Flower
Flower

Wednesday, June 19, 2019

FONOLOJIA NA MICHAKATO YAKE

TUKI (2004), wanaeleza kuwa michakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu fulani kufikiwa. Hivyo katika uwanja hu wa fonolojia tunaweza kuwa mchakato unaweza kufanyika pale ambapo fonimu mbili zinapokutanishwa na huweza kutokea mabadiliko fulani katika fonimu mojawapo.

Massamba na wenzake (2007) wanasema kuwa kanuni ni taratibu maalum zinazosababisha mabadiliko ya sauti katika lugha husika.

Massamba (2011) anasema kuwa kuna michakato ya aina mbili ambayo ni michakato ya kiusilimisho na michakato isiyo ya kiusilimisho. Miongoni mwa michakato ya kiusilimisho ni kama ifuatayo:

Ifuatayo ni data tutakayotumia katika kazi hii
Umbo la ndani                                umbo la nje
/ mu + alimu /                                 [ mwalimu ]
/ mu + anafunzi /                          [ mwanafunzi ]
/ mu + ana /                                 [ mwana ]
 /Nbaya/                                          [mbaya]
  /Nbuga/                                         [mbuga]
  / mama /                                        [ mãmã ]
  / nyanya /                                      [nyãnyã
/ ki + angu /                                    [ change ]
/ ki + etu /                                       [ chetu ]
/ ki + ako /                                       [ chako ]
/ pa+ingine /                                    [ pengine ]
/ waingi /                                          [wengi]
/ waizi /                                             [ wezi
/Mu+japani/                                      [Mjapani]
/Mu+tu/                                            [ Mtu]
/Mu+gonjwa/                                    [ Mgonjwa]
/Mu+taalamu/                                   [Mtaalamu]

Uyeyushaji, Kwa mujibu wa Mgullu (1999) anasema kuwa huu ni mchakato unaoelezea mabadiliko ya sauti na kuwa kiyeyeyusho (y au w). Irabu za juu ambayo ni (u na i) ikifuatana na irabu isiyofanana nayo katika neno, irabu hiyo hubadilika na kuwa kiyeyeusho kwa mfano


Umbo la ndani                                umbo la nje
/ mu + alimu /                                  [mwalimu ]
/ mu + anafunzi /                            [ mwanafunzi ]
/ mu + ana /                                     [ mwana ]

Katika data hiyo hapo juu inaonesha wazi kwamba irabu ya juu nyuma /u/ imebadilika na kuwa kiyeyusho /w/ kutokana na kufuatiwa na irabu ambayo haifanani nayo. Mchakato huu unaweza kuoneshwa na sharia / kanuni ifuatayo:
/ u / → [ w ] / − I   ≠u

+sila                    -sila                         +sila
+juu             →    -kons            ∕ ─      +nyuma
+nyuma               +kk laini                 +chini
- mviringo

Aidha irabu ya juu mbele / i / inabadilika na kuwa kiyeyusho / y / kama inavyooneshwa katika data ifuatayo:
/ Mi + aka /                                              [ myaka ]
/ mi + anzo /                                             [ myanzo ]

Hivyo mchakato huo hunaweza kuoneshwa kwa kanuni ifuatayo:
/ i / → [y]  /   I  ≠i
+ sila-sila      +sila
 + Juu      →  -kons   ∕               ─+nyuma
 + mbele        +kk gumu            +chini     



Mchakato mwingine ni wa konsonanti kuathiri nazali (usilimisho pamwe wa nazali). Massamba na wenzake (2007) wanaeleza kuwa katika lugha ya Kiswahili sanifu, na kwa hakika katikalugha nyingi za kibantu, umbo la sauti la nazali huathiriwa na konsonanti inayoliandamia. Mchakato huu unajidhihirisha latika data zifuatazo:
Umbo la ndani                                             Umbo la nje
/Nbaya/ [mbaya]
/Nbuga/ [mbuga]

Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:
N→[m] ∕ ─/b/
+kons                   +kons               +kons
+nazali        →      +nazali       ∕ ─  +midomo
+ufizi                    +ant                  -nazali




Katika data hizo fonimu n imebadilika kuwa fonimu  m katika mazingira ya kufuatiwa na konsonanti /b/. kwahiyo, sauti n ambayo ni ya ufizi imefuata mahali pa matamshi pa /b/ ambayo na ya mdomo

Mchakato mwingine ni unazalishaji wa irabu, Massamba (1996), anafafanua kuwa ni aina ya usilimisho ambao irabu inachukua sifa za unazali kutokana na kuwa kwake karibu na nazali. Unazalishaji huoneshwa kwa alama ya kiwimbi [ ~ ] juu ya sauti ambayo imepitia mchakato huo. Mchakato huu unajidhihirisha katika data zifuatazo :
Umbo la ndani                                 Umbo la nje
a)/ mama /                                        [ mãmã ]
b)/ nyanya /                                      [nyãnyã ]
Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:

(a)    +sila                      +sila                     +kons
        +nyuma         →     +nyuma        ∕       +nazali        
         +chini                    +chini                   +midomo
                                    +unazali
(b)
+sila                        +sila                  +kons            
+nyuma         →      +nyuma       ∕     +kk laini         ─
+chini                      +chini               +nazali
                                            +unazali
Katika data (a) na (b) irabu /a/ imepata sifa ya unazali kwa kutanguliwa na fonimu /m/  na fonimu /ը/.
Hivyo basi katika mifano hiyo tunaona kuwa irabu zilizo karibu na konsonanti nazali zimepata sifa ya unazali, hii inamaana kuwa irabu itapata sifa ya unazali kama itatanguliwa au kufuatiwa na konsonanti ambayo ni nazali.

Mchakato mwingine ni ukakaishaji, Massamba, anasema kuwa hii ni aina ya usilimisho wa konsonanti , Massamba ( 2007) akimrejelea Lass (1984) anaeleza kwamba ukakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu zisizo za kaakaa gumu zinapobadilika  na kuwa za kaakaa gumu. Lugha ya Kiswahili inafonimu mbili tu za kaakaa gumu ambazo ni / ᶡ / na / t /. Vilevile Mgulu (1999), anafafanua kuwa ukakaishaji katika lugha ya Kiswahili ni kitendo cha fonimu ambazo si vizuio kwamizwa kubadilika na kuwa vizuio kwamizwa.  Kama inavyooneshwa katika data ifuatayo:
Umbo la ndani                                       Umbo la nje
a)/ ki + angu /                                           [ change ]
b)/ ki + etu /                                              [ chetu ]
c)/ ki + ako /                                               [ chako ]
Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:
/ k / →            [ t s]   /   /i/ + I≠ /i/
+kons              +kons                      +sila                     +sila
                            +kizuiw             +kiz kwamz            +mbele                  +chini
+kk laini     →      +kk gumu            +juu            +       +nyuma
-ghuna                  -ghuna                -viringo               -viringo

Katika data (a) na (c), fonimu /k/ imebadilika na kuwa fonimu /t/ katika mazingira ya kufuatiwa na fonimu /i/ katika mpaka mwa irabu /a/.
Pia katiak data (b), fonimu /k/ imebadilika kuwa /t/ katika mazingira ya kufuatiwa na irabu /i/ katika mpaka wa irabu /e/.

Mvutano wa irabu/ muunganiko wa irabu, kwa mujibu wa massamba (2007) anaeleza kuwa kuna mabadiliko mengine ya sauti yanayohusu irabu lakini ambayo hayahusu irabu kudondoshwa au kugeuka kuwa kiyeyusho. Upo pia uwezekano wa irabu ya fonimu moja kukabiliana na irabu ya fonimu nyingine kisha irabu hizo mbili zikaungana na kuzaa irabu moja tu.Mchakato huu unajidhihirisha katika data zifuatazo :
Umbo la ndani                          umbo la nje
/ pa+ingine /                             [ pengine ]
/ waingi /                                [wengi]
/ waizi /                                   [ wezi ]
Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:
/ a/ + /i / → [ ƹ ]
                                                     +sila          +sila                  +sila                      
    +chini             +juu              +mbele
    +nyuma     + mbele      →  nusu- juu
                                                  -viring          -viring               -virng
Katika data hizo, fonimu /a/ na /i/ zimeungana na kuunda irabu nyingine isiyofanana nazo ambayo ni [ ƹ ]

Mchakato wa udondoshaji, Massamba na wenzake (keshatajwa) anasema kuwa mchakato huu unahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati fonimu mbili zinapokabiliana, yaani katika mazingira hayo sauti ambayo hapo awali ilikuwepo hutoweka. Hii inajidhihirisha katika data ifuatayo:
Umbo la ndani                                 Umbo la nje
(a)/Mu+japani/                                    [Mjapani]
                                        (b)/Mu+tu/                                          [ Mtu]
(c)/Mu+gonjwa/                                 [ Mgonjwa]
 (d) /Mu+taalamu/                               [Mtaalamu]

Katika data (a) (b) na (C) fonimu /u/ imedondoshwa na kuwa kapa katika mazingira ambayo imetanguliwa na nazali /m/ na kufuatiwa na konsonanti halisi. Pia katika data (d), fonimu /u/ ya mwisho imedondoshwa na kuwa kapa katika mazingira ya kutanguliwa na nazali /m/.
Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:
 Katika data (b),     /u/→[ᴓ] ∕−/t/
          +sila                               +kons
        +juu                               -ghuna
        +nyuma        →[ᴓ] ∕          +fizi
        +viringe                          -nazali
Katika data (d), /u/→[ᴓ] ∕  /m/
        +sila                             +kons
        +juu                             +nazali
        +nyuma       → [ᴓ] ∕     +midomo      
        +viringe


Katika data hizo, data (b) fonimu /u/ imekuwa kapa katika mazingira ya kufuatiwa na konsonanti halisi ambayo ni /t/. Vilevile katika data (d) fonimu /u/ imekuwa kapa katika mazingira ambayo imetanguliwa na nazali /m/.

Mchakato wa tangamano la irabu. Massamba na wenzake (keshatajwa) wanasema ni hile hali ya mabadiliko sauti husababishwa na hali ya utangamano ambayo hujitokeza katka baadhi ya vitamkwa. Yaani kunakuwa na namna fulani ya kufanana au kukubaliana kwa vitamkwa ambavyo ni jirani. Hii inajidhihirisha katika data ifuatayo;
                         Umbo la ndani            umbo la nje
                       / Cheka/                              [ chekea]
Kutokana na data hizo, tunaweza kufafanua kanuni na mazingira ya ubalikaji wa sauti kama ifuatavyo:
+sila                           +kons                 +sila                   +kons               +sila
-kons       → [ ƹ ]∕        +kk gumu           +nusu juu          +kk laini           +chini
                                   -ghuna                +mbele              -ghuna           +nyuma          


Katika data hiyo, irabu ya utendea imebadilika na kuwa irabu ya utendea  [ ƹ ]
Kwa ujumla, katika lugha ya Kiswahili mabadiliko ya sauti hayatokei tu, isipokuwa hutokea sambamba na michakato na kanuni inayohusika na mabadiliko hayo.


                                                       MAREJELEO
Massamba, D.P.B na wenzake (2007) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Mgullu, R.S (1999) Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi;         
                                Longhorn Publishers.
Massamba D.P.B (2011) Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI

























No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny