kazi hii tumeigawa katika sehemu kuu nne ambazo ni utangulizi, kiini cha swali,
hitimisho pamoja na orodha ya vitabu tulivyotumia kukamilisha kazi hii. Katika
utangulizi tumeeleza dhana msingi ambazo zimejitokeza ambazo
ni fasihi ya watoto na ufaraguzi katika kiini tumetoa hoja madhubuti
zinazoshadadia kuwa bila mbinu ya ufaraguzi utunzi na uwasilishaji wa fasihi ya
watoto hautowezekana kabisa. Na mwisho tumetoa hitimisho maridhawa pamoja na orodha
ya vitabu vilivyotumika kukamilisha kazi hii.
Dhana ya ufaraguzi wamitila (2003)
anaeleza kuwa ni tendo la kutafuta au kuchukua kitu kilicho ili kukifanya
kichukue nafasi ya kingine ambacho hakiwezi kupatikana. Tukiingalia fasili hii
na kiihusisha na muktadha wa fashi wa watoto tunaona kuwa katika utunzi na
uwasilishaji wa fasihi ya watoto fanani hutumia akili yake kubadilika kuendana
na mazingira ili aweze kukidhi mahitaji hadhira yake.
Kwa ujumla tunasema ufaraguzi ni
ule ufundi wa papo kwa papo ambao mtunzi na mwasilishaji wa kazi ya fasihi ya
watoto hutumia, ambao hulenga kuibua hisia na kuburudisha hadhira husika ili iweze kunufaika na kazi
hiyo mfano kuchanganya nyimbo katika masimulizi ya hadithi pia kumia picha na
maandishi makubwa katika uandishi wa vitabu vya fasihi ya watoto.
Bakize (2002), Fasihi ya watoto ni
fasihi inayotungwa ama na watu wazima au watoto wenyewe yenye kutumia lugha na
kukusudiwa kusomwa au kutendwa na watoto. Wamitila (2013), anaeleza kuwa Fasihi
ya watoto ni fasihi inayoandikwa kwaajili ya watoto.
Lymo (2014), Fasihi ya watoto ni
dhana inayotumika kumaanisha kazi
za kifasihi ambazo zimetungwa kwaajili
ya kusomwa na utendwa na watoto, kazi
hizi ni pamoja na kazi za fasihi simulizi kama vile nyimbo, semi na kazi za fasihi
andishi kama vile riwaya, tamthilia ya ushairi.
Kwa ujumla fasihi ya watoto ni
fasihi maalumu iliyoandikwa kwa ajili ya watoto na huweza kuwa hadithi, ushairi
na drama. Lengo la fasihi hii ni kuburudisha na kuwaelimisha watoto. Ni kweli
kuwa bila mbinu ya ufaraguzi utunzi na uwasilishaji wa kazi ya fasihi ya watoto
hautowezekana kabisa kwa sababu mbinu hii inamchango mkubwa sana kwenye fasihi
ya watoto. Zifuatazo ni hoja zinazodhibitisha kuwa bila mbinu ya ufaraguzi,
utunzi na uwasilishaji wa kazi za fasihi ya watoto hautowezekana kabisa.
Ufaraguzi unasaidia uteuzi wa
wahusika; Wahusika katika katika kazi ya fasihi ni watendaji ambapo visa
vimejengwa juu yao. Katika kazi ya fasihi wahusika wanaweza kuwa binadamu, wanyama,
mimea, majitu, vitu na kadhalika. Katika fasihi ya watoto huwa kuna wahusika
watoto na watu wazima, wahusika hawa hupewa uhusika wao kulingana na kile
alichokusudia mtunzi hivyo mtunzi huamua kutumia wahusika wa aina fulani
kulingana na kile anachotaka kiwasilishwe kulingana na hadhira yake lakini pia
wahusika hutegemea muktadha au mazingira ya uwasilishaji.
Mfano katika kitabu cha Watoto Wanaofanana mwandishi ametumia
wahusika wanyama kama vile Sungura na Fisi katika simulizi ya Sungura na Fisi. Katika simulizi hii
mwandishi amewapa wanyama hawa uwezo wa kutenda kama binadamu ambapo Sungura na
Fisi walichorwa kama wazazi, walezi wanaowalea watoto wao pia walipewa uwezo wa
kuzungumza. Katika simulizi ya Buibui na
Sungura, mwandishi amemtumia mdudu Buibui kama mhusika ambapo alimpa uwezo
wa kibinadamu ambapo anatenda mambo tofautitofauti kama vile kuoa ambapo katika
hali ya kawaida hakuna mdudu anayeweza kuoa au kufunga ndoa.
Pia wahusika binadamu kutumika
katika kazi ya fasihi ya watoto wahusika hao wanaweza kuwa watoto wenyewe au
watu wazima. mfano katika kitabu cha Zinderza mwandishi amemchora mhusika
zindera kama mtoto, Sara kama mtu mzima ambaye alikuwa mama yake Zindera,
Mpanduji, Peter nakadhalika. Hivyo basi ubunifu wa wahusika katika fasihi ya
watoto husaidia kukuza umakini na hisia kwa hadhira iliyokusudiwa.
Uteuzi wa muundo katika kazi ya
fasihi ya watoto; Senkoro (2011) anaeleza kuwa muundo wa kazi ya fasihi ni
mpangilio na mtiririko wa visa na matukio. Pia anabainisha miundo miwili ambayo
ni muundo wa moja kwa moja na muundo usiokuwa wa moja kwa moja au changamani.
Muundo wa moja kwa moja ni muundo ambao hujenga visa katika mtiririko
unaoeleweka yaani mwisho wa kisa kimoja huwa ni mwendelezo wa kisa kingine,
lakini muundo changamani ni muundo wa kiurejeshi ambao huweza ama kumrudisha
nyuma msomaji au msikilizaji au mtazamaji katika mpangilio matukio yake.
Ufaraguzi humsaidia mwandishi au
msimuliaji kuteua muundo sahihi kulingana na muktadha aliopo. Katika fasihi ya
watoto muundo wake huwa ni wa moja kwa moja ambapo visa na matukio hupangwa
katika mtiririko unaoeleweka mfano katika kitabu cha Safari ya Prospa mwandishi ametumia muundo wa moja kwa moja kueleza
visa na matukio. Mwandishi anaeleza jinsi Merisho alivyopotea katika mazingira
ya kutatanisha kisha akaeleza jitihada za Prospa kumtafuta Merisho amabaye
alikuwa mtoto wa dada yake hivyo hadi mwisho Prospa anafanikiwa katika safari
yake.
Pia katika kitabu cha Zindera mwandishi ameeleza matukio yake
moja kwa moja kuanzia Sara alipokuwa alipoolewa na Mpanduji, alivyomzaa Zindera
aivyopoteana na mwanae mpaka mwisho ambapo walikutana tena na kuishi pamoja
hadithi nyingine zenye muundo wa moja kwa moja ni kama vile sungura na fisi, buibui na sungura, watoto
wanaofanana mwanamke asiye uliza na nyinginezo. Katika fasihi simulizi
watoto husimuliana visa katika mtiririko wa moja kwa moja. Hivyo basi ubunifu
wa muundo wa moja kwa moja humsaidia mtoto kuelewa kazi husika lakini humpa
hamu ya kuendelea kusoma au kusikiliza ili afahamu jinsi kisa hicho
kitakavyoishia na hivyo kama hadithi ililenga kuelimisha, kuburudisha, kuonya
au kueleza maadili itamfikia hadhira amabaye ni mtoto kwa ufasaha zaidi.
Uteuzi wa mtindo katika kazi ya
fasihi watoto; Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia (2003) wanaeleza kuwa
mtindo ni dhana inayojieleza jinsi mwandishi au mtunzi anavyojieleza mwenyewe.
Pia mtindo ni ukiushi, uteuzi, nyongeza, mazoea au kaida. Mtindo ndio
unaotuwezesha kwa kiasi kikubwa kupata utofauti wa mwandishi mmoja na mwingine
au kazi moja na nyingine. Mtindo huhusisha jinsi au namna ya kanuni katika
kujenga wahusika wake, jinsi anavyoanza na kumaliza visa vyake, jinsi
anavyotumia lugha, jinsi anavyowasilisha ujumbe wake kwa hadhira. Katika fasihi
ya watoto waandishi na wasimuliaji hutumia mitindo tofautitofauti ili kufikisha
ujumbe wake kwa hadhira.
Mifano ya mitindo hiyo ni matumizi
ya nyimbo kwenye simulizi, matumizi ya picha, matumizi ya barua, majibizano
katika masimulizi na kadhalika. Mfano katika kitabu cha Watoto Wanaofanana simulizi ya Sungura
na Fisi ukurasa wa kwanza mwandishi ametumia picha pia katika simulizi ya Mwanamke Asiyeuliza ukurasa wa tano, Buibui na Sungura ukurasa wa sita, Wivu Unaua ukurasa wa kumi nanane.
Katika fasihi ya watoto mwandishi huweza kutumia mtindo wa nyimbo kufikisha
ujumbe mfano katika kitabu cha Mbawala na
Nchi ya Ujinga ukurasa wa sita mwandishi ametumia wimbo.
Mama
yako mkatili, nyayangunga,
Kanichimbia
shimoni, ngayangunga,
Sitamsahau
ngayangunga yeye anguyanguza
Mkeo
mkatili, ngayangunga
Kanichimbia
shimoni ngayangunga
Kanizika ni hai, ngayangunga
Sitamsahau
ngayangunga yeye aguyaguza
Katika fasihi ya watoto mwandishi huweza
kutumia dailojia au majibizano mfano katika kitabu Kinyume cha Matarajio katika simulizi hii mwandishi amejengga
simulizi yake katika mtindo wa ushairi ambapo ndani yake kuna majibizano mfano
katuka ukurasa wa kumi kuna majibizano kati ya pili na mwalimu.
Ninakusihi
mwalimu
Yaishie
humuhum’
Baba
akiyafahamu’
.
Shule
sitaendelea.
Nimekusikia
pili’
Kwa
hiyo yako kauli’
Ni
kweli hastahili’
Siri
yetu kuijua
Katika fasihi ya watoto matumizi ya
picha na vielelezo humsaidia mtoto kupata taarifa ya ziada kuhusu kile
kilichozungumzwa pia humsaidia mtoto kuelewa kwa sababu humsaidia kutunza
kumbukumbu kwa mda mrefu tofauti na pale asingepata picha, pia humsaidia mtoto
kupata moyo wa kuendelea kusoma au kusikiliza kwa makini kazi husika
.
Uteuzi wa lugha; Ufaraguzi
humsaidia mwandishi na mtunzi kuteua lugha kulingana na muktadha na mazingira
ambapo kazi husika ya fasihi inatendeka. Lugha ya kifasihi hutofautiana na
lugha ya kawaida. Katika fasihi ya watoto lugha huwa ni rahisi ila yenye mvuto
kulingana na ngazi ya watoto. Kwa mujibu wa mradi wa vitabu vya fasihi ya
watoto vinaweza kugawanyika katika ngazi tatu ambapo ngazi ya kwanza
inajumuisha darasa la kwanza na la pili’ ngazi ya pili ni darasa la tatu na la
nne na ngazi ya tatu ni darasa la tano, sita na saba. Kahigi (1997) anaeleza
kuwa kitabu cha ngazi ya kwanza huwa na sentensi chache na rahisi ukilinganisha
na vitabu vya ngazi nyingine hivyo katika fasihi ya watoto mwandishi au
msimulizi hutumia lugha rahisi ambayo huchangia kumfanya mtoto aweze kufuatilia
na hatimaye kuelewa kilichokusudiwa na fanani wa kazi husika bila kuchoka
haraka hivyo basi mwandishi wa msimuliaji anatakiwa aepuke lugha ya mafumbo au
yenye tamathali za semi hasa kwa watoto wa ngazi ya chini.
Uteuzi wa mandhari; Wamitila (2008) anaeleza
kuwa mandhari ni wakati na mazingira ambapo kazi ya fasihi imetolewa. Mandhari
katika fasihi ya watoto huweza kuwa halisi au ya kubuni. Ufaraguzi humsaidia
fanani kuelewa mandhari kulingana na mazingira au muktadha mafano katika kitabu
cha Safari ya Prospa mwandishi
ametumia mandhari halisi kueleza visa na matukio ya kazi yake. Ametumia mandhari
ya halisi kama vile TPC, Moshi, Kisangara, Same, Manzese, Unguja na kadhalika.
Pia mawanndishi wa fasihi ya watoto huweza kutumia mandhari ya kubuni mfano
katika hadithi ya Sungura na Buibui mwandishi
ametumia mandhari ya Mbinguni ambapo Buibui alienda kutafuta mke. Pia katka
kitabu cha Mbawala na Nchi ya Ujinga kwenye
hadithi ya Katutu na Chawivu na Tongoza mwandishi ametumia
mandhari ya kubuni.
Kwa kuhitimisha ni kwamba mbinu ya
ufaraguzi katika utunzi na uwasilishaji wa kazi ya fasihi ya watoto ina faida
zifuatazo moja humsaidia mtunzi na mwasilishaji kufupisha kazi yake, mbili
husaidia kuvuta hisia na kuongeza umakini kwa hadhira, tatu humsaidia mtunzi na
mwasilishaji kutenga viwango vya hadhira pia mbinu hii humsaidia mtunzi na
mwasilishaji kukidhi mabadiliko ya kijamii kulingana na muktadha wa masimulizi.
MAREJEREO
Lyimo E.B (2014)” Ubaguzi wa kijinsia katika
vitabu vya Kiswahili vya fasihi ya watoto na mtazamo wa medani nchini Tanzanina “ Taasisi ya PhD
chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Wamitika K.W (2013) “Kamusi ya fasihi,Istilahi na Nadhania .Nairobi foans publishers.
Bakize L.(2013) Changamoto zinazoikabili fasihi ya watoto
Tanzania katika Kiswahili. Jalida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili 76 (uk
61-70) TATAKI.
Sabuni
E.G (2008) “Zindera Dar es salaam Tanzania solution publishers.
Mulokozi M.M (2014) Ngome mianzi; Dar es Salaam Tanzania
“KAUTU l.t.d
Mulokozi M.M (2017) Utangulizi wa fasihi ya Kiswahili; Dar es Salaam KAUTTU Paplisher
l.t.d.
Omari S, na Mtikatia S.e (2006) Watoto wanaofanana; Dar es Salaam ,Taasisi ya uchaguzi wa Kiswahili
Chuo kikuu Dar es Salaam.
Omari S, na Mnikaria S.E (2006) Mbawala na Nchi ya Ujinga ; Dar es
Salaam,Taasisi
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com