Dhana
ya kategoria imejadiliwa kwa namna tofauti tofauti. Khamis na Kiango (2002)
wameigawa kategoria katika mitazamo miwili wanamapokeo na wanausasa. Ambapo
wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria kumaanisha sifa bainifu zinazoambikwa
kwenye aina za maneno kama vile nafsi, idadi, njeo, dhamira, na ngeli. Wakati
wanausasa wanaona kuwa kategoria ni zile aina za maneno kama vile Nomino (N),
vivumishi (V), vielezi (E), viunganishi (U), vitenzi (T), viwakilishi (W), na
Kihusishi (H).
Massamba
(2009) anaeleza kuwa kategoria ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine
ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja.
Samwel
(2) anaeleza kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo kuwa ni darajia mbalimbali
katika uundaji wa tungo. Anaendelea kueleza kuwa kuna kategoria za darajia
mbili ambazo ni kategoria ya neno (kileksika) na kategoria ya virai. Ambapo
kategoria ya kileksika huhusika na aina mbalimbali za maneno kama vile nomino,
vivumishi, viwakilishi, vielezi, vitenzi, viunganishi, vihusishi na vibainishi.
Naye O’Grady (1996) katika kufafanua kategoria za kileksika anaona kuwa ni
kategoria za kiwango cha neno mojamoja na anataja aina nne za maneno ambazo ni
nomino, kivumishi, kitenzi na kielezi. Darajia ya pili ni kategoria ya virai
Samwel (keshatajwa) anaeleza kuwa hii ni kategoria inayofuata katika ile ya
neno. Hivyo anaeleza kuwa kategoria ya virai imeundwa na kirai nomino (KN),
kirai kivumishi (KV), kirai kitenzi (KT), kirai kihusishi (KH) na kirai kielezi
(KE).
Kwa
ujumla kwa kurejelea mtazamo wa sarufi mamboleo kategoria ni jamii au makundi
yanayofanya kazi kwa kufanana na yenye sifa zinazofanana.Wesana-Chomi (2003)
anaeleza kuwa dhana ya kategoria za maneno ni muhimu sana katika sarufi kwani
maelezo ya sarufi ya lugha hayana budi kurejea kategoria za maneno kwa namna
moja au nyingine. Hivyo zifatazo ni hoja zinazofafanua faida ya kuwa na
kategoria.
Husaidia
katika utungaji wa sentensi, O’Grady (1996) anaeleza kuwa neno fulani liko
katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa, mfano nomino hutaja vitu,
vitenzi ni maneno yanayotaja vitendo, vivumishi ni maneno yanayotaja sifa za
nomino na vielezi ni maneno ambayo hueleza namna tendo linavyofanyika. Hivyo
kutokana na maelezo ya O’Grady (keshatajwa) ni wazi kuwa mwanagenzi anapotaka
kutunga sentensi ni lazima ajue kategoria za maneno kwani hawezi kutunga
sentensi pasipo kuhusisha kategoria za manneno.
Hivyo kategoria husaidia katika utungaji wa tungo mbalimbali katika
lugha husika. Kwa mfano;
Wanafunzi
wanasoma
N T
Mtoto
anacheza mpira
N T N
Baba
analima na mama anafua nguo
N T U
N T N
Hivyo
mifano ya juu inaonesha namna kategoria za maneno zilivyotumika katika kuunda
ama kutunga sentensi mbalimbali.
Husaidia
kujua miundo ya sentensi katika lugha, Obuchi na Mukhwana (2015) wanaeleza kuwa
kategoria za maneno hufahamisha kwamba muundo wa sentensi huelezwa kwa kutaja
kategoria za maneno yanayounda sentensi hiyo. Hivyo kategoria za maneno
husaidia kujua miundo mbalimbali ya sentensi kwani kuna sentensi zenye muundo
wa (N + T) yaani Nomino na kitenzi, kuna sentensi zenye muundo wa nomino +
kivumishi + kitenzi + kielezi (N + V+ T+E), sentensi zenye muundo wa nomino +
kitenzi + kielezi (N + T+E). kama inavyojidhihirisha katika mifano inayofuata;
Muundo
wa (N + T + E)
Mama ameenda
sokoni
N
T E
Muundo
wa (N + V + T +E)
Msichana
mzuri ameenda shuleni
N V
T E
Hivyo
mifano tajwa hapo juu dhahiri inaonesha namna kategoria mbalimbali za maneno
zilivyotumika katika kuonyesha miundo ya sentensi.
Kategoria husaidia kujua aina za maneno katika
lugha husika na dhima zake katika tungo, Wesana-Chomi (2003) anaeleza kuwa
maneno ya lugha hufanya kazi mbalimbali katika tungo. Mfano kuna maneno
yanayofanya kazi kuonesha nani katenda tendo, nani katendewa tendo au nani
katendwa tendo. Maneno yenye kazi hizo katika tungo huitwa nomino. Pia, maneno
mengine hutoa taarifa juu ya nomino na maneno hayo ni kivumishi. Aidha, maneno
mengine hutaja tendo au jambo lifanywalo na mtenda tendo na maneno hayo huitwa
vitenzi. Kwa mfano;
Mwalimu anafundisha
N
Mtoto mzuri
V
Hivyo
katika mifano hii neno Mwalimu ambalo ni nomino limesimama kama mtenda wa jambo
na katika mfano wa pili neno mzuri limesimama kama kivumishi ambacho kinatoa
sifa juu ya nomino. Hivyo kategoria husaidia kujua aina za maneno.
Husidia
kujua aina mbalimbali za virai pamoja na miundo yake, Massamba na wenzake
(2012) wanaeleza kuwa miundo ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo
ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivi. Mfano wa virai
hivyo ni KN, KV, KE, KT na KU. O’Grady (1996) anaeleza kuwa
Husaidia
na kutuwezesha kutunga sentensi zisizokikomo na zinazoeleweka. Sentensi
zisizokikomo ni sentensi ambazo ni ndefu na zisizo na mwisho, kwa mfano;
Baba
na mama walipanda mlima Kilimanjaro ambao mlima huo upo mpakani mwa Kenya na Tanzania
ambapo
Mama
alimnunulia mtoto zawadi iliyokuwa ikiuzwa sokoni kariakoo karibu na mtaa wa
mama lishe uliopakana na mtaa wa kongo pembezoni mwa maduka ya vitambaa vya kihindi vinavyouzwa na
wahindi kutoka India ambao walikuja Tanzania kufanya biashara zinazowaingizia
kipato kikubwa kiasi cha kuweza kumudu na kukidhi mahitaji ya familia yao.
Husaidia
katika uchanganuzi wa sentensi za lugha husika, katika kuchangua sentensi za
lugha kategoria za maneno hutumika kwani huwezi changanua sentensi pasipo
kuhusisha kategoria za maneno kwa mfano;
Baba
analima
N T
S.S
KN KT
N
T
Baba
analima
Husaidia
kuunda nadharia mbalimbali za sintakisia, kutokana na uchambuzi wakategoria za
kisintakisia kumepatikana nadharia mbalimbali kama vile sarufi miundo virai na
sarufi geuza maumbo zalishi.
Husaidia
kupata sarufi inayojitosheleza kwa usahihi katika lugha, lengo la uchambuzi wa
kisintakisia ni kutafta ukubalifu au usioukubalifu wa tungo zisizo sahihi.
MAREJELEO
Besha,
R.sM (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu.
Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Massamba,
D na Wenzake. (1999) Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu,Sekondari na vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Aina za Kategria za Kisintaksia na jinsi zinavyojidhihirisha katika lugha ya Kiswahili
ReplyDelete