesha na kuja) kumwachisha kunyonya katika miaka miwili – ya kwamba unishukuru mimi na wazazi wako; marejeo yenu ni kwangu,” (Quran 31:14) Nafasi ya pekee ya akina mama katika Uislamu imeelezwa kwa umbuji (ufundi wa kupanga na kutumia maneno kwa ujuzi wa hali ya juu sana) na Mtume Muhammad (S.A.W): “Mtu mmoja alimuuliza Mtume: “Ni nani nimfanyie wema zaidi? Mtume (S.A.W) akamjibu: “Mama yako”. “Na nani anafuata?” Aliuliza yule jamaa. Mtume (S.A.W) akamjibu: “Mama yako”. “Na nani anafuata?” Aliuliza yule jamaa Mtume (S.A.W) akamjibu: “Mama yako”.  
Mirathi kwa Wanawake
Moja ya tofauti kubwa kati ya Quran na Biblia ni mitazamo yao juu ya mirathi ya wanawake kurithi mali za ndugu zao waliofariki. Mtazamo wa Kibiblia una maneno mafupi yaliyowazi na yalioelezwa na mwanazuoni Epstein: “Mafundisho yanayoendelea na yasiyovunjika tangu enzi za kuanza Biblia hayampi mwanamke, mke na mabinti haki ya kurithi mali ya familia. Katika mfumo mkongwe sana wa urithi, wanafamilia wa kike wanazingatiwa kuwa ni sehemu ya mali ya urithi na kuwa ni watu wa mbali kabisa na utu, kisheria wanarithiwa na kuwa wao ni kama watumwa. Wakati ambapo kanuni za Musa zinatoa mirathi kwa mabinti ikiwa hakuna mwanaumume. Lakini hata hivyo mke harithi hata katika hali kama hiyo.  Kwa nini wanafamilia wa kike wanachukuliwa kuwa ni sehemu ya urathi? Mwanazuoni Esptein ana jibu: “Wanawake ni miliki ya baba zao kabla ya kuolewa na ni miliki ya waume zao baada ya kuolewa.”
Ukristo umekuwa ukifuata sheria hizo hizo kwa muda mrefu. Sheria zote mbili za kikanisa na za kiraia kwa Wakristo zinazuia mabinti wasishirikiane na kaka zao katika urithi kutoka kwa baba yao. Kando ya hayo, wake walikuwa wananyimwa haki zote za kurithi. Sheria hiyo ya udhalimu sana ilidumu hadi mwishoni mwa karne iliyopita. Sheria za mirathi za Biblia zimeelezwa katika (Hesabu 27:1-11). Mke hapewi fungu lolote katika mirathi ya mumewe, huku huyo mume ndio mrithi wa kwanza wa kumrithi mkewe, tena hata kabla ya watoto wake. Binti anaweza kurithi kama tu hakuna mwanamume wa kurithi. Mama harithi kabisa kabisa huku baba akirithi. Wajane na mabinti, katika hali ya kuwepo watoto wa kiume, wamo katika huruma ya warithi wa kiume kwa kusaidiwa. Na hiyo ndiyo sababu wajane na mayatima wa kike wamekuwa ni miongoni mwa mafukara sana katika jamii ya Kiyahudi hapo kale.
 
Akina mama, wake, wasichana na madada wa Kiislamu wamepokea haki za kurithi miaka elfu moja na mia tatu kabla ya Ulaya kutambua kuwepo kwa haki hiyo. Mgawo wa urithi ni somo kubwa sana lenye maelezo kamili katika (Quran 4:7, 11, 12, 176). Sheria mama ni kuwa fungu la mwanamke ni sawa sawa na nusu ya Miongoni mwa wapagani wa Kiarabu kabla ya Uislamu, haki za kurithi zilikuwa kwa ndugu wa kiume tu. Quran imekomesha dhuluma zote hizo za kiutamaduni na ukawapa ndugu wote wa kike mafungu ya kurithi: “Wanaume wana sehemu katika mali wanayoyaacha wazazi na jamaa waliokaribia. Na wanawake (pia) wanayo sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliokaribia. Hizi ni sehemu zilizofaridhiwa na Mwenyezi Mungu katika (Quran 4:7) “…mwanamume ispokuwa katika hali ambazo mama anapata sawa sawa na baba” Hii sheria mama kama itachukuliwa kwa kutengwa kutoka katika sheria nyinginezo zinazowahusu wanaume na wanawake inawezekana kuonekana kuwa haina uadilifu. Ili kufahamu uwiano uliopo katika sheria hii, mtu lazima azingatie ukweli kwamba mujukumu ya kipesa kwa wanaume katika Uislamu yanazidi sana yale ya wanawake (Tazama kitengo cha mali za wanawake). Mume lazima ampe mkewe mali. Mahari hiyo ni mali ya huyo mke na inaendelea kuwa hivyo hivyo hata kama ataachwa hapo baadaye. Bi harusi hana wajibu wa kutoa kitu cha kumpa bwana harusi. Zaidi ya hayo, mume wa Kiislamu anachajiwa huduma za mkewe na wanawe. Mke, kwa upande mwingine, halazimishwi kumsaidia mumewe katika majukumu haya. Mali na pato la mke ni kwa ajili yake binafsi ila kile atakachojitolea kumpa mumewe. Kando ya hayo, mtu lazima atambue kuwa Uislamu kwa juhudi kubwa unahimiza maisha ya kifamilia.
 Wajane
Kwa sababu ya ukweli kwamba Agano la Kale halitambui haki yoyote kwa wanawake, wajane wamekuwa ni miongoni mwa watu masikini sana katika jamii ya Kiyahudi. Ndugu wa kiume ambao wamerithi mali yote ya mume aliyefariki ambayo ilikuwa apewe huyo mke kutoka katika mali hiyo. Hata hivyo, wajane hawana jinsi ya kujihakikishia matumizi hayo ambayo yameshasombwa, na wanaishi kwa kungojea huruma za watu wengine. Kwa hiyo wajane wamekuwa ni watu wa daraja la chini mno katika Israeli ya zamani na ujane ulizingatiwa kuwa ni alama ya kushuka hadhi sana (Isaya 54:4). Lakini hali mbaya ya mjane katika mafundisho ya Kibiblia inaenea hadi nga`mbo ya kutengwa kutoka katika mali ya mumewe. Kwa mujibu wa Mwanzo 38, mjane asiye na mtoto lazima aolewe na ndugu wa mumewe, hata kama atakuwa ameshaoa, kwa hiyo huyo ndugu azae mtoto kwa ajili ya kaka yake aliyefariki, jambo ambalo litaimarisha jina la ndugu yake na halitokufa. “Yuda akamwambia Onani, uingie kwa mke wa nduguyo ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao” (Mwanzo 38:8). Radhi za mjane kuridhia ndoa hiyo hazihitajiki. Mjane anatendewa kama ni sehemu ya mali ya mumewe aliyefariki, mke ambaye faida yake kuu ni kuhakikisha kizazi cha mumewe. Hii sheria ya Kibiblia bado inatumiwa katika Israeli ya leo. “Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye” (Walawi 21: 13-15).
Quran kwa ukali imeshambulia na kutokomeza mila hii ya kudhalilisha: “Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; ispokuwa yale yaliokwisha pita (Yaliyopita yamepita yasirejeshwe tena). Bila ya shaka jambo hili ni uovu na uchukizo na ni njia mbaya.” (Quran 4:22) Wajane na wanwake walioachwa wanadhalilishwa sana katika itikadi ya Kiyahudi kiasi ambacho Kuhani Mkuu hakuruhusiwa kumuoa mjane, mtalikiwa, au malaya: Quran kwa upande mwingine, haimchukulii mtu yeyote kuwa ni wa bahati wala ni wa mikosi. Wajane na watalikiwa wana uhuru wa kuolewa na mwanamume yeyote wamtakaye. Hakuna aibu inayomkumba mtalikiwa au mjane katika Quran: “Na mtakapowapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au tokaneni nao kwa wema. Wala msiwaweke kwa kuwapa dhara mkaruka mipaka. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu mwenyewe. Wala msizifanyie mzaha Aya za Mwenyezi Mungu. Na mkumbuke neema za Mungu zilizo juu yenu, na (khasa ile neema ya) kuteremshiwa Quran; na (kujuvywa) ilimu nyingine anazokuonyeeni. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.” (Quran 2:231) “Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na kuacha wake; hawa (wake) wangoje (wasiolewe) miezi minne na siku kumi. Na wanapofikia muda wao (wa kumaliza eda yao hiyo), basi si dhambi juu yenu kwa yale wanayoyafanyia nafsi zao (hao wanawake) kwa yanayowafiki (kufuata) Sharia. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. (Quran 2:234) “Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na wakawaacha wake, wawausie (mawarithi wao) kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kutolewa katika majumba waliyokuwamo ya waume zao.

Ukewenza
Mitala ni jambo la zamani sana linalopatikana katika jamii za kibinadamu nyingi na Biblia haijakemea mitala. Kwa kulinganisha, Agano la Kale na maandiko ya wanazuoni wa Kiyahudi mara kwa mara yanathibitisha haki ya mitala. Inasemekana kuwa mfalme Suleimani alikuwa na wake 700 na masuria 300. (1 Wafalme 11:3) Vile vile, mfalme Daudi, inasemekana alikuwa na wake wengi na masuria pia (2 Samweli 5:13). Agano la Kale lina sheria za kugawa mali za mume na kuwapa watoto wake kutoka kwa wake mbali mbali. (Kumb. 22:7).
Kizuizi cha pekee dhidi ya mitala ni kuharamishwa kumtwaa dada wa mkeo awe mke mwenza. (Walawi 18:18). Talmudi inashauri idadi ya mwisho kuwa ni wake wane 51 na Wayahudi wa Ulaya waliendelea kufanya mitala hadi karne ya kumi na sita. 
Makanisa ya Kiafrika na Wakristo wa Kiafrika mara nyingi wanawakumbusha wenziwao wa Ulaya kuwa Kanisa kuharamisha mitala ni mila za utamaduni na sio amri ya sheria thabiti ya Kikristo. Quran, vile vile imeruhusu ukewenza, lakini sio bila ya mipaka: “Na kama mkiogopa kutowafanyia uadilifu mayatima (basi ogopeni vile vile kutowafanyia uadilifu wanawake). Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, (maadamu mtawafanyia insafu) wawili au watatu au wanne tu. Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja tu, au (wawekeni masuria) wale ambao mikono yenu ya kiume imewamiliki. Kafanya hivi ndiko kutapelekea kutofanya jeuri” (Quran 4:3). Quran kinyume na Biblia, imeweka mipaka ya idadi ya wake hadi wanne tena chini ya masharti makali ya kuwatendea hao wake kwa usawa na uadilifu. Isifahamike kuwa Quran inawahimiza waumini wafanye mitala, au kuwa na mitala ndio ukamilifu. Kwa maneno mengine, Qurani “imesamehe” au “imeruhusu” mitala, na si zaidi, lakini kwa nini? Kwa nini mitala imeruhusiwa? Jibu ni lepesi: kuna maeneo na nyakati ambazo zinalazimisha jamii kufanya hivyo, pia malengo ya kimaadili ya kuwepo kwa mitala. Kama aya ya Quran iliyopo hapo juu ilivyoonyesha, mada hii ya mitala katika Uislamu haitofahamika peke yake nje ya shuruti za jamii na kuhusu mayatima na wajane.
Uchunguzi uliofanywa vijijini Kenya, wanawake 25 katika kila 27 wanapendelea ukewenza kuliko kuwa mke mmoja tu. Wanawake hao wanahisi kuwa ukewenza ni furaha na unafaida kama wake wenza watashirikiana na kusaidiana. Uchunguzi uliowahusisha zaidi ya wanawake elfu 6, wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 59, walio katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria wameonyesha kuwa asilimia sitini 60% ya wanawake hao watafurahi kama waume zao wataoa wake wengine. Ni asilimia 23% tu walioonyesha kukerwa na wazo la ukewenza. Asilimia 76% ya wanawake waliofanyiwa uchunguzi nchini Kenya walionyesha kukubali mitala (Bergin & Garvey, 1994:108-109). Ukewenza katika jamii nyingi za Kiafrika ni msingi unaoheshimika kwa kiasi ambacho baadhi ya Makanisa ya Kiporestanti yamekuwa yakiruhusu mitala. Askofu wa Kanisa la Kianglikana nchini Kenya ametangaza kuwa, “Ingawa kutokuwa na mitala huenda likawa ni jambo bora kwa kuelezea mapenzi kati ya mume na mke, Kanisa lazima lizingatie kuwa katika baadhi ya tamaduni mitala ni jambo linalokubaliwa na jamii na kuwa imani ya kuwa mitala ni kinyume na Ukristo si ya kufuatwa tena.
Baada ya uchunguzi yakinifu juu ya mitala ya Waafrika, Reverend David Gitari wa Kanisa la Kianglikana amehitimisha kuwa mitala ni bora kufanywa, na ndio Ukristo zaidi kuliko talaka na kuoa tena, ili kuwaonea huruma wake walioachwa na watoto wao.

Tatizo la ujinsia usio na uwiano limekuwa ni tatizo sugu nyakati za vita. Makabila ya Wahindi Wekundu, watu asilia wa Marekani walikuwa wanasumbuliwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la ujinsia usio na uwiano baada ya kumalizika vita wakiwa wameshindwa. Wanawake katika makabila hayo, ambao kwa hakika walifurahia hali ya kijamii ya hali ya juu, walikubali mitala kuwa ndio kinga bora zaidi dhidi ya matendo ya mahusiano yasiyo na heshima.
Ni jambo la kuvutia kujua kwamba katika mkutano wa kimataifa wa vijana uliofanyika Munich mwaka 1948 tatizo la ujinsia usio na uwiano nchini Ujerumani lilijadiliwa. Na ilipodhihirika kwa uwazi kuwa hakuna dawa iliyoafikiwa, baadhi ya washiriki walipendekeza mitala. Jibu la kwanza la washiriki wa mkutano huo lilikuwa ni mchanganyiko wa mshtuko na kero. Hata hivyo, baada ya uchunguzi wa kina juu ya pendekezo hilo, washiriki walikubaliana kuwa jambo hilo lilikuwa ndio utatuzi wa pekee. Kwa hiyo, mitala ilihitimishwa kuwa ni miongoni mwa mapendekezo ya mwisho ya mkutano huo.
Ulimwengu leo hii unamiliki silaha nyingi za maangamizi kuliko ilivyokuwa hapo kabla na makanisa ya Ulaya hivi karibuni au baadaye, yatalazimika kukubali mitala kuwa ndio njia pekee. Huonesha nia ya mwanamke mmoja kutokuwa mchoyo kwa mwanamme.
Billy Graham, mwinjilisti maarufu wa Kikristo ameutambua ukweli huo: “Wakristo hawawezi kuafiki suala la mitala. Kama sasa hivi Wakristo hawawezi kufanya hivyo, huko ni kujivunja wenyewe. Uislamu umeruhusu mitala kama ni utatuzi wa matatizo ya kijamii na umeruhusu kiwango maalumu cha uhuru wa kimaumbile ya kibinadamu lakini hayo yote yakiwa katika mzingo wa sheria kali zilizotambulishwa. Nchi za Kikristo zinaonyesha maonyesho makubwa ya ndoa za mke mmoja, lakini kwa hakika zinatekeleza mitala. Hakuna mtu asiye na mwanamke zaidi ya mkewe, kuna vimada vinavyowekwa katika jamii za Kimagharibi. Kwa hiyo, Uislamu ni dini ya kuheshimika yenye wema wa kimsingi, na umemruhusu Mwislamu aoe mke wa pili kama atalazimika, lakini pia umeharamisha vikali mno aina zote za ndoa za siri na uzinzi unaohusika ili kulinda uaminifu wa kimaadili wa jamii.”
Biblia, kwa upande mwingine na wakati mwingine inakimbilia ndoa za mitala za lazima. Mjane asiye na mtoto lazima aolewe na ndugu wa mumewe, hata kama tayari ameshaoa (tazama sehemu ya “Matatizo ya Wajane”), bila kujali radhi zake. (Mwanzo 38:8-10). Ifahamike kuwa katika jamii nyingi za leo hii suala la kutekeleza mitala ni chache mno kwa kuwa mwanya kati ya idadi ya jinsia mbili ya kike na ya kiume si mkubwa. Mtu, kwa kujiamini, anaweza kusema kuwa kiwango cha ndoa za mitala katika ulimwengu wa Kiislamu ni kidogo sana kulinganisha na kiwango cha ngono za nje ya ndoa katika nchi za Kimagharibi. Kwa maneno mengine, wanaume katika ulimwengu wa Kiislamu leo hii ni wapenda mke mmoja sana kuliko wanaume katika nchi za Kimagharibi. Ni jambo la kuzingatia kuwa, katika nchi zisizo za Kiislamu na za Kiislamu ulimwenguni, leo hii, kuna mitala ya kinyume cha sheria. Kujitwalia mke wa pili hata kwa radhi za mke wa kwanza, ni uvunjaji wa sheria. Lakini kwa upande mwingine, kumdanganya mke, bila kujua au kutoa radhi zake, ni jambo linalokubalika.

Kwa kurejelea Biblia takatifu, dhana ya ufeministi imejadiliwa na kisha kuibua harakati baada ya kuwepo kwa mifumo ya ukandamizwaji wa mwanamke kama inavyoonyeshwa katika vifungu mbalimbali:
1Timotheo 2:11-18 “mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna na kwa unyenyekevu. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanaume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa…”
1Wakorintho 11:7-10 “kwa maana kweli mwanaume haimpasi kufunika kichwa kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume. Maana mwanaume hakutoka katika mwanamke bali mwanamke katika mwanaume. Wala mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
1 Wakorintho 14: 34-36”Wanawake na wanyamaze katika Kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii kama vile inenavyo torati. Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa…”
Walaka wa kwanza kwa Wakolintho 14:34-35 unasema kuwa: Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
Fundisho kuu lilikuwa ni kusema kwamba imani pekee inatosha, hakuna haja ya matendo kwa kuwa ulimwengu wa kiroho haulingani na ulimwengu halisi wa kimwili. Kwamba Mungu ni roho na mambo yake ni ya rohoni. Kwamba binadamu ana sehemu mbili (Pyisical & Spiritual)  upande wa spiritual ndiko binadamu hufanana na MUNGU na anapaswa kuamini tu ikatosha. Upande wa pyisical ni masuala ya kimwili, na hayawezi kulingana na ya kiroho.
Mathayo 15:38 anasema kwamba, “…nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto”.  Hii in maana kwamba katika mkutano ule walikuwepo watu wake kwa waume lakini wanawake hawakuhesabika.
Harakati za ukombozi wa mwanamke katika kitabu kitakatifu cha Biblia (ufeministi)
Waamuzi 4:4-10 “Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efrahimu; wana wa Israeli wakakwea kwake awaamue…”. Maneno haya yanamsawiri mwanamke kama my mwenye kutoa maamuzi sahihi katika jamii yake.
Matendo ya Mitume 9:36-40 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani Paa) mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa…” Hii inaonesha ni kwa kiasi gani mwanamke anasawiriwa kuwa mtu mwenye matendo safi.
Marko 16:1-12 “Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalena na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka…” Wanawake ni watu wema na wakarimu kwani huweza kuwa huruma dhidi ya watu wanaopata mateso.
Esta 4:4-15 “Basi wajakazi wa Esta, na wasimamizi wake wa nyumba wakamjia, wakampasha habari; naye Malkia akahuzunika mno;…” Mwanamke ameitwa malkia ikiwa na maana ya mtawala. Hivyo mwanamke anaweza kuwa mtawala na akatawala nchi au eneo fulani kwa mafanikio makubwa.
Luka 10:38-42 “Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akisikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana,…”
Rejea hizi katika Biblia Takatifu zinaonesha ni kwa jinsi gani mwanamke alikwishaanza harakati za kujikomboa na kuanza kufanya mambo ambayo hayakutegemewa kufanywa naye mfano unabii, uongozi na utumishi.
Pamoja na hayo, wanawake ndani ya taasisi mbalimbali mfano kanisani, wanashiriki katika kuendesha semina na mafundisho mbalimbali mfano Mchungaji Rwakatale Getruda. Aidha, wamefanikiwa kuanzisha vyama mbalimbali ndani ya taasisi hizo mfano Dorikasi (chama cha wanawake makanisani) ambacho hujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi, WAWATA, BETHANIA na Karsimatiki.
Pia katika uenezaji wa injili kwa njia ya nyimbo, wanawake wanaonekana kuwa mstari wa mbele mfano Rose muhando, Bahati Bukuku, Christina Shusho na Jennifa Mgendi; kitu kinachodhihilisha mabadiliko na kujishughulisha kwao katika kutekeleza majukumu ya kijamii.

Dini ya uislam inatofautiana au kufanana na dini ya ukristo katika Ufeministi
Maandiko mbalimbali yanasisitiza kuwa fikra hii inapingana na itikadi na mafundisho ya Uislamu unaomtambua mwanamke na mwanaume kuwa wanakamilishana ndani ya familia na katika jamii. Itikadi za kifeministi zinakukosoa misingi ya mrengo huo katika mtazamo wa dini ya Uislamu ikilinganisha na ukristo. 
Pamoja na kwmba tumeona mjadala mrefu juu ya uthamini wa mwanamke katika dini za kikristo na uislam, bado mwanamke wa kikristo anayo haki ya kusimama mbele ya kanisa (waumini) na kuhubiri au kuendesha mafunzo ya biblia kwa watu wote mfano mchungaji Faith Rugazia, Halice Kabugumila na Getruda Rwakatale. Hii inadhihirisha harakati za ukombozi kwa wanawake wa kikristo tofauti na ilivyo kuwa katika Uyahudi. Katika upande wa waislam dhana ya ufeministi bado haijajidhihirisha kwani mwanamke wa kiislam hawezi kuongoza ibada ya waumini wote (wake kwa waume).  
Katika ukristo, suala la ufeministi limeibuliwa kwa kuonyesha ukombozi wa kifikra juu ya ndoa ya mke mmoja tofauti na waislamu ambapo mwanaume anaruhusiwa kuoa mwanamke zaidi ya mmoja. Hii inaondoa usawa kati ya mwanamke na mwanamme kwa sababu mwanamke hawezi kuwa na wanaume wawili ila mwanamme anaweza. Lakini pia, hali ya kuwa na mke mmoja inaashiria uchoyo kwa wanawake waliokwisha olewa maana takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume.

Ufeministi pia unaonekana au unajitokeza kwa wakristo pale ambapo wanawake huondokana na kasumba za kutochangamana na wanaume (kukaa pamoja katika ibada). Kwa sasa wanawake hukaa pamoja na wanaume wakibadilishana mawazo. Kwa upande wa dini ya kiislamu bado wanawake hawaruhusiwi kuchangamana na wanaume (kukaa pamoja wakati wa ibada) kwani hutenganishwa na ukuta kati yao na hivyo kutopata fursa ya kubadilishana mawazo kati yao na wanaume.
Hapo kale mwanamke alikuwa haruhusiwi kwenda ibadani kama yupo katika hedhi kwani aliitwa najisi. Lakini baada ya kugundulika kuwa ni badiliko la kawaida katika mwili wa mwanamke, sasa mwanamke wa kikristo anashiriki ibada. Harakati hizi bado hazijamfikia mwanamke wa kiislamu kwani yeye akiwa katika hedhi bado haruhusiwi kufunga na kufanya ibada msikitini.
Ufeministi kwa wanawake wa kikristo pia umeonekana pale ambapo wanakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika marehemu jambo ambalo ni tofauti kwa mwanamke wa kiislam. Wao hawaendi makaburini na hubakia nyumbani kana kwamba hawawezi kuweka udongo kaburini. Hili jambo linaonekana kwenda kinyume na usawa wa wanawake kwa wanaume. Fikilia kama mtu amefariki mikonooni mwa wanawake, je hatazikwa?
Suala la mfanano juu ya dhana ya ufeministi kati ya wakristo na waislam haliko wazi kutokana na kutokuwepo kwa harakati za kumkomboa mwanamke wa kiislamu ukiliinganisha ukristo baada ya ujio wa Kristo na kuachana na dini za kiyahudi zilizojikita katika sheria (torati). Hii ni kutokana na kuiamini Quran tukufu kwamba yaliyosemwa juu ya mwanamke yanapaswa kubaki vilevile kwani ni agizo la Mungu na sio ukandamizaji.  Bado dini ya uislam inalinganisha ukristo wakati wa sheria za Kiyahudi na si baada ya ujio wa Kristo.  
Hivyo basi, kwa kuirejelea biblia, ufeministi umekuwepo ili kumkomboa mwanamke au kumfanya aweze kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi mfano ushemasi na uchungaji, kuendesha semina na mihadhara mbalimbali, kuketi pamoja na wanaume ili kubadilishana mawazo, kushiriki shughuli za uchumi na ujenzi wa kanisa na kuilea jamii katika maadili yapasayo. 


Nadharia ya Ufeministi katika Fasihi ya Kiswahili
Wamitila (2006:160-161) na Ntarangwi (2004:52-56) wamebainisha ukandamizaji mbalimbali na harakati za ukombozi (Ufeministi) katika maisha ya jamii ya kiafrika kupitia katika kazi mbalimbali za kifasihi. Ni kweli kwamba kuna baadhi ya harakati za ufeministi zinakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika lakini baadhi ya harakati hizo zanasawiri maisha halisi ya mwanamke wa kiafrika kama ifuatavyo:
Katika kubainisha umuhimu wa mwanamke kutokana na mwanamke kukulia katika jamii zenye mfumodume Ufeministi Ufeministi umesawiliwa. Awali umuhimu wa mwanamke haukuonekana, ndiyo maana ikaanzishwa nadharia ya ufeministi ambayo yenyewe iligundua umuhimu wa mwanamke katika jamii. Umuhimu wake upo katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Mfano, katika nyanja ya kisiasa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora na mwenye ushauri. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994). Mwandishi anathibitisha hili anaposema:
Tunayo karibu miaka ishirini ya uhuru! Lini tutampata mwanamke wa kwanza awe waziri atakaye husishwa na maamuzi yatakayoongoza nchi yetu huko tuendako? Kumbe nguvu walizonazo wakina mama, uwezo wao wa kupambana, na kujihusisha kwao bila kutegemea kupata faida yoyote ni mambo ambayo hayahitaji tena kuthibitishwa. Wanawake wamewainua wanaume wengi kwenye ngazi za juu” (uk.82)
Mwanamke ameonekana kama mlezi wa familia katika jamii; Mfano, Ramatulayi katika riwaya ya Mariama Ba (1994) anailea familia yake kwani ameweza kulipa bili ya maji, umeme bila hata kumtegemea mwanaume. Mfano, mwandishi anasema:
Licha ya mzigo niliokuwa nao tangu zamani, nikaubeba na ule uliokuwa wa Modu. Ununuzi wa vyakula muhimu ulinishughulisha kila mwisho wa mwezi. Nilihakikisha kwamba sikuwa na upungufu wa nyanya au mafuta, viazi mviringo na vitunguu wakati ambapo vyakula hivi viliadimika sokoni… Nilikuwa mwangalifu kuzilipa bili za maji na umeme pindi zilipofika.” (uk.69)

Mtembei (2012) akimnukuu Angelica Baschiera (2003) anadai kuwa, Penina Muhando ni mmoja wa waandishi mashuhuri wanawake wanaojulikana nchini mwake na kimataifa. Kutokana na uandishi wake ameweza kupata tuzo ya kimataifa ya ‘‘Africa Education Journalism.’’Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mkabala wa Thieta kwa maendeleo katika Afrika ambamo ubunifu wa sanaa za maonesho hutumiwa na wananchi katika jamii zao kujiletea maendeleo yakiwamo ya kielimu.
Kawiche (2000) anasema kuwa, Penina Muhando ametumia ufeministi kumchora mwanamke. Amempa mwanamke nafasi ya kipekee. Pia, anatetea maslahi ya wanawake katika kazi zake za fasihi, kupitia wahusika aliowachagua kufikisha ujumbe. Anatambua umuhimu wa wanawake katika jamii. Pia, anadai kuwa, mwanamke kwenye suala la uongozi anaweza, ingawa anaweza kukandamizwa katika jamii za ulimwengu kwa sababu ni mwanamke na pia, mfanyakazi wa nyumbani, kama ilivyojitokeza katika tamthiliya zake za Hatia, Heshima Yangu na Nguzo Mama na mbinu zilizotumika kusawili. Watafiti mbalimbali wamehakiki tamthiliya za Penina Muhando, wengi wao wameelezea fani na maudhui na nafasi ya mwanamke katika jamii.
Kuondoa utegemezi wa wanawake kwa wanaume; lengo hili la ufeministi linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika. Kwa kuwa mwanamke wa Kiafrika anaonekana hana umuhimu katika jamii, pia anaonekana kuwa dhaifu ambaye hawezi kuiendesha familia yake bila msaada wa mwanaume hii ni kutokana na jamii nyingi kuendeshwa na mfumodume. Kihistoria wanawake wamekuwa ni tegemezi na wasaidizi wa wanaume, ni kweli kihistoria wanawake wamekuwa wategemezi na wasaidizi wa wanaume. Mfano katika tamthiliya ya Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) tunaona mhusika BI MOJA alivyokuwa akimtegemea mume wake na kutaka anunuliwe kanga. Mwandishi anasema:
“BI MOJA: (kwa Shaabani): Kama ulijua kufika sasa hivi nipe hela ya kanga bwana meli meli hii hainikosi leo utanipa hela hizo kanga nikakate. Mwezi wa tatu huu kanga sizijui.
Shaabani: Nimekuambia mimi hela sina. Sasa unataka nikaibe?”(uk.31-32)
Ni kweli kwamba mwanamke wa kiafrika amekuwa tegemezi katika jamii, kwani humtegemea mwanaume katika mambo mbalimbali ya kifamilia. Kwa mfano kutafuta au kununua mahitaji ya nyumbani kama vile chakula, mavazi yake na watoto wake au kulea watoto wake.
Lakini kupitia katika utendaji wa nadharia hii, wanawake wameweza kuhamasishwa katika Kujitegemea kufanya kazi na kujipatia pato halali.


Kuondoa ukandamizaji wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kijamii, kidini, kisiasa na kiuchumi. Jamii nyingi za Kiafrika zimejengeka katika mfumodume, hivyo basi jamii zinamkandamiza mwanamke kutokana na pingu hizo. Katika kulithibitisha hili waandishi wa kazi za fasihi nao hawakuwa nyuma kulizungumzia katika kazi zao na lengo ni kuondoa mfumodume uliojengeka muda mrefu katika jamii. Kwa upande wa kiutamaduni mwanamke ameonekana kukandamizwa kwa kuonekana hana mamlaka hata ya kurithi mali za mumewe au zake mwenyewe, badala yake hata akifiwa na mumuwe anapigwa, anafukuzwa na kudhalilishwa. Penina Muhando anayathibitisha haya katika tamthiliya yake ya Nguzo Mama kwa kumtumia BI SABA pale anaposema:
           “Akalia Bi Saba tena akalia
           Hana wa kumsaidia
           Mumewe kafa nduguze wakaja juu
           Pesa wamechukua senti tano haikubaki
Vyombo na nguo zote wakagawana
           Roho ilimpasuka Bi Saba kuwaona hao ndugu
           Walivyogombania mali wasiyoichuma…
Sasa juu ya yote haya wamerudi kufagia
Hata ufagio wamebeba
          Na lawama kumtupia eti pesa kazificha.” (uk.39)

Kuhamasisha mwanamke kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujiletea maendeleo yake binafsi. Kwa kuwa mwanamke amekuwa anarudishwa nyuma kwa kukandamizwa na mwanaume basi nadharia hii inampa nguvu ya kuendeleza na mapambano yake. Penina Muhando anayathibitisha haya kwa kumtumia BI PILI ambaye alikuwa anapika pombe ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha lakini mumewe SUDI alizichukua hela zote alizokuwa alizozipata. Kwa mfano, mwandishi anasema:
            “BI MSIMULIZI: Upishi wa pombe balaa ulimzushia
                                    Visa na mikasa Bi pili havikumuishia
                                   Pesa alizipata kutokana na hiyo pombe
                                   Lakini visa vya pombe hiyo pesa hazikufidia”
            SUDI:             (kwa Bi Pili) Nani kalewa? Umeninywesha wewe?
                                  Wee!hawara zako ndiyo wamekutia jeuri unaninyima pesa.
 Toa pesa sasa hivi (Anampiga) Bi Pili anakimbia huku   akilia.”          (uk.16)

Vilevile nadharia hii inaondoa mila potofu mfano mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kulazimishwa kurithiwa na kaka au ndugu wa mume pindi anapofiwa na mumewe. Mwandishi analithibitisha hili katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii pale anaposema:           
 “Tamsiri, zitapike hizo ndoto zako za kutaka kuniposa.
            Umeshakaa nazo kwa siku arobaini. Kamwe sitokuwa mkeo.”(uk.81)
Mwandishi anamchora mwanamke akimweleza mwanamme kuacha ndoto zake za kutaka kumposa mjane. Mwanamke mjane anaonesha kuwa imara katika maamuzi yake na kwenda kinyume na mila potofu.

Kwa upande wa kisiasa, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kuonekana hawezi kuwa kiongozi bora wa kuiongoza nchi ndio maana hata nafasi za wanawake zilikuwa chache huko bungeni. Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ mwandishi anayadhihirisha haya kwa kumtumia Ramatoulayi ambaye akilalamika kuhusu ukandamizwaji wa wanawake huko bungeni pale anaposema:
“Wanawake wanne, Dauda, wanne miongoni mwa wabunge mia moja uwiano gani huu wa kimzaha! Wala hakuna uwakilishaji wa kimkoa” (uk.81)
Wanawake wanaonekana kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi lakin bado hawakubaliani na uwiano uliopo kati ya wanawake na wanaume. Mwandishi anaonyesha wanawake kuendeleza mapambano dhidi ya kushika nyadhifa mbalimbali ili kuleta uwiano wa katika kutoa maamuzi juu ya maendeleo ya nchi yao.

Kwa upande wa kijamii, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kupigwa na mumewe bila sababu zozote za msingi. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (1988) kwa kumtumia mhusika Zakaria ambaye alikuwa anampiga mkewe bila sababu. Mwandishi anasema:
“Regina tangu aolewe hakuwa na raha! Alikuwa akisumbuliwa na kuteswa na mumewe kwa kosa lisilokuwa lake. Katika kijiji chote cha Namagondo hapakuwa na mwanamke aliyekuwa akipigwa karibu kila juma kama Regina. Wanawake wengi kijijini walijiuliza kwa nini hakutaka kumuacha bwana wake. wengine walimuonea huruma, wengi lakini walimuona mjinga.” (uk.3)

Pi, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kuonekana kuwa yeye ndiye mwenye majukumu ya malezi, kwa hiyo hata watoto wakiharibika anayelaumiwa ni mwanamke. Euphrase Kezilahabi analithibitisha hilo pale anaposema:
“Lete hiyo barua iko wapi? Pamoja na shilingi ulizopewa unafikiri sisi hapa maskini. Rosa alipigwa tena na tena. Makofi yalikwenda mfululizo hata damu zikamtoka puani na mdomoni. Baba nihurumie sitarudia tena… Zakaria hakujali alichukua fimbo na kuongozana na bintiye mpaka chumba cha watoto hali akinguluma lazima unioneshe barua hiyo unataka kuniletea umalaya wa mama yako hapa.” (Uk.7)

Vilevile, mtoto wa kike alikuwa anaonekana hana thamani katika jamii, na watoto wa kiume ndio waliopewa kipaumbele. Euphrase Kezilahabi anathibitisha haya katika riwaya ya Rosa Mistika kwa kumtumia Zakaria ambaye kabla ya kumpata mtoto wa kiume alikuwa anamnyanyasa sana mke wake lakini baada ya kujifungua mtoto wa kiume manyanyaso yaliisha na alimpenda sana mkewe. Mwandishi anasema:
“Zakaria alirudi nyumbani siku hiyo. Alikuwa amekwisha pata habari hizo njiani. Alimbeba mtoto. Alimpa pongezi mke wake. Regina sasa mji huu umekuwa wako. Asante Regina alijibu akitabasamu, alijiona anauwezo wa kuzungumza.”(uk.24)
Pamoja na hayo, lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwani mwanamke hakutakiwa kurithi mali yoyote pindi wazazi wake wanapofariki au mumewe anapofariki. Pia mwanamke kushindwa kupewa nafasi ya kutoa maamuzi yoyote katika masuala ya kiukoo. Kwa upande wa dini mwanamke anakandamizwa na kuonekana dhaifu hivyo kutokuwa na nafasi ya kuongoza waamini. Mfano, dini ya Kiislamu na baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
Wanawake wanafanya juhudi za kuzitambua na kuzibainisha dhamira kuu katika kazi zilizoandikwa na wanawake. Dhamira kuu ni dhamira inayomsukuma mwandishi katika kuandika kazi ya fasihi. Baadhi ya waandishi wanawake wameonesha dhamira kuu katika kazi zao ni kama:
Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) imebeba dhamira kuu ambayo ni ukombozi wa mwanamke. Ukombozi huo upo katika nyanja mbalimbali kama vile kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa. Mfano, mwandishi ameonesha wanawake wanavyojishughulisha katika kuinua uchumi wao, kwani walikuwa wakiuza vitambaa na kupika pombe. Mwandishi anathibitisha haya kwa kusema:
“BI TANO: Yaani mnasema mimi mvivu siyo nimezunguka mji mzima na zigo hilo halafu mnaniambia mimi mvivu. Nawaambia watu hawataki kununua au mnataka niwagawie bure.”
BI NANE: Lakini kwa nini wakatae kununua hivi, mbona vile vya mwanzo walivinunua? (uk.16).
Vilevile, Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994) suala la ukombozi wa mwanamke limejitokeza kama dhamira kuu. Ukombozi huu umejikita katika nyanja za kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kiuchumi.
Mfano, katika nyanja ya kijamii, mwandishi ameonesha jinsi ya kumkomboa mwanamke kielimu, pale anaposema:
…Shangazi Nabu anampeleka Nabu mdogo katika shule ya Kifaransa huko. Huko Nabu alijifunza aina mbalimbali za mapishi, matumizi ya pasi na zana za kutumia na kumenyea...” (uk.39)
Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa tangu mwanzo wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi, badala yake wanaume ndio waliochukuwa jukumu hilo la uongozi katika jamii. Pia, wanawake hawakuruhusiwa kupata elimu wakitegemezwa katika majukumu ya nyumbani na kuandaliwa kwenda kuolewa na kuja kuwa walezi wa familia.
Kuichunguza historia ya kifasihi ya jadi ya kike na kuwamulika waandishi wa kike waliotambua hali za wanawake na ambao wanaweza kuchukuliwa kama vielelezo kwa wasomaji wao. Hapo awali kazi mbalimbali za kifasihi za jadi za kike zilielezwa na waandishi wa kiume. Lakini nadharia hii imemulika waandishi wa kike wanaotambua hali mbalimbali na wameamua kuandika kazi mbalimbali ambazo zinaelezea matatizo ya wanawake. Mfano, katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwandishi anaelezea jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na kuachiwa majukumu ya kulea familia, kuchukuliwa mali zilizoachwa na waume zao baada ya kufariki. Mfano, mwandishi anasema:
…Haa! Shemeji mmerudi kuchukua hata kitanda! Hata sufuria! Nitalala wapi na nitapikia wapi jamani!” (uk.39)
SUDI: Haya nipe pesa ulizokwisha kupata.
BI PILI: Hee! Kwa nini nikupe?
            SUDI: Leta pesa upesi kabla sijakukong’ota.” (uk.13)
Mariama Bâ naye ni kielelezo kwani ameelezea matatizo mbalimbali yanayowakumba wanawake na namna wanavyokabiliana na matatizo hayo. Mfano mwandishi anasema:
“… Ramatulayi, Acha nisikilize mimi zaidi; Redio ya Kankan ilinifahamisha kwamba ulikataa kuolewa na Tamsiri. Ni kweli? Ndio.”  (uk.87)
 Mwandishi anaonesha jinsi mhusika Ramatulayi alivyojitambua na kukataa kurithiwa na Tamsiri, pia anamkataa Dauda ambaye alitaka kumrithi baada ya kufiwa na mume wake.
Kupitia lengo hili tunaona wanaufeministi wameongelea kuhusu wanawake tu ambao ni vielelezo katika kazi za fasihi, lakini wapo wanaume ambao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake. Mfano, Shaaban Robert aliyeandika Wasifu wa Siti Binti Saad.
Kudhihirisha kuwa kuna sifa fulani za kike na uzoefu fulani wa kike katika uwazaji, hisia, kutathmini, kujiangalia na kuuangalia ulimwengu wao wa nje. Uzoefu fulani wa kike unajitokeza katika uwazaji na jinsi wanavyousawiri uhalisi. Kazi ambazo zinamsawiri mwanamke kwa njia chanya, mfano ni riwaya ya Kiwasifu ya Shaaban RobertWasifu wa Siti Binti Saad.  Kuna mashairi kadhaa aliyoyatunga mwandishi ambayo yanaendeleza suala hili la uchanya wa wanawake katika jamii. Mfano wa usawiri wa wahusika linathibitishwa pale mwandishi anaposema:
            “Siti binti Saad,
Ulikuwa mtu lini,
Ulitoka shamba,
Na kaniki mbili chini,
Kama si sauti,
Ungekula nini?” (uk.22)

Hisia; mfano, katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii kupitia mhusika Daba alivyomwambia mama yake kuhusu Benetuu. Mwandishi anasema:
“Hasira ya Daba iliongezeka zaidi jinsi alivyozidi kuichambua hali ilivyokuwa. “Mama! Vunja ndoa yako! Achana naye mtu huyu hajatuheshimu, si wewe wala si mimi… sitaki kukuona unagombania mwanaume na mwanamke mwenye umri sawa na mimi.” (uk.52)

Mwanamke Kama Kiongozi Mwenye Maamuzi ya Sheria

Kupitia katika kazi ya Penina Mhando, tunagundua kuwa, mwandishi amemsawiri mwanamke kama kiongozi ambaye anajiamulia mambo yake mwenyewe. Ilielezwa katika majadiliano ya vikundi kuwa mfano mzuri unaojitokeza katika kitabu cha tamthiliya ya Nguzo mama ni pale Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri anapoamua kesi aliyoisikiliza kwa upande wa mtoa mashtaka tu wakati mshitakiwa hakuwepo. Bi Nane alihukumiwa kwa kosa la kuanzisha kikundi cha kupinga juhudi za Wanapatata za kuinua Nguzo Mama wakati si kweli. Lakini kwa kuwa Mwenyekiti hakutaka kumsikiliza Bi. Nane.  Mwenyekiti anatoa uamuzi wa kumwambia Bi. Nane avunje kikundi chake kwa kuwa hakikupata kibali cha ofisi ya mshauri na uamuzi ambao unamshangaza Bi. Nane. Mwandishi anasema,
Bi. Simulizi: Bi. Nane akawaza
Kumbe kazi hii ya uongozi au Uenyekiti
Inampa mtu uwezo wa kufanya
 Mambo kinyume cha kawaida
Vipi mtu akubali kutoa ushauri
Kutumia vitisho
Kufuatia maelezo ya mshitaki peke yake
Tena yaloyoelezwa wakati mshitakiwa hakuwepo?
Vipi mwenyekiti bila kamati
Akatoa ushauri katika mashtaka? (uk. 22)
Nukuu hizi zinaonyesha jinsi mwanamke alivyochorwa kama kiongozi mwenye kufuata sera ya udikteta katika jamii. U-dikteta wa mwanamke unatokana na kutokujiamini kama kiongozi hivyo huamua kufuata mbinu ya udikteta ili kuepuka changamoto za wale anaowaongoza.
Kupitia tamthiliya ya Nguzo Mama tunagundua kuwa, mwanamke amechorwa kama kiongozi ambaye anafuata sheria na kanuni, ingawa wananchi wa Patata wanamuona kuwa,ni mkiuka maadili na sheria za uongozi. Kwa mfano, mwenyekiti alichorwa akitumia nafasi yake ya uongozi kukiuka sheria. Mwandishi anaeleza,
 Bi. Simulizi:  Sheria hii Bi. Nane hajapata kusikia
Miaka kumi kazi kafanya
Mikutano kwa mamia kazini imefanyika
Na mwenyewe Bi. Nane Katibu hata Mwenyekiti kashakuwa hajawahi kusikia mikutano ya kikazi kwanza kupata kibali
….. kumbe wakubwa wakiwania vibaya kukuangusha 
Mbinu zote watatumia madaraka watachukua hata yale wasiyopewa (uk. 22-23)
Mwandishi wa tamthiliya hii amemsawiri mwanamke kwa upande hasi kwani anaonesha jinsi gani wanawake wanavyotumia vibaya nafasi za uongozi wanazozipata. Hivyo, si kila mwanamke au mwanamume anaweza kutumia vizuri nafasi yake katika uongozi.
Kukuza na Kuendeleza Hisia za Umoja wa Wanawake kama Kundi Linalodhulumiwa.
Kwa kuzingatia mtazamo kike mhusika Natala katika tamthiliya ya “Natala” ya Kithaka Mberia amesawiriwa kupitia katika tamthilia ya Natala ambapo tunamuona mhusika Gane akimtia moyo Natala kwa kumuunga mkono katika harakati za kutetea haki zake (uk 24) Gane anasema
Gane: Usivunjike moyo Natala mapenzi yako imara moyo wako wa kazi na nidhamu yako  thabiti   ni  baraka kubwa.
Baraka hizi zitakuwa jahazi la kuwafikisha watoto wako waendako, naamini hawataachwa nyuma na rika lao.
Natala: Ahsante kwa maneno yako ya kutia moyo.
Pia tunawaona wahusika Natala na Gane  ni wanawake wanaopambana  ili kuondoa mila na desturi potofu zilizopitwa na wakati,  dhana hii imejitokeza pale Natala alipokataliwa kupewa   mwili wa marehemu mume  wake na alipotaka kunyanganywa hati ya shamba.
Hivyo basi hata katika jamii za sasa wapo wanawake wanaoshirikiana katika kuondoa mila na desturi  potofu   zilizo pitwa na wakati   zinazowakandamiza wanawake.

Lengo hili la wanaufeministi linaendana na hali halisi ya wanawake wa Kiafrika, kwa kuwa mawazo ya mwanamke jinsi anavyojiwazia yeye mwenyewe au kuwawazia wanawake wenzake hutofautiana. Vilevile, hisia za mwanamke zinaweza kudhihirika katika maandishi na kuonesha jinsi wanavyowaza katika hali ya kawaida.
Ukweli ni kuwa msisitizo mkubwa kupita kiasi wa mfumo wa kiliberali juu ya mitazamo ya humanism, uhuru wa mtu binafsi, ubinafsi na kadhalika vimesambaratisha msingi wa maisha ya kifamilia na kijamii katika nchi za Magharibi. Vilevile msimamo wa kupinga tofauti za kimaumbile kati ya wanaume na wanawake na kuamini usawa kamili baina ya wawili hao katika nyanja za kijamii, uliufanya mlengo wa mafeministi wa kiliberali ukabiliwe na mikinzano mikubwa. Ni vyema kukumbusha hapa kuwa usawa katika fursa na matunda yake una maana ya kuwa sawa nyanja zote za ushindani baina ya wanaume na wanawake; wakati huo vipi wanawake ambao wana mchango makhsusi katika uzazi wa wanadamu (Reproduction) na ni mwenye nguvu dhaifu zaidi za kimwili wakilinganishwa na mwanaume hususan katika kipindi cha ujauzito, wataweza vipi kushindana sawa na mwanaume? Kama atamualika mgeni nyumbani kwake na kumlisha, atakuwa anamuibia mumewe…” (san. 71a, & Git.Ra).

Yapo mambo kadha wa kadha yanayojitokeza na ambayo kwayo huwa ni changamoto kwa mwanamke kuendeleza mapambano yake dhidi ya minyororo kaandamizi. Utafiti huu uligundua kuwa changamoto ambazo zinawakabili wanawake ni pamoja na; uvivu, usariti, wivu, kutokupendana, ukosefu wa elimu, umaskini, kubaguliwa, kutoaminiwa ndani ya jamii.

Usaliti

Kwa mujibu wa TUKI (2004) usaliti ni kutoa siri za nchi kwa adui wa nchi hiyo kwa lengo la kuihujumu; toa mipango ya siri ya wenzako kwa watu wengine ili wenzako wakamatwe, fitini. Utafiti huu uligundua kuwa suala la usaliti ni kikwazo kikubwa katika uongozi kwa wanawake. Usaliti unaonekana kwa wanawake wenyewe kwa wenyewe ambao wanaonekana wanasalitiana. Usaliti unafanya suala zima la uongozi kuwa gumu na hata ugumu katika kujikomboa kuondokana na ukandamizwaji unaofanywa na wanaume. Lakini pia wanawake wanaonekana kuwasaliti waume zao na kuwaingiza katika hatari (tazama Samson alivyosalitiwa na Mkewe Delila).

Uvivu Uliokithiri

Neno uvivu lina maana ya hali ya kutotaka kufanya kazi au hali ya ulegevu katika kufanya kazi (TUKI, 2004). Katika kazi hii iligundulika kuwa, viongozi wa Patata (wanwake) hawapendi kufanya kazi ya kuletea maendeleo ya Taifa lao. Wanapanga mambo yasiyotekelezeka na kushindwa kuyafanyia kazi kwa wakati kulingana na malengo yao

Ukosefu wa Elimu Miongoni mwa Wanawake

Kwa mujibu wa TUKI (2004) neno elimu lina maana ya mfumo wa mafunzo yanayopatikana shuleni, vyuoni, maishani. Katika utafiti huu tuligundua kuwa, tatizo la elimu ni tatizo kubwa ambalo linawakabili. Wanawake ni kundi ambalo limeachwa nyuma katika masuala ya elimu hivyo basi, kukosekana kwa elimu kunawafanya wanawake washindwe kushika nafasi za uongozi hasa uongozi wa juu. Mwandishi anaonesha jinsi ukosefu wa elimu unavyosababisha viongozi kutokuwa makini.  

 

Kupenda Starehe

Kwa mujibu wa kamusi ya TUKI (2004) neno starehe lina maana ya hali ya kutokuweko na shida au usumbufu, burudani; hali ya kuweko mambo ya anasa au furaha; burudani. Mwanamke anaonekana kupenda kufanya starehe kuliko kufanya kazi. Bi tatu anaona Nguzo Mama haina faida kwake.Mume na starehe ndiyo vitu anavyovipenda.Hivyo anawasusia wenzake kwa kutimkia kwenye Volvo lililomfuata na kuelekea kwenye sherehe.
                      ……Jamani mie naondoka mnaiona Volvo imenifuata mie….tunakwenda. Kwenye pati na mume wangu leo saa moja. Lazima nipalilie unga kwa baba watoto wangu ati. Nitakula nini… (Uk.41)
Mfano huo unaonyesha jinsi ambavyo wanawake wanavyopenda starehe na kwa kuwa tegemezi wa wanaume ambao huonekana ndiyo wenye haki ya kuwapa starehe wanawake.  Hii yote ni mifumo dume, ambayo wanawake wanaona hawawezi kufanya kitu pasipo kumtegemea mwanaume.

Umasikini wa Wanawake

Maskini ni mtu asiyekuwa na pato la kutosha; fukara, dhalili. Katika utafiti huu iligundulika kuwa suala la umaskini ni changamoto kubwa katika uongozi kwa wanawake. Umaskini humfanya mtu kukosa elimu, kuhangaika ili ajikwamue na umaskini kuna mfanya apoteze muda mwingi katika hilo na kusahahu majukumu yake kama kiongozi. Katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwandishi amelionyesha hili kwa kusema wanawake wa Patata wanalia tabu, Bi tano shida zinamwandama. Watoto wake wanapata taabu. 

Malezi na Mafundisho Mbalimbali hasa ya ki-mila na ki-dini

Malezi lina maana ya njia za ukuzaji wa mtoto kwa kutarajia kufuata tabia na mwenendo unaostahili. Utafiti huu ulibaini kuwa, Mwanamke amejengwa na kuaminishwa na mfumo wa jamii kuwa kazi yake kubwa ni kulea familia na kukaa nyumbani.

Njia za Kutatua Changamoto Zinazowakabili Wanawake 

Njia zianzofaa katika kutatua changamoto ambazo zimebainishwa kutatiza mchakato wa wanawake kujikomboa zinapendekewa ili zifanyiwe kazi kupitia katika taasisi mbalimbali za kijamii kama vile dini, kiuchumi, kisiasa na kijamii huku mila na desturi zikitazamwa kwa ukaribu zaidi.   
Elimu, Usawa wa kijinsia na Ujasiliamali
Mabadiliko yanatakiwa kwa mwanamke kwa kufundishwa elimu ya kijinsia ili waweze kutambua haki zao. Shafi (1999) anaitaka jamii kukubaliana na mabadiliko yanayofanywa na wanawake. Wanatakiwa wajione wao wote wako sawa ili kuondoa kasumba ya kuamini kuwa, wanaume wako juu, zaidi ya wanawake.  Wanawake na wanaume wanatakiwa kuelemishwa kuhusu haki za binadamu. Watu wote ni sawa ili kuondoa vikwazo na vipingamizi wanavyopata wanawake katika harakati zao. Wanawake wapewe elimu ya ujasiliamali ili waweze kujitegemea wenyewe pasipo kumtegemea mwanaume. Mila kandamizi ziangaliwe na jamii ichukue nafasi yake katika kuendana na mila stahiki kutokana na maendeleo ya teknolojia. Taasisi za kidini ziboreshe Mfumo wa utoaji huduma na haki sawa kwa watu wote hasa kwa wanawake.
Hitimisho 
Kwa kuwa dini ni sehemu ya jamii na wanajamii ndio waumini wa dini hizo, basi mikakati madhubuti iwepo ili kuwafanya wanawake wajiskie huru katika suala zima la kuitumikia jamii. Uhalisia wa maisha ya mwafrika umeonekana kupitia katika kazi mbalimbali za kifasihi zikieleza uhalisia wa maisha yao. Kazi mbalimbali za fasihi hazikuwa mbali na Vitabu vitakatifu katika kumsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye dhambi, dhaifu, maskini na mwenye kumtegemea mwanamme katika kutatua matatizo yake.
Hata hivyo, tumeona juhudi mbalimbali za wanawake katika Biblia wakiwa tayari wameshika nyadhifa mbalimbali na wakilitumikia kanisa kwa nguvu. Pia katika jamii ya kiafrika wanawake wameonekana wakiwa msitari wa mbele katika kutoa haki, kuonesha upendo, kuongoza vizuri na kutunza familia. Wito wangu ni kwa wanaume kuwaunga mkono wanawake katika mapambano yao ili hatimaye sote kwa pamoja tushilikiane katika kuleta maendeleo kwa kuwa “umoja ni nguvu…”

MAREJELEO:

Ba, M. (1994). Barua Ndefu Kama Hii. Tafsiri.Mkuki na Nyota Publishers
Beltsville, M. D. (1990). Elsayyed Sabiq, Figh al Sunnah; Darul Fatah Lile`lam Al-Arabi, 11th edition, vol. 2, Abdel-Haleem Abu Shuqqa, Tahreer al Mar`aa fi Asr al Rasala Kuwait: Dar al Qalam.
Gabriel, G. (2015). Ufeministi, itikadi na misingi yake. Mwanza: Serengeti Publishers
Irib, World Service (2014). Matatizo ya Wanawake katika Ulimwengu wa Magharib. http://www.kiswahili.irib.ir/38823    .
James A. B., (1987). Law, Sex and Christian Society in Medieval Europe. Chicago: University of Chicago Press. 
Jeffrey H. T. (1990). Adultery,” Encyclopaedia Judaica, Vol. 2, col. 313 and Standing Again at Sinai: Judaism from a Feminist Perspective. New York: Harper & Row Publishers. 
Jeffrey, L. (1994). Struggling to Surrender, Cairo: Amana Publications
Malenya, M. M. (2012), Matumizi ya  Lugha katika Fasihi Simulizi. Mwanza: Inland Press.
Mbunda, M. (1990). Usiku Utakapokwisha. Dar es Salaam University Press, University of Dar es Salaam.
Metuchen, N. J. (1976). Memories of an Orthodox youth” in Susannah Haschel ed. On being a Jewish Feminist.New York: hocken Books.-
Mohamed.S.A. (1990). Kivuli Kinaishi. Nairobi. Oxford University Press.
Mtembei A.K., (2012). Korasi katika Fasihi: Nadharia Mpya ya Uhakiki. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
Muhando. P. (1982). Nguzo Mama, Dar es Salaam University Press, University of Dar es salaam, Tanzania
Njogu, K & Wafula, R. M. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation Collage
Njogu, K. & Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta
Philip L. Kilbride (1994). Plural Marriage for Our Times Westport Conn.: Bergin & Garvey.
Ntarangwi, M. (2004): Uhakiki wa kazi za fasihi. Rock Islands.Augustine college.

Routlendge, (1974). Women in Stuart England and America; The Law of the Father. London:  Gage, op. cit.
Shafi, A.S. (1999). Vuta ni Kuvute. Mkuki na Nyota Publishers, DSM. Tanzania.
Swidler L. M. E. (1973). The Jewish Marriage Contract. New York: Arno Press op. cit.
The Toronto Star (1995). Muhammad al Ghazali, Qadaya al Mar`aa bin al Taqaleed al Rakida wal Wafida. Cairo: Dar al Shrooq, 4th edition Sabiq, op. cit.
David W. A., (1896). The Jewish Law of Divorce According to Bible and Talmud Philadelphia: Edward Stern & Con., Inc Publishing Ltd. .,
TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi.Oxford University Press
Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia.Nairobi.Focus
Wamitila, K. M. (2002). Uhakiki wa Fasihi, Misingi na Vipengele vyake. Nairobi: Phoenix.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny