Dhana ya tungo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali,
Massamba,Kihore na Hokororo (2012;67) wanasema tungo ni nomino ambayo
hutokana na kitenzi tunga ambacho kina maana ya kushikanisha vitu kwa pamoja kwa
kuptsha kitu kama uzi,ungwe, ndani yake,hivyo kataka taaluma ya sarufi neno
tungo lina maana ni ambayo ni kuweka au
kupanga pamoja vipashio sahihi li kujenga kipashio kikubwa katika tungo.
Kamusi teule ya Kiswahili
(201;1015) tungo kifungu cha maneno
kinachoongozwa na kanuni kisarufi kataika lugha inayo husika ambapo vipashio
vipashio vinapoungana huunda kipashio kikubwa zaidi.
Kamusi teule ya
Kiswahili(2014;632) tungo ni kipashio
cha kimuundo kipatikanacho kwa kuunganisha vipashio sahihi kuweza kupata
kipashio kikubwa zaidi katika sarufi Kwa ujumla tungo ni kipashio cha kimuundo
ambacho huweka pamoja il kujenga vipashio vikubwa zaidi katika sarufi.
Tungo
hujidhihilisha katika miundo minne ambayo ni tungo neno,tungo kirai,tungo
kishazi,tungo na tungo sentensi.
Kwa kuanza na
tungo neno wataalamu mbalimbali wameweza kufasili maana ya tungo neno kama
ifuatavyo,
Kamusi ya
Kiswahili sanifu (2004) neno ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazoandikwa au
zinazotamkwa na kuleta maana.
Kamusi kuu ya
kiswahili (2015;787) tamko moja wapo miongoni mwa mengi ambalo mtu hutamka
katika mchakato wa mazungumzo.
Massamba,Kihore
na Hokororo (2012;69) wanasema tungo ni
mahusiano ya viamba jengo vyake yamekitwa katika kiwango cha neno.
Kwa ujumla
tunapochunguza tungo neno katika kiwango chochote kile tunajikita katika
kuangalia jinsi tungo hizo zinavyoundwa pamoja na vipashio vyake vinavyohusika.
Maelezo
yaliyotolewa na Massamba na wenzake ni
kwamba ili kupata tungo neno katika lugha ya Kiswahili taratibu mbili muhimu
lazima zifuatwe.Utaratibu wa kwanza ni mpangilio wa vitamkwa ili kupata
silabi,mpangilio wa pili ni mpangilio wa mofimu.
Mpangilio wa
vitamkwa katika kujenga silabi,huhusu vitamkwa kupangwa katika mfuatano
unaotupatia silabi zinazokubalika katika lugha yoyote iwayo,pia silabi ni
kipashio cha utamkaji ambacho huruhusu sauti za lugha kutamkwa kama fungu moja
hivyo tunaposema kwamba lugha zote zinampangilio wa vitamkwa zinazokubaliwa
katika kujenga silabi na lugha zote hutumia utaratibu wake katika vitamkwa.
Katika lugha ya
Kiswahili taratibu zitumikazo ni kama zifuatazo,
(i)irabu peke yake
mfano,au,
(ii)konsonanti
na irabu
mfano wa,na,za
(iii)kiyeyusho
na irabu
mfano wa,ya
(iv)konsonanti,kiyeyusho
na irabu
mfano kwa
(v)konsonanti,konsonanti,irabu
mfano (a)mbaya
(b)nyenzo
(vi)konsonanti,konsonanti,kiyeyusho,irabu
mfano (a)kushindwa
(b)kinazungumzwa
Mpangilio wa
mofimu katika kujenga tungo neno unahusu
hasa mpangilio wa viambishi na mzizi katika neno,katika lugha ya kiswahili
tungo neno huweza kujegwa na mzizi
huru(usiohitaji viambishi katika kukamilisha maana yake) au hujengwa na
viambishi na mizizi,
mfano(i)
mzizi huru sayansi ,bunge
(ii)mzizi tegemezi watoto,wanaume
Pia
mizizi na viambishi huandamana katika kuunda tungo neno kwa kufuata taratibu
maalumu taratibu hizo ni kama zifuatazo
(i)Mizizi kufuatwa na kiambshi
au viambishi
mfano (a)somo,mzizi ni{som}
(b) soma,mzizi ni
{som}
(ii)Mizizi kutanguliwa na
viambishi
mfano (a)M-toto
(c)M-zazi
(iii)Mizizi kutanguliwa
kufuatiwa na viambishi
mfano (a)wa-toto
(b)ana-lind-a
(c)anapo-kul-a
Katika lugha ya Kiswahili kuhusu aina za
maneno wataalamu wa mitala mbalimbali ya Kiswahili wamekua wakitofautiana,ingawa
pengine tofauti hizo si kubwa sana.Baadhi wamehitilafiana katika istilahi
wanazotumia,na wengine wamehitilafiana katika idadi ya aina yenyewe.Kwa mfano
Nkwera ana aina saba za maneno Nomino,Vivumishi,Viwakilishi,Vitenzi,Vielezi,Viunganishi
na vihisishi. Kapinga ana aina saba za maneno
Majina,Vivumishi,Viwakilishi,Vitenzi,Vielezi,Vihusishi,Viigizi na Kihore ana
aina nane Majina,Vitenzi,Vivumishi,Vielezi,Viunganishi,Kiwakilishi,Viingizi na
Viigizi. Kwamba Nkwera na Kapinga wanatambua aina saba za maneno,ambapo Kihore
ana aina nane za maneno.Aidha wakati Kihore na Kapinga wanatumiia istilahi ya
majina wakati Nkwera anatumia nomino,Hivyo kutokana na wataalamu hao ninamtumia
mtaalamu Nkwera kuonyesha aina za maneno na mifano kutoka katika makala
elekezi,
(i)Nomino
mfano
Raisi,Nchi,Msumbiji,Chisano,Ghana
(ii)Kivumishi
mfano(a)
ushujaa,ustawi,
(b)Watoto wake
(c)Wanafunzi wote
(iii)Kiunganishi
mfano kwa,na, kama.
(iv)Vitenzi
mfano
kufundishia,fundisha.
(v)Kielezi
mfano vizuri mno,kesho na baadae
Mbali na tungo
neno lugha ya Kiswahili pia hujengwa na tungo kirai,aina hii ya tungo imeweza
kujadiliwa na wataalamu mbalimbali
Massamba,Kihore
na Hokororo (2012;74) wanasema aina hii ya tungo hujidhihrisha katika kiwango
cha kirai.Katika kiwango hiki miundo ya tungo huhusisha maneno mawili au zaidi
ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalumu unazingatia uhusiano uliopo
baina ya neno kuu na maneno mengine.
Kamusi teule ya
Kiswahili (2014;311) tungo kirai hutumika katika sarufi kuelezea kipashio cha
kimuundo ambacho huweza kuwa neno moja au zaidi linalotokea
nomino,kielezi,kiarifa
Kamusi kuu ya
Kiswahili (2015;463) tungo kirai ni kipashio cha kimuundo kinachoundwa kwa neno
moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.
Kwa ujumla tungo
kirai ni kipashio cha kimuundo ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu lakini
hutoa taarifa fulani.
Katika tungo
kirai tunaona Massamba na wenzake anasema tungo virai zina maumbo na miundo
mbalimbali kulingana na virai vilivyomo
katika lugha inayohusika,Katika lugha ya Kiswahili kuna aina mbalimbali za
virai lakini vifuatavyo ni aina ya virai
kutoka kaka makala elekezi
Kirai nomimo,ni aina ya kirai ambalo neno kuu ni nomino
mfano
(i) Afrika
(ii)Wasomi wabobezi
(iii),Kiswahili
kinafunzwa.
Kirai kielezi ni aina ya kirai
ambalo neno kuu ni kielezi
mfano
(i)Sasa tutizame kesho na baadae
(ii)Anafundisha mara
chache
(iii)Lugha
moja hufa kila baada ya siku kumi na nne
(iv)Kuogezeka kwa kasi
Kirai kivumishi ni aina ya kirai ambalo neno kuu ni kivumishi
mfano (i)Wanafunzi wote
(ii)Mjadala mkali kuhusu
kutumia kiingereza au kufundishia ukupamba
moto kati ya 1965 mpaka mwanzo wa 1980
Kirai kitenzi ni aina ya kirai ambayo
neno kuu ni kitenzi
mfano
(i) Anafundisha
(ii)pendekezo
(ii)kufundisha
Tungo kishazi ni aina ya tungo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali
Kamusi Teule ya
Kiswahili (2014;314) tungo kishazi hutumika katika sarufi kuelezea kundi la
maneno yanayojumusha kundi la nomino na kundi kitenzi,kiima na kiarifu,kishazi
huru na tegemezi,kishazi sharti,beba,chopekwa,ambatani na ongezi.
Kamusi ya
Kiswahili Sanifu (2004;124) tungo kishazi ni kifungu cha maneno yasiyo
kamilisha maana.
Kamusi Kuu ya
Kiswahili (2015;469) kishazi ni tungo yenye kiima na kiariafu ambayo imo ndani
ya tungo kuu.
Massamba,Kihore
na Hokororo (2012;77) wanasema tungo kishazi ni matokeo ya kuweka pamoja miundo
miwili au zaidi yenye kirai nomino na kirai kitenzi ndani ya tungo
sentensi.Fasili hii na maana kwamba tungo kishazi ni kubwa kuliko tungo
kirai,lakini ni ndogo kuliko tungo sentensi.
Kwa jumla tungo
kishazi ni neno au kifungu cha maneno yanayotoa taarifa kamili au isiyo kamili.
Kwa kawaida
tungo kishazi hujidhihirisha katika muktadha wa sentensi ambamo huwa
zinabebwa.Utaratibu wa miundo hii ni kwamba tungo kishazi mbili au zaidi huwa
hubebwa na sentensi moja.Massamba na wenzake wanasema kuna aina tatu za tungo
kishazi,aina hizo ni kama zifuatazo
Tungo kishazi kirejeshi ambacho kwa kawaida hubebwa na kirai nomino
mfano
(i)Miundo mbinu iliyowekwa ilikuwa ya gharama kubwa
(ii)Mmeona hizo lugha zinazotumika (AU) na (SADC) ukilinganisha
na
hizo
za (EU) kuna nini kwetu.?
Tungo kishazi kielezi ambacho kwa kawaida hubebwa na kirai kielezi
mfano
(i)Hawa wakawa wanasisitiza umuhimu wa watoto kujifunza katika lugha
yao
ya asili ambayo wanaielewa vizuri
Tungo kishazi ambatani ambazo kwa kawaida huunganishwa ni viunganishi
mfano(i).
Kuhusu Kiswahili,matumizi yake yamekuwa yakipanuka tena kwa kasi
kubwa
ikiwa ni pamoja na msamiati na istilahi zake kuongezeka,Nyanja
za matumiz yake kupanuka,idadi ya
wazungumzaji wake kuongezeka…
(ii)Swali lingine muhimu
Je katika dunia inayobadilishwa kasi na sayansi
na teknolojia
Kiswahili kitakuwepo 2050 au kitakuwa kimevia na
Tungo sentensi
ni aina ya tungo ambayo imeweza kufasiliwa na wataalamu mbalimbali kama
ifuatavyo,
Kamusi teule ya
Kiswahili (2014;559) tungo sentensi ni neno au fungu la maneno linalojitokeza ama lenye maana kamilifu
na ambalo huwa na mtenda,kitendo na mtendwa.
Kamusi kuu ya
Kiswahili (2015;918) tungo sentensi ni tungo yenye neno moja au zaidi ambayo
hutoa taarifa kamili,swali au amri na ambayo ina muundo wan a karifu ndan yake.
Kamusi ya
Kiswahili Sanifu (2014;251) tungo sentensi ni fungu la maneno au neno
linalowakilisha nafsi,kitenzi wakati na kinachotendwa na linapasha habari
kamili.
Massamba,Kihore na Hokororo
(2012;197) wanasema tungo sentensi ni tungo ambayo mahusiano ya viambajengo
vyake yamejikita katika kiwango cha sentensi,Wanaendelea kwa kusema tungo
sentensi ni za aina nyingi kutegemea
aina ya sentensi zinazohusika.
.
Kwa ujumla tungo
sentensi ni kipashio kimuundo ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu na
hutoa taarifa kamili.
Massamba,Kihore
na Hokororo wanasema kuna aina tatu za tungo sentensi nazo ni
Sentensi sahili
ni muundo wa tungo sentensi naohusisha kirai
kirai nomio,kirai kitenzi, na yenye maana kamili iliyokusudiwa,kiini cha
sentensi sahihi ni kirai kitenzi ambacho kwa kawaida huweza kutokea peke yake
au kuandamana na vipashio vingine vya sentensi kama kirai nomino,kirai
kivumishi,kirai kielezi.
mfano
(i) Shirika la kazi duniani.
(ii)Mawasiliano ya lugha huwa nyenzo kuu katika kufanikisha shughuli za
binadamu,kiuchumi,kisiasa,kijamii,kiutamaduni,kifasihi,kiteknolojia
na
kisayansi,kielimu nk
Sentensi
ambatani ni sentensi ambazo huwa ni
sentensi mbili au zaidi zilizo huru ambazo uunganishwa pamoja kwa viunganishi.
mfano Miundombinu iliyowekwa
ilikuwa ya gharama kubwa lakini serikali ya
wakati huo
ilidhamilia,ikapanga na kutekeleza ili kusimika Kiswahili
lugha ya taifa.
Sentensi
changamani ni tungo sentensi ambayo inaundwa na kishazi tegemezi na kishazi
huru
mfano (i)Lugha isiyotumika au
kutumiwa hatima yake hutoweka/hufa
(ii)Mioyo
ikainuliwa wakaielekeza majuu….na bondeni…
(iii)Wakati
mjadala huu unaendelea fungo anayeitwa UTANDAWAZI akaingia
uvunguni.
Hivyo,Tungo
za Kiswahili zimeweza kufafanuliwa na wataalamu mbalimbali ambao kila mtaalamu
kwa mawazo yao wameweza kutoa michango yao mbalimbali kuhusu tungo za
Kiswahili.Katika lugha ya Kiswahili tungo ndogo ni tungo neno na tungo kubwa ni
tungo sentensi.Tukingalia katika makala elekezi iliyowasilishwa na prof, A. D.
Kiwara ameweza kutumia aina za tungo japokuwa amejikita katika lugha ya
mazungumzo lakini ameweza kutumia tungo za Kiswahili kuanzia kiwango kidogo cha
tungo yaani tungo neno mpaka kiwango kikubwa tungo sentensi
MAREJELEO
Kiwira A.D (2017) Ukuaji wa Kiswahili na ustawi wa jamii ya
wazungumzaji wake.
(CHAUKIDU) Dar
es saalam.
Massamba na wenzake (2012) Sarufi ya Miundo ya Kiswahili Sanifu. ( SAMIKISA)
Sekondari na
vyuo.Dar es saalam.
Ndalu,A.E,Babusa,H n Mirikau,S.A (2014) Kamusi
Teule ya Kiswahili.Nairobi,Kampal
a ,Dar es salaam,Kigali.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com