ni sauti inavyoumbwa,
inavyosafiri na inavyotafsriwa katika ubongo wa msikilizaji. Vilevile, katika
ufasili wa dhana ya fonolojia wataalamu hawa wanasigana kwani de Courtenay
anasema kwamba fonolojia ni ule uwanja unaoshughulikia sauti kama
inavyokusudiwa katika ubongo wa msemaji wakati Trubetzkoy anasema kwamba
fonolijia ni sayansi inayoshughulikia uamilifu na Katika kuifafanua dhana ya
fonimu tutajikita katika mitazamo mitatu kwa mujibu wa Hyman (1975) ambapo
anaeleza kuwa mtazamo wa kwanza kuwa fonimu ni tukio la kifonetiki, mtazamo huu
wa fonimu kama tukio la kifonetiki unatetewa na wanaisimu kama Daniel Jones
(1975) pale anaposema:- Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani lenye
sauti muhimu yaani phonemes pamoja na
sauti zinazohusoiana na ambazo hutumiwa mahali pake katika muktadha
maalumu.Jones anaendelea kueleza kuwa fonimu ni huwakilisha umbo halisi la
kifonetiki na sauti zilizo katika fonimu moja huwa na sifa muhimu za kifonetiki
zinazofanana. Tunapoyachunguza maelezo ya Jones hapo juu tunaona ya kuwa
yanatilia mkazo suala la sifa za kifonetiki za fonimu.
Vilevile, dhana ya fonimu kama tukio la
kisaikolojia, mtazamo huu unaungwa mkono na Noam Chomsky ambaye alidai kuwa mtu
anapojifunza lugha huanzia na umilisi ambao ni msimbo uliopo akilini mwa mtu
ambao hutumiwa wakati wote mtu anapoongea. Pia mtazamo huu unaungwa mkono na de
Courtenay (1952) pale anaposema kuwa fonimu ni tukio la akilini ambalo huwa na
nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji anavyomuelewa mzungumzaji au vyote kwa
wakati mmoja. Anaendelea kueleza kuwa fonimu ni kipande cha sauti ambacho picha
yake huwa akilini mwa mtu ambaye hukusudia aitoe wakati anapoongea.
Pia,
dhana ya fonimu imeelezwa kama tukio la kifonolojia, mtazamo huu unashadidiwa
na Trubetzkoy pale anaposema, fonimu haiwezi kufasiliwa kikamilifu ama kwa
kutumia kigezo cha sifa za kisaikoloji au sifa za kifonetiki bali ni lazima
ifasiliwe kwa kutumia sifa za uamilifu wa fonimu hiyo katika mfumo wa fonolojia
ya lugha maalumu inayotumika, mfano /z/ + /a/ + /a/ pamoja na /k/ + /a/ + /a/
kwahiyo hapa mkazo unatiliwa katika kaza mbalimbali zinazofanywa na fonimu
katika lugha maalumu.
Kwa
ujumla tunaweza kusema kuwa dhana ya fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha
kifonolojia chenye uwezo wa kubadili maana ya neno au kupoteza kabisa maana
hiyo.
Uchanganuzi
wa sauti za lugha katika nadharia ya fonimu imejadiliwa vyema na wataalamu
mbalimbali kama vile Baudouin de Courtenay pamoja na Nikoloj Trubetzkoy ambao
wataalamu hawa wanafanana na kutofautiana katika suala zima la uchanganuzi wa
sauti lugha katika nadharia ya fonimu.
Baudouin
de Courtenay mtaalamu huyu alizaliwa huko Radzymin Poland (1845). Kwa mujibu wa
Jones (1975) anaeleza kuwa de Courtenay alianza kushughulika na nadharia yafonimu na ubadilishanaji wa kifonetikimnamo
mwaka (1868). Katika uchunguzi wa de Courtenay (1868) anaweka bayana tofauti ya
sauti kama zinavyobainishwa na wasemaji wa lugha yaani katika bongo zao na
sauti kama vitu halisi kama vinavyotamkwa. De Courtenay pia anadai kuwa kuna
mambo mawili yanayochunguzwa katika uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa lugha
kileo, anaendelea kueleza kuwa ule uwanja unaoshughulikia sauti za lugha
zinazotamkwa na msemaji hujulikana hii leo kama fonetiki (anthropofoniki) na
ule uwanja unaoshughulikia sauti kama zinavyokusudiwa katika ubongo wa msemaji
hujulikana hii leo kama fonolojia (saikofonetiki).
Vilevile,
Trubetzkoy kwa mujibu wa Massamba (2002) anadai kuwa huyu ni miongoni mwa wanafunzi
kutoka katika shule ya prague ambaye anafuta nyayo za Dessausure alibainisha
matawi yanayoshughulikia sauti, matawi hayo ni pamoja na fonetiki na fonolojia.
Massamba (keshatajwa) anendelea kueleza kuwa Trubetzkoy alifasili dhana ya
fonetiki kama sayansi inayoshughulikia sauti katika uumbwaji wake halisi
kifiziolojia, kiakustika na kimasikizi, vilevile alifasili dhana ya fonolojia
kama ni sayansi inayoshughulikia uamilifu na utofautishaji wa sauti katika
mfumo wa lugha. Pia Massamba anaendelea kueleza kuwa Trubetzkoy aliamini kuwa
fonetoiki na fonolojia ni nyanja zinazorejeleana.
Katika
uchanganuzi wa sauti za lugha katika nadharia ya fonimu wataalamu hawa
wanafanana kwa mambo kadha wa kadha kama vile:-
Trubetzkoy
na de Courtenay wote wanachunguza sauti kwa kutumia matawi mawili, matawi hayo
ni fonolojia na fonetiki. Kwa mujibu wa Massamba (2012) anaeleza kuwa de
Courtenay anadai kwamba kuna mambo mawili yanayochunguzwa katika uchunguzi na
uchanganuzi wa lugha kileo; kuchunguza kile kinachokusudiwa katika ubongo wa
msemaji. Massamba (2012) anaendelea kueleza kuwa de Courtenay ule uwanja
ulioshughulikia sauti kama zinzvyotamkwa na msemaji hujulikana leo hii kama
fonetiki (Antropofoniki). Vilevile, de Courtenay anaeleza kuwa ule uwnja
unaoshughulikia sauti kama zinavyokusudiwa katika ubongo wa msemaji hujulikana
hii leo kama fonolojia (saikofonetiki) vilevile Trubetzkoy kwa mujibu wa
Massamba (kashatajwa) anabainisha matawi mawili yanayoshughulikia sauti ambapo
tawi la kwanza ni fonetiki ambayo yeye alieleza kuwa ni sayansi
inayoshughulikia sauti katika uumbwaji wake halisikifiziolojia, kiakustika na
kimasikizi. Tawi la pili ni fonolojia ambalo yeye alifasili kama ni sayansi
inayoshughulikia uamilifu na utofautishaji wa sauti katika mfumo wa lugha.
Ukiwachunguza wataalamu hawa utaona kuwa wanakubaliana kwamba unapochunguza
sauti za lugha sharti uzingatie matawi yote mawili ambayo ni fonetiki na
fonolojia.
De
Courtenay na Trubetzkoy wote wanakubaliana kwamba dhana ya fonimu yaweza
kufasiliwa kama tukio la kisaikolojia, Mgullu (2001) akimnukuu de Courtenay
anaeleza kwamba fonimu ni tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au
jinsi msikilizaji anavyomuelewa mzungumzaji au vyote kwa pamoja. Anaendelea
kueleza kuwa watumiaji wa lugha fulani huzijua fonimu zote za lugha yao kwahiyo
watumiaji hao huwa wanataswira ya kila fonimu akilini mwao na kwa hali hiyo
fonimu ni taswira iliyo akilini mwa mzungumzaji, vilevile Trubetzkoy
akinukuliwa na Mgullu (keshatajwa) anasema kwamba fonimu hauwezi kufasiliwa
kikamilifu ama kwa kutumia kigezo cha sifa kisaikolojia au sifa za kifonetiki
bali lazima ifasiliwe kwa kutumia sifa za uamilifu wa fonimu hiyo katika mfumo
wa fonolojia ya lugha maalumu inayotumika. Ukichunguza maelezo ya Trubetzkoy
hapingi moja kwa moja kama fonimu ni tukio la kisaikolojia ila yeye anaongeza
tu kwamba inatakiwa ifasiliwe pia kwa
kuzingatia uamilifu wake.
Pamoja
na kukubaliana kwa mambo kadha wa kadha katika uchanganuzi wa sauti katika
nadharia ya fonimu pia de Courtenay na Trubetzkoy wanasigana katika mambo
yafuatayo:-
De
Courtenay na Trubetzkoy wanasigana katiaka kufasili dhana ya fonimu, kwa mujibu
wa Mgullu (keshatajwa) anaeleza kuwa de Courtenay anafasili dhana ya fonimu
kuwa ni tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji
anavyomuelewa mzungumzaji au vyote kwa pamoja, de Courtenay anaendelea kueleza
kuwa watumiaji wa lugha fulani huzijua fonimu zote za lugha yake. Kwahiyo
watumiaji hawa wana kila fonimu akilini mwao na kwa hali hiyo fonimu ni taswira
iliyo akilini mwa watumiaji wa lugha hiyo, wakati Trubetzkoy akinukuliwa na
Mgullu (keshatajwa) anasema kuwa fonimu haiwezi kufasiliwa kikamilifu ama kwa
kutumia kigezo cha sifa kisaikolojia au sifa kifonetiki bali lazima ifasiliwe
kwa kutumia sifa za uamilifu wa fonimu hiyo katika mfumo wa fonoloji yaani
fonimu kama kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia chenye uwezo wa kubadili
maana. Mfano, /z/ + /a/ + /a/ na /k/ + /a/ + /a/ kwahiyo hapo fonimu ambayo ina
uwezo wa kubadili maana ni /z/ na /k/. Hivyo ukichunguza fasili za wataalamu
hawa utaona kwamba de Courtenay anaamini kwamba fonimu ni tukio la kisaikolojia
wakati Trubetzkoy haamini hivyo bali yeye anaamini kuwa fonimu ni tukio la
kifonolojia.
Pia,
de Courtenay na Trubetzkoy wanasigana katika kufasili dhana ya fonetiki na
fonolojia, kwa mujibu wa Massamba (2012) akimnukuu de Courtenay anasema kwamba
fonetiki ni ule uwanja unaoshughulikia sauti kama zinavyotamkwa na msemaji
wakati Trubetzkoy yeye anadai kuwa fonetiki ni sayansi inayoshughulikia sauti
katika uumbwaji wake halisi kifiziolojia, kiakustika na kimasikizi.Hivyo,
katika kufasili dhana ya fonetiki wataalamu hawa wanasigana kwani de Courtenay
katika fasili yake anatilia mkazo hasa jinsi sauti inavyotamkwa na msemaji wa
lugha wakati Trubetzkoy anatilia mkazo katika fasili yake mambo matatu ambayo utofautishaji
wa sauti katika mfumo wa lugha. Hivyo, ukiwachunguza de Courtenay na Trubetzkoy
wanasigana katika mambo kadhaa kama uamilifu wa sauti katika mfumo wa lugha.
De
Courtenay na Trubetzkoy wanasigana katika mtazamo kuhusu kufanana na
kutofautiana kwa fonetiki na fonolojia katika kuchunguza sauti katika nadharia
ya fonimu, kwa mujibu wa Massamba (keshatajwa) akimnukuu de Courtenay anasema
kwamba kuna tofauti ya wazi baina ya sauti kama zinavyobainishwa na wasemaji wa
lugha yaani katika bongo zao na sauti kama vitu halisi vinavyotamkwa,
anaendelea kueleza kuwa matawi haya mawili yanajitegemea akiwa na maana ya kuwa
ni matawi mawili yasiyohusiana wakati Trubetzkoy anaamini kwamba fonetiki na
fonolojia si nyanja zinzotengana kabisa kwani zinarejeleana. Hivyo, Trubetzkoy
anasigana na de Courtenay kwani anaamini kwamba fonetiki na fonolojia ni
taaluma zinazorejeleana katika uchunguzi wa sauti katika nadharia ya fonimu
wakati de Courtenay anaamini kwamba ni taaluma zinazotengana katika uchunguzi
wa sauti katika nadharia ya fonimu.
Kwa
ujumla unavyochunguza sauti za lugha katika nadharia ya fonimu sharti
huzingatie matawi yote mawili ambayo ni fonetiki na fonolojia.
MAREJELEO
Massamba,
D.P.B, (2011). Nadharia ya Fonimu. Dar
es Salaam: TATAKI.
(2012).
Misingi ya Fonolojia.Dar es Salaam:
TATAKI.
Mgullu,R.
(2001). Mtalaa wa Isimu. Nairobi
Longhorn Publisher Limited.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com