Kwa
kuanza na maana ya fasihi Mulokozi (2017; 6) Anasema kuwa fasihi ni Sanaa ya
lugha yenye ubunifu inayojaribu kusawili vipengele vya maisha, mahusiano,
mazingira na hisia za watu katika muktadha fulani anaendelea kusema kuwa fasihi
imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni fasihi simulizi na fasihi
andishi. Hivyo kwa swali letu tutajikita Zaidi katika kueleza na kufafanua
dhana ya fasihi simulizi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali kwa kuanza na
wataalamu wa Tanzania.
Matteru
(2003), anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia midomo katika
kuumbwa, kuwasilishwa, na kusambazwa kwa wasikilizaji na watuamiaji wake,
anaendelea kusema kuwa ni Sanaa itumiayo maneno katika kutoa dhana Fulani
hutegemea sana nyenzo mbalimbali za kuonekana na kusikika zitumiwazo na
binadamu katika kujieleza mathalani fasihi simulizi hutegemea utendaji ili
kukamilika. Fasili hii ya Matteru ina ubora kwani imetupatia mwanga wa namna ya
uwasilishwaji na utendaji wa fasihi simulizi kwa upande wa uwasilishaji wa
fasihi simulizi fasihi hii imetupa mwanga kuwa fasihi simulizi huwasilishwa kwa
njia ya mdomo na kwa upande wa utendaji ameonesha kuwa fasihi simulizi hutumia
vitabia, miondoko na visogeo katika utendaji wake. Licha ya fasili hii kuwa na
ubora pia ina udhaifu kwani mtaalamu huyu hajabaini uwepo wa umuhimu wa kichwa
katika kuumbwa kwa fasihi simulizi kwani kichwa ndicho hutumika kuumba na
kutunza fasihi simulizi kabla na baada ya uwasilishwaji.
Balisidya
M.L (1982;1). Ameeleza kuwa fasihi simulizi “Is the type of literature that
is very much dependent on verbal performance distribution and circulation. Even
though it can be preserved through script and in fact the scripts can be used
to aid its composition oral literature remains oral likely any verbal
communication oral literature employs the use of the ear and eyes”. Kwa
maana kuwa
“Ni
ile aina ya fasihi ambayo hutegemea sana usanii wenye sauti katika mtawanyiko
na usambazwaji wake hata kama inaweza kusambazwa kwa maandishi. Kwa kweli
maandishi yanaweza kusaidia kuongeza utunzi. Fasihi simulizi hubaki kuwa ya mdomo.
Kama mawasiliano yoyote ya maneno, fasihi simulizi hutumia sikio na jicho”
Fasili
hii ni bora kwani fasihi simulizi hutegemea sana usanii wenye sauti (yaani
matumizi ya mdomo) Katika usambazaji wake japo hajagusia uhifadhi wake kabla na
baada ya uwasilishaji.
Mulokozi
(1996;24). Fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa
kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila kutumia maandishi. Anaendelea
kusema fasihi simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha (mazingira) Fulani
wa kijamii na kutawaliwa na mwingiliano wa mambo sita: fanani, hadhira, fani
inayotendwa, tukio, mahali, na wakati. Fasili hii imefanikiwa kueleza namna
fasihi simulizi inavyotungwa au kubuniwa kichwani inavyowasilishwa kwa njia yam
domo na vitendo bila kutumia maandishi japo amepuuza maandishi kama njia moja
wapo ya utunzaji wa kazi za fasihi simulizi ikishirikiana na njia zingine za
utumiaji wa kazi za fasihi simulizi kama vile kanda za video na vinasa sauti.
Mbunda
(1993:3) anasema kuwa fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha. Kazi
hiyo huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
Anaendelea kusema kuwa fasihi simulizi imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi hadi
kizazi. Fasili hii ina ubora wake kwa sababu ni kweli fasihi simulizi
hurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi na pia uwasilishwaji wake ni wa
masimulizi ya mdomo. Lakini kwa upande mwingine ina mapungufu kwa sababu
inaonesha njia moja tu ya uhifadhi wa fasihi simulizi kwa maana kwamba fasihi
simulizi huhifadhiwa kichwani tu, fasili hii haijazungumzia uhifadhi wa njia
zingine ambazo ni vinasa sauti, kanda za kurekodi, na maandishi.
Baada
ya kuona fasili mbalimbali za fasihi simulizi kutoka kwa wataalamu wa
kitanzania sasa tuangazie wataalamu wa fasihi simulizi kutoka Kenya
wanavyofasili fasihi simulizi huku tukitazama ubora na udhaifu wa fasili zao
kama ifuatavyo:-
Wamitila
(2003;43). Anafasiri dhana hii ya fasihi simulizi kuwa ni dhana inayotumika
kurejelea kazi ambazo kimsingi hupokezana kwa njia ya masimulizi au kwa mdomo.
Sanaa hii ambayo huweza kuhifadhiwa kwa njia kuu mbili yaani njia ya mdomo na
maandishi. Anaendelea kusema “fasihi simulizi siyo simulizi tena bali
inahifadhiwa kwa njia mbalimbali kama vile kinasa sauti, kanda za video na
kompyuta. Mtaalamu huyu ameweka msisitizo juu ya uwasilishwaji wa fasihi
simulizi kwa njia ya mdomo pia ameonyesha njia mbalimbali za utunzaji na
uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi ambazo amezitaja kuwa ni kinasa sauti,
kanda za video na kompyuta.
Njogu
(2013:2). Anaeleza kuwa fasihi simulizi ina ubunifu na uhai wa kipekee wenye
kutoa fursa njema ya kuibua nadharia za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Pia
anaifananisha aina hii ya fasihi na uti wa mgongo wa maendeleo ya binadamu
kwani ndani yake kuna simulizi, maigizo, tathimini za mazingira na mahusiano.
Ubora wa fasili hii ni kuwa imetuonesha kuwa fasihi simulizi ni hai na ina
ubunifu wa kipekee wenye kuibua nadharia mbalimbali. Udhaifu wa dhana hii
haijaweza kufafanua ni kwa vipi fasihi simulizi huumbwa, huhifadhiwa na
kusambazwa.
M’ngaruthi
(2008;3). Anasema fasihi simulizi inaweza kuelezwa kama aina ya Sanaa
inayowasilishwa kwa ubunifu kupitia lugha ambayo haijandikwa , anaendelea
kusema kuwa hata hivyo kufikia sasa fasihi hii imepata kuhifadhiwa kwa njia
mbalimbali ili isipotee. Baadhi ya njia hizi za uhifadhi ni kama vile kupitia
maandishi, kanda za kunasa sauti na picha au hata tarakilishi. Ubora wa fasili
ni kuwa amezungumzia nyenzo muhimu ya fasihi simulizi ambayo ni lugha hususani
lugha ya mazungumzo, yaani isiyo katika maandishi pia ameonesha uhifadhi wake
ambao ni maandishi, kanda za kunasa sauti na picha au hata tarakilishi, lakini
ameonesha udhaifu kwani hajaeleza namna inavyobuniwa.
Uwasilishaji,
katika kuangalia kigezo cha uwasilishwaji wa kazi za fasihi simulizi wataalamu
walio wengi wametofautiana kwa namna moja ama nyingine kwa mfano:- Matteru (1983)
anasema kuwa fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo kuumbwa,
kuwasilishwa, na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mtaalamu huyu
ameonesha wazi kuwa fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo na
wanaomuunga mkono mtaalamu huyu ni Balisidya (1982),
Mulokozi (1996), Mbunda ( 1992),
Wamitila (2003) wakati Njogu (2013) yeye hajaonesha wazi suala la matumizi ya
,mdomo katika uwasilishwaji wa kazi za fasihi simulizi anaposema
“Aina
hii ya fasihi ni uti wa mgongo kwa maendeleo ya binadamu kwani ndani yake kuna
usimulizi, maigizo, tathimini za mazingira na mahusiano”.
Baada ya kuangalia fasili za wataalamu kwa kubaini ubora na udhaifu sasa tuone
mfano na utofauti baina ya fasiri hii kwa kuzingatian baadhi ya sifa bainifu za
fasihi simulizi ambazo ni uwasilishaji, uhifadhi, utendaji na hadhira kama
ifuatavyo:-
Uhifadhi,
suala la uhifadhi wa fasihi simulizi limezungumziwa na wataalamu kwa namna
tofauti huku wengine wakishindwa kuonesha waziwazi ni kwa namna gani fasihi
simulizi huhifadhiwa kwa mfano:- M’ngaruthi (2008:24) anaeleza kuwa fasihi
simulizi inaweza kuhifadhiwa kwa maandishi, vinasa sauti, picha au hata
tarakirishi. Wakati Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni ile ambayo
hutegemea sana usanii wenye sauti katika mtawanyiko na usambazaji wake hata
kama inaweza kusambazwa kwa maandishi kwa kweli maandishi yanaweza kusaidia
kuongeza utunzi. Fasihi simulizi hubaki kuwa ya mdomo kama mawasiliano yoyote
ya maneno, fasihi simulizi hutumia sikio na jicho. Mtaalamu huyu ameonesha njia
moja tu ya uhifadhi wa maandishi. Wataalamu wengine kama vile Matteru,
mulokozi, Wamitila, na Njogu hawajaligusia suala la uhifadhi katika uhifadhi
wao. Kwa mfano:- Mulokozi (1996:34) anasema fasihi simulizi ni fasihi
inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo
na vitendo bila kutumia maandishi.
Utendaji,
kwa upande wa utendaji wataalamu hawa wametofautiana kukielezea kipengere hiki
katika fasili zao kuna waliokiona kipengere hiki kuwa ni cha muhimu na kuna
waliokipuuza kwa namna fulani kwa mfano:- Matteru (1983) na Mulokozi (1996)
waliona ni kipengere cha muhimu sana katika fasihi simulizi Mulokozi
(amekwishatajwa) yeye anasema kuwa ni fasihi iliyotungwa au kubuniwa kichwani
na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila kutumia
maandishi. Kutokana na fasili hii tunaona kuwa suala la utendaji limechukuliwa
kuwa ni la muhimu sana. Wakati kwa wataalamu kama Balisidya, Mbunda na Wamitila
hawakuona umuhimu wa matendo (utendaji) katika kufasili dhana hii.
Hadhira,
suala la hadhira pia limezungumziwa na baadhi ya wataalamu huku wengine
hawakuliongelea kwa Mfano:- Mulokozi (ameshatajwa) anazungumzia hadhira katika
fasihi simulizi kuwa ni jambo la muhimu sana na anasema kuwa
“fasihi
simulizi ni tukio linalofungamana na muktadha (mazingira) Fulani wa kijamii na
kuitawaliwa na muingiliano wa mambo sita yaani fanani, hadhira, fani
inayotendwa, tukio, mahali, na wakati. Hapa anasisitiza kuwa hadhira ni muhimu
sana katika fasihi simulizi kwani wao ndio washiriki na wahakiki wa Sanaa hiyo
inayowasilishwa na fanani. Suala hili la hadhira linaungwa mkono na Wamitila
(amekwishatajwa) yeye anasema “ hadhira ya fasihi simulizi inaweza kuwa tendi
ambayo inashiriki na kuchangia katika uwasilishwaji wa kazi inayohusika” hapa
Wamitila anaonesha ushirikiano baina ya fanani na hadhira katika fasihi
similizi. Wakati wataalamu wengine hawakuzungumzia suala la hadhira.
Baada
ya kulinganisha na kulinganua fasili hizi za wataalamu tumebaini kuwa fasili ya
Mulokozi (1996) kama anvyosema fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au
kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila
kutumia maandishi. Fasihi hii kwa kiasi ni bora kuliko zingine kwani imegusia
sifa za msingi za kazi ya fasihi simulizi ambazo ni kutungwa au kubuniwa
kichwani, kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo.
Hivyo
basi fasihi simulizi inapaswa kuwa na sifa bainifu ambazo zitaifanya kuwa
tofauti na fasihi andishi sifa hizi zimekuwa zikibadilika kulingana na
maendeleo ya sayansi na tekinolojia sifa hizi ni uwasilishwaji, kuwa fasihi
simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au masimulizi japo maendeleo ya sayansi
na tekinolojia yameleta maendeleo katika hili kwani fasihi simulizi imekuwa
ikiwasilishwa kwa vyombo kama vile redio, televisheni pamoja na tarakirishi.
Pia sifa nyingine ni utendaji wa papo kwa papo japo kwa sasa utendaji sio
lazima kuwa wa papo kwa papo kwani kazi ya fasihi yaweza kurekodiwa na kutunzwa
ili iwasiliswe pasi na kuwepo na fanani hai. Sifa nyingine ni uhusishwaji wa
fanani na hadhira fasihi simulizi huhusisha fanani na hadhira japo kwa sasa
fanani na hadhira si lazima wawe ana kwa ana, Pia humilikiwa na jamii nzima
ambapo huwa ni tukio ambalo hufungamana na muktadha au mazingira
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com