Wamitila (2016:122) anaeleza fasili ya dhana utelezi inatokana na neno teleza, ambayo ina maana ya kutaka kuanguka hasa baada ya kukanyaga au kupita mahali penye utelezi. Mfano udongo wa mfinyanzi unateleza. Wanaendelea kueleza maana nyingine ya utelezi kuwa ni kufanya kosa au kutenda bahati mbaya. Mfano; Mwalimu aliteleza katika kuzungumza. Pamoja na kuwepo kwa fasili nyingi za dhana utelezi, kazi hii imejikita kuangalia fasili inayoendana na mawanda ya taaluma ya sintaksia.
Kwa mujibu wa Wamitila (2016:122) telezi ina maana ya mkanganyiko au mpishano uliopo baina ya wataalamu katika kufasili au kuelezea dhana fulani, maelezo haya yameegemea katika mawanda ya kitaaluma. Hivyo utelezi unaojitokeza katika kufasili dhana ya sintaksia ni kule kutokushikika kwa dhana hiyo, kwani kila mtaalamu anapojaribu kuifumbata dhana hiyo humponyoka. Suala ambalo limezua utata au kuibua utelezi kwani kila mtaalamu ameeleza kwa namna yake kwa kushadidia mawazo yake juu ya dhana ya sintaksia kama ifuatavyo;
TUKI (1990) wanaeleza kuwa, sintaksia ni tawi la sarufi linalojishughulisha na mpangilio na uhusiano wa vipashio katika sentensi. Wakati huo Massamba (2012:34) anaeleza kuwa, sintaksia huchunguza uhusiano wa kipashio kimoja na kingine katika sentensi za lugha fulani. Maelezo ya
TUKI (keshatajwa) kwa namna moja ama nyingine yanaelekeana na fasili ya Massamba (keshatajwa). Utelezi unaojitokeza ni kuwa, Massamba (keshatajwa) anaeleza sintaksia kwa kuegemea katika uhusiano wa kipashio kimoja na kingine katika sentensi ila TUKI (keshatajwa) wameelezea dhana ya sintaksia kwa kuegemea kwenye mpangilio pamoja na uhusiano wa vipashio kwa ujumla japokuwa, utofauti wao unajitokeza pale ambapo, TUKI (keshatajwa) hawajaeleza kuhusu kanuni na sheria zinazotakiwa kufuatwa kama ilivyo katika fasili ya (Massamba 2012:34).
Chomi (2003:01) taaluma ya sarufi miundo inahusika na maelezo ya sentensi kwa kuchunguza jinsi sentensi zinavyoundwa. Maelezo hayo yanahusisha mambo mengi yakiwemo ya msingi, baadhi ya mambo hayo ni; kueleza kategoria ya maneno, kueleza muundo wa sentensi kwa kutaja viambajengo vyake, kueleza uhusiano kati ya viambajengo vya sentensi kwa kutaja dhima au kazi za viambajengo hivyo, kueleza mfuatano wa maneno katika sentensi. Utelezi upo kwenye istilahi ametumia sarufi miundo wakati wataalamu wengine kama; Massamba (keshatajwa), Obuchi na Mukhwana (2015:136) na Besha (2007) wametumia neno sintaksia.
Besha (2007) ameeleza kuwa, sintaksia ni taaluma inayojishughulisha na uchambuzi wa muundo wa sentensi za lugha. Fasili ya Besha inaelekeana na fasili za wataalamu wengine kama Obuchi na Mukhwana (2015:136) ambao wanafasili kuwa, sintaksia ni kitengo cha kimuundo ambacho hushughulikia sentensi katika lugha. Katika fasili ya Obuchi na Mkhwana (2012:136) wameeleza kuhusu muunndo unaochunguzwa na sintaksia lakini hawajaeleza uhusiano wa vipashio namna vinavyoteuana ili kuleta maana inayokubalika katika lugha husika.

Habwe na Karanja (2012:125) wameeleza kuwa sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile; kategoria za maneno, vikundi na vishazi. Utelezi wa wataalamu hawa upo katika kueleza maana ya sintaksia kuwa, inashughulikia muundo wa sentensi pamoja na elementi zake. Kwani wameongeza kuwa taaluma ya sintaksia hushughulika zaidi na vipashio vya sentensi ambavyo wao wanaviita vikundi. Mfano vikundi vishazi na vikundi virai.
Massamba (2012:34) ameeleza kuwa, sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake. Massamba (keshatajwa) ameongeza kuwa katika utanzu huu kinachochunguzwa ni sheria au kanuni ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano (neno moja na jingine) kwa namna ambayo itafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.
BAKITA (2017:977) wanaeleza kuwa sintaksia ni taaluuma inayoshughulikia uhusiano wa maneno yaliyomo katika tungo au sentensi moja. Fasili hii imeeleza juu ya uhusiano wa maneno uliopo katika tungo bila kuangalia mpangilio wake.
Kwa mujibu wa fasili za wataalamu hawa, wameeleza baadhi ya vipengele katika taaluma ya sintaksia. Hivyo, tunakubaliana na fasili ya Massamba (2012) kwa sababu amezingatia vitu vya msingi ambavyo taaluma ya sintaksia inashughulika navyo kama vile; mpangilio wa maneno katika sentensi, uhusiano wa vipashio vyake, sheria na kanuni ambazo zinapaswa kufuatwa katika kuyapanga maneno hayo.

Kwa ujumla sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake kama vile neno, kirai na kishazi ambavyo ndivyo vinaunda sentensi, na namna vipashio hivyo vinavyoteuana ili kuleta maana iliyokamilika na yenye kueleweka katika lugha husika, kwa sababu kila lugha inautaratibu wake maalumu wa mpangilio wa maneno katika sentensi au tungo kwani maneno hayawezi kukaa kama shanga bali kwa kuteuana kati ya kipashio kimoja na kingine ili kuleta maana sahihi. Massamba (keshatajwa).
Katika kufasili dhana ya sintaksia kumekuwa na utelezi miongoni mwa wataalamu, ambapo chanzo cha utelezi huo usababishwa na mambo yafuatayo;
Kwanza, wataalamu wanakinzana katika kuelezea taaluma sintaksia inajishughulisha na nini? Kulingana na fasili za wataalamu hao Massamba (keshatajwa) anatilia mkazo kuwa sintaksia inajihusisha na kuchunguza mpangilio wa maneno katika sentensi na vipashio vyake wakati Besha (keshatajwa) anatilia mkazo sintaksia hujishughulisha na uchambuzi wa muundo wa sentensi. Hivyo kwa mitazamo hiyo ya wanataaluma hawa wanatofautiana katika matumizi ya istilahi ya mpangilio na muundo lakini wanaelezea kitu kimoja ambacho ni sintaksia.
Pili, wataalamu wanatofautina katika kuelezea asili ya neno sintaksia. Online Etimology Dictionary inaeleza kuwa neno sintaksia lilitokana na neno la Kifaransa ambalo ni Synta’xe na neno hilo limetokana na asili ya neno la Kilatini Syntaxis lenye maana ya kupanga au kuweka vitu pamoja katika mpangilio. Wakati Massamba na wenzake (2012:34) pamoja na kuifasili dhana ya sintaksia kuwa ni utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusisno wa vipashio vyake. Pia ameongeza kuwa katika utanzu huu kinachochunguzwa ni sheria au kanuni ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano. Hivyo, fasili ya Massamba na wenzake (keshatajwa) inavuka mipaka ya asili ya neno lenyewe sintaksia jambo ambalo linazua utata au kuibua utelezi katika dhana ya sintaksia.
Tatu, wataalamu wanakinzana katika kuelezea kanuni na sheria zinazopaswa kufuatwa katika taaluma ya kisintaksia. Wataalamu hawajaonesha wazi kuwa kanuni zipi na sheria zipi zifuatwe katika sintaksia, Chomi (2003) anaeleza kuwa ili tuchunge namna sentensi zinavyoundwa ni lazima tueleze kategoria za maneno, mfuatano, uhusiano wa viambajengo vyake kwa kuangalia kazi zake, wakati Massamba (2012) anaelezea kuwa katika sintaksia kinachochunguzwa ni sheria au kanuni ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano fulani yaani neno moja kulifuata neno lingine. Hivyo hawatofautiani sana isipokuwa, mtaalamu Massamba (keshatajwa) anaelezea kanuni na sheria ambazo hazina budi kufuatwa na mtaalamu Chomi (keshatajwa) anaeleza namna viambajengo vinavyoweza kufuatana na kuhusiana kikazi zaidi suala ambalo linaibua utelezi. Mfano;
a) Asha jana alikwenda sokoni b) Mwalimu ameenda darasani
c) Alikwenda Asha jana sokoni d) Mwalimu darasani ameenda
Sentesi (a) na (b) zinampangilio unaokubalika katika lugha ya Kiswahili kwa sababu katika lugha ya Kiswahili maneno huteuana yenyewe kwa namna inayokubalika kuwa neno lipi lianze na lipi lifuate, kama vile; nomino au kiwakilishi na kivumishi vinapoanza huteua maneno yenye kuhusiana nayo kama vitenzi na hata kuishia na vielezi wakati sentensi (c) na (d) mpangilio wake haukubaliki katika lugha ya Kiswahili kwa sababu namna maneno yalivyopangwa hayajateuana. Katika lugha ya Kiswahili huwezi kuanza na neno lenye sifa ya kitenzi au kielezi, bali huanza na nomino na neno linalotegemewa kufuatwa lazima liwe kitenzi au kivumishi kwa kufuata kanuni na sheria, katika taaluma ya sintaksia.

Nne, wataalamu wanakinzana katika kuelezea mpangilio wa maneno au vipashio katika sentensi. Wataalamu kama TUKI (1990) wanaelezea sintaksia kama mpangilio na uhusiano wa vipashio katika sentensi wakati, Besha (2007) ameeleza kuwa sintaksia inahusika na uchambuzi wa muundo wa sentensi za lugha. Kulingana na maelezo hayo, wataalamu wanatofautiana kueleza kuwa ni kipashio kipi kinachoungana na kipashio kingine ili kuunda sentensi, na vipashio hivyo ni vipi? Kwa ujumla kauli hizi zilizotolewa na wataalamu wameshindwa kuonesha bayana kuwa sintaksia inatazama muundo wa maneno katika sentensi au vipashio vingine kama muunganiko wa virai au vishazi suala linalosababisha utelezi.
Tano, wataalamu wanakinzana katika kuelezea mawanda ya sintaksia. Kila mtaalamu hajaeleza kuwa mawanda yasintaksia yanaanzia kiwango kipi katika taaluma ya lugha? Wataalamu wengi hawajaweka bayana kiwango kipi au kipashio kipi ambacho sintaksia inaanzia? Mfano Besha (keshatajwa) ameelezea sintaksia inaishia katika kiwango fulani yaani sentensi lakini hajaonesha kiwango cha chini cha sintaksia au kiwango ambacho sintaksia inaanzia. Wataalamu wengine hawajaeleza suala la mawanda suala linalosababisha utelezi.
Kwa ujumla, dhana ya sintaksia ni telezi kwa kiwango fulani, kwa sababu kila mtaalamu ameelezea kitu kimoja kwa namna yake, kwani kila mtaalamu anapojaribu kuifumbata dhana ya sintaksia inamponyoka kulingana na mipaka wanayokuwa wamejiwekea katika kuifasili dhana ya sintakisia.
Marejeleo
BAKITA (2017). Kamusi Kuu ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Pubrishers.
Besha, R. M. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Dar es Salaam
University Press.
Chomi, E.W. (2003). Utangulizi katika Sarufi Miundo ya Kiswahili. Sebha Libya: Chuo Kikuu
cha Sebha
Habwe, J. na Karanja, P. (2004). Misingi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.
Massamba na Wenzake (2012). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA) Sekondari na
Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Obuchi na Mukwana. (2015). Muundo wa Kiswahili Ngazi na Vipengele. Nairobi:
Printing Service Limited.
TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu. Dar es Salaam: TUKI & Philadelphia Benjamin.
Wamitila, K. W (2016). Kamusi Pevu ya Kiswahili. Nairobi: Vide~Muwa Publishers.

No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com