Dhana ya kishazi imefasiliwa na wataalamu
mbalimbali kama ifuatavyo:
Lyons
(1968:170-171), akinukuliwa na Massamba na wenzake (2012:121) anaeleza kuwa
kishazi kama kundi la maneno lenye kiima na kiarifu, hasa likiwa ndani ya
sentensi kuu. Mtaalamu huyu anasisitiza kuwa kishazi lazima kiwe ndani ya
sentensi kuu.
Matei
(2008:208), anafasili kishazi kama kundi la maneno ambalo lina kiima kimoja na
kiarifu kimoja. Anaendelea kusema kuwa katika kila sentensi huwa kuna angalau kishazi
kimoja. Anasisitiza kuwa katika kila sentensi lazima kuwe na angalau kishazi
kimoja. Lakini pia Matei (kashatajwa), anabainisha sifa mbalimbali za kishazi
ambazo ni pamoja na;
(i).Kishazi lazima kiwe na kiima na
kiarifu.
Mfano I; mtoto aliyekuja jana /
ameondoka
K A
(II). Kishazi lazima kiwe na
kitenzi ndani yake
Mfano II; Juma /anatembea.
T
Chomi (2003:135), anasema kishazi ni
tungo iliyoundwa kwa kikundi nomino (KN) pamoja na kikundi kitenzi (KT). Kwa
mfano:
Mwalimu wetu/ anafundisha.
KN
KT
Kwa ujumla kishazi ni neno au mpangilio
wa maneno wenye kirai kitenzi kimoja ndani yake, ambapo kitenzi hicho kinaweza
kuwa ni kitenzi kikuu au kitenzi kilichoshushwa hadhi.Hivo chakusisitiza hapa
nikwamba kishazi hujidhihirisha katika maingira ya sentensi inamaana kwamba
bila kuwepo kwa sentensi kuu iliyokibeba hatuwezi kuwa na kishazi kwa sababu
kishazi chenyewe kitakua sentennsi.
Katika uainishaji wa vishazi kuna vigezo
vitumiwavyo ili kuainisha aina zake. Miongoni mwa vigezo hivyo na aina
inazotupatia kwa kila kigezo ni kama ifuatavyo;
Kwa kuzingatia kigezo cha kitenzi
kilichobebwa, hapa tunapata aina mbili za vishazi ambavyo ni vishazi ukomo na
vishazi viso ukomo. Kwa mujibu wa Radford(1988:287), anasema kuwa kuna vishazi
ukomo ni vile ambavyo vina vitenzi vyenye ukomo yaa ni vilivyoundwa na njeo na
upatanisho wa kisarufi. Vishazi visoukomo ni vishazi visivyobeba njeo wala
upatanisho wa kisarufi.
Kwa kuzingatia kigezo cha dhima kuna
vishazi vikumushi, vishazi jalizi, vishazi elezi na vishazi rejeshi. Hii ni kwa
mujibu wa Luraghi na Parodi (2008:76), wanafafanua kuwa vishazi vyenye sifa
hizi ni vishazi tegemezi pekee.
Pia kwa kuzingatia kigezo cha kujitegemea, kuna aina
kuu mbili za vishazi ambavyo ni vishazi huru na vishazi tegemezi.
Kwa mujibu wa Chomi (2003:191), kishazi
huru ni kishazi chenye uwezo wa kutumika peke yake na kuleta maana kamili
katika mawasiliano bila kutegemea kishazi kingine kwa mfano;
i)mtoto anatembea
ii)Waacheni watoto waje kwangu.
Mifano
iliyopo hapo juu ni vishazi huru ambavyo havihitaji vishazi tegemezi
kukamilisha maaana.
Kwa mujibu wa Obuch (2015:119), kishazi
tegemezi ni kishazi kisicho kamili ambacho huweza kutegemea kishazi huru ili
kikamilike. Hivi ni kusema kuwa vishazi tegemezi haviwezi kutokea peke yake
kama tungo au sentensi kamili. Kishazi tegemezi hutoa
habari ya ziada kuhusu kishazi huru kwa mfano;
i)Sentensi : mwalimu aliyekuja jana
amepotea
Kishazi
tegemezi: mwalimu aliyekuja jana.
ii)Sentensi :Mbuzi aliyepotea jana amepatikana
Kishazi
tegemezi:mbuzi aliyepotea jana
Yafuatayo ni mambo yanayosababisha
utegemezi wa vishazi tegemezi;
Uwepo
wa viambishi rejeshi, kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999:26) anasema kuwa
ni viambishi ambavyo hurejerea kwenye kirai nomino kinachokibeba. Vviambishi
hivyo husababishwa na o -rejeshi ambavyo inapachikwa katika mzizi wa kitenzi,
mfano wa viambishi rejeshi ni kama vile
–ye,-cho,-ko,-vyo,-nakadhalika.Viambishi hivyo vinavyopachikwa kwenye mzizi wa
kitenzi huweza kukishusha kitenzi hadhi nakufanya kiwe tegemezi na kusababisha
utegemezi katiaka tungo.
I) kiti kilichovunjika jana, kimepatikana.
II) N`gombe aliyepoteajana, amepatikana.
III) Gari lililopita jana,lilianguka
Hivyo maneno yaliyokolezwa wino ni
viambishi rejeshi vya o rejeshi vilivyosababisha vishazi hivyo kuwa tegemezi na
maneno yaliyopigiwa mstari ni vishazi tegemezi.
Aidha uwepo wa viambishi vinavyodokeza
hali ya masharti, hivi ni viambishi vinvyoonesha kuwa ili tendo fulani
lifanyike yapasa kitu fulani kifanyike kwa maana kwamba ili tukio fulani
litokee hadi masharti fulani yatimizwe. Kwa mujibu wa Massamba (kashatajwa),
anabainisha viambishi vya masharti kuwa ni kama vile, ki, ngali na ngeli.
Viambishi hivi vinapopachikwa ndani ya kitenzi hubadili hadhi yake kwa mfano:
i)Tungelikimbia mapema, tungelipona
ii)Akifundisha vizuri, tutafaulu
iii)Wananchi
wakinichagua, kawatajuta
Katika mifano hiyo hapo juu maneno
yaliyokolezwa wino ni viambishi vya masharti vilivyopachikwa katika kitenzi na
kuleta mabadiliko ya kitenzi na kusababisha kushushwa hadhi kitenzi na maneno
yaliyopigiwa mstari ni vishazi tegemezi.
Vilevile matumizi ya kiambishi “KU”,
husabasha utegemezi, Matei keshatajwa anasema vishazi tegemezi vinavyoundwa na
kiambishi “Ku” (kitenzi kisoukomo) huundwa kwa kitenzi jina. Kiambishi hichi
kinapopachikwa katika viteni hushusha hadhi vitenzi hivyo, na kuvifanya kuwa
vitenzi jina. Mfano ;
i)kuimba kwake, kunafurahisha
ii)kusoma kwake
kunasidia
iii)kupenda kwake kunafurahisha
Hivyo basi vitenzi kama vile imba, soma
na penda vimeshushwa hadhi na kubeba utegemezi baada ya kuambikwa kiambishi kuna
kusababisha kishazi tegemezi kutokea.
Aidha kishazi tegemezi husababishwa na
ujazilizaji, Kamusi Pevu ya Kiswahili wanafasili ujazilizaji kuwa ni upachikaji
au uongezaji wa vipashio katika tungo ili kutoa taarifa fulani. Kishazi
tegemezi hutumikakujaliza kiarifu cha kishazi kikuu kwa mfano;
i)mwalimu ametangaza kuwa
jaribio litafanyika wiki ijayo
ii)mtoto
anakula huku mama anaosha vyombo
iii)Raisi
ametangaza kuwa waziri atakuja kesho
Hivyo basi maneno kama vile kuwa na
kwamba yanayotokea katika upande wa kiarifu
yanaonesha vijalizo vya kiarifu cha kishazi kikuu. Ambavyo vinapelekea
kishazi kushushwa hadhi na kuwa tegemezi.
Vilevile uwepo wa maneno tegemezi ambayo
mara nyingine hujulikana kama viunganishi tegemeziambavyo hutumika kuunganisha
vishazi huru na vishazi tegemezi, baadhi ya maneno hayo ni kama vile,
ijapokuwa, endapo na ikiwa. Maneno hayo yakitumika husababisha kishazi kuwa
tegemezi. Massamba (keshatajwa), anaeleza kuwa utegemezi wa kishazi huweza
kupatikana kwa kutumia vishazi tegemezi vyenye muundo uliokitwa katika maneno
na ambavyo hutokea mwanzoni mwa kitenzi, nomino au kiwakilishi kinachounda
kishazi hicho. Kwa mfano:
i)Ijapokuwa hapendezi, mimi
nitamuoa
ii)Ili uende mbinguni ni lazima uwe mwema
Katika mifano hiyo, maneno yaliyokolezwa
wino ndiyo yaliyosababisha kishazi kushushwa hadhi na kuwa na hali ya
utegemezi, maneno yaliyopigiwa mstari ni kishazi tegemezi kilichosababishwa na
maneno yaliyopachikwa mwanzoni mwa sentensi.
Hivyo basi ingawa vishazi tegemezi
havitoi taarifa kamili, lakini huwa na dhima muhimu sana kwani vishazi tegemezi
hufanya kazi kama vijalizo vya nomino, aidha kishazi tegemezi katika sentensi
huweza kuongeza maana ya ziada katika kishazi huru.
MAREJELEO
Chomi, E.W (2003). Sarufi Miundo ya Kiswahili. Libya: Chuo Kikuu Cha Sebha.
Luraghi, S. na Parodi, C (2008). Key Terms in Syntax
and Syntactic Theory. New York: Continuum
International
Publishers
Massamba
na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu. Dar Es Salaam: TUKI.
Massamba, P.B (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar
Ea Salaam: TUKI.
Massamba na wenzake(2012).Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu, Secondari
na Vyuo. Dar Salaam:TUKI.
Matei, A.K (2008). Darubini ya Sarufi. Nairobi:Phoenix Publishers Limited.
Mulokozi, M.M (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar
Es Salaam.Moccony
Printing Press.
Obuch, S.M & Mukibiwana, A (2015). Muundo wa Kiswahili, Ngazi na Vipengel
Nairobi:Printing
Services Ltd.
Radford, A. (1998) Syntactic
theory and the Structure of English: A minimalist approach. Cambridge University
press
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com