Data, kwa mujibu wakamusi ya isimu na falsafa
(2004;25) imefasili data kuwa ni jumla ya habari au taarifa zilizokusanywa kwa
ajili ya kufanyia uchunguziwa kipengele au vipengele maalum vya kiisimu. Pia
umbo la ndani kwa mujibu wa massamba na wenzake (2004:55) wanasema umbo la
ndani ni jinsi neno lenyewe lilivyoundwa
na mofimu zake mbalimbali. Michakato, massamba (2004:50 katika isimu ya
falsafa ya lugha, ni utaratibu ambao husababisha mabadiliko au mageuko ya kitu
kutoka umbo moja na kuingia umbo jingine. Na michakato ya kifonolojia ni hali
ya mabasdiliko ijitokezayo inapokuwa vitamkwa viwili hama vimekalibiana,
vimegusana au vimeathiriana. Massamba anasema ni utaratibu ambao hauna budi
kufuatwa katika uchambuzi na uchanganuzi wa lugha katika ngazi yoyote
inayohusika, utaratibu ambao ukifuatwa katika utokeaji wa mabadiliko au sula
fulani ya jambo hilo.
Kwa ujumla mtaalamu aliyegundua umbo la ndani
na la nje ni Naom Chomsky, pia uhusisha michakato na kanuni za kifonolojia kama
vile, udondoshaji, uchopekaji, ukakaishaji, usilimisho pamwe wa nazali na
muungano wa irabu.
Kutokana na data (a)
mgongo, (b) wezi, (c) woga, (d) chao, (e) salamu, (f) mvua, na (g) mvuvi. Yafuatayo
ni maumbo ndani na maumbo nje,
Umbo la nje umbo la ndani
(a)
Mgongo mu+gongo
(b)
Wezi / wa+izi/
(c)
Woga / u+oga/
(d)
Chao / ki+ao/
(e)
Salamu / salam/
(f)
Mvua /n+vua/
(g)
Mvivu /n+vivu/
Kutokana na
kuangalia maumbo ya ndani zifuatazo nui kanuni na michakato iliyojitokeza
katika data ihi,
Data (a) mgongo,
umbo lake la ndani ni /mu+gongo/ na mchakato wake uliojitokeza ni udondoshaji, kwa mujibu wa
Massamba na wenzake (2004:55) anasema kanuni hii inahusu kuachwa kwa sauti
fulani katika matamshi wakati mofimu mbili zinapokubaliana yaani katika
mazingira hayo sauti ambayo hapo awali ilikuwepo hutoweka. Pia kwa mujibu wa
Mugullu (1999:90) anasema irabu hudondoshwa zaidi pale ambapo irabu mbili au
zaidi zinazofanana huwa zimefuatana, tuseme penye shadda kla irabu kuliko
mahali pengine ambapo hapana shadda lolote la irabu. Kwa ujumla udondoshaji ni
moja kati ya michakato isiyo ya kisilimisho ambapo sauti hudondoshwa
inapokabiliwa na mazingira fulani ya kifonetiki.
Kutokana na fasili
hizo na data, kanuni iliyojitokeza katika mchakato wa udondoshaji katika data
hii ni kama ifuatavyo, /u/→ [Ө ]/m ―k,
irabu /u/ imebadilika na kuwa kapa katika mazingira ya kutanguliwa na nazali
[m] na kufuatiwa na konsonati halisi.
Data (b) wezi, umbo
lake la ndani ni /wa+izi/
na mchakato uliojitokeza ni muungano wa irabu. Muungano wa irabu kwa mujibu wa
Massamba na wenzake (2004:59) anasema ni uwezekano wa irabu ya mofimu moja
kukabiliana na irabu ya mofimu nyingine kisha irabu hizo mbili zikaungana na
kuzaa irabu moja tu. Kwa ujumla muungano wa irabu ni mchakato unayohusu
uunganishaji wa irabu mbili kuzalisha irabu nyingine mpya, hivyo kanuini ya
mchakato huu ni, /a/+/i/→ [ԑ]. Irabu /a/ na irabu /i/ zimekubaliana na
kuzalisha irabu mpya ambayo ni [ԑ].
Data (c) woga, umbo lake la ndani ni /u+woga/ na mchakato
uliojitokeza ni uyeyushaji. Uyeyushaji ni badiliko la irabu kuwa kiyeyusho,
katika kiswahili irabu za juu /i/ na /u/ zikifuatana na irabu isiyofanana nayo
katika neno hubadilika na kuwa kiyeyusho, irabu /u/ hubadilika na kuwa
kiyeyusho [w], na irabu /i/ hubadilika na kuwa kiyeyusho [j]. Hivyo kutokana na
data hii kanini yake inakuwa kama ifuatavyo, /u/→[w]/――I≠u. Sauti /u/
inabadilika kuwa [w] katika mazingira ya kufuatiwa na irabu isiyofanana na
irabu /u/.
Data (d) chao, umbo lake la ndani ni /ki+ao/ mchakato wake
uliojitokeza ni ukakaishaji, kwa mujibu wa Mgullu (1999:87) akimnukuu
Lass(1984) anaeleza kuwa ukakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu
zisizo za kaa kaa gumu zinapobadilika na kuwa fonimu za kaa kaa gumu. Katika
lugha ya kiswahili fonimu za kaa kaa gumu ni mbili tu yaani /ɟ/ / na /ʦ/.
Kanuni yake ni, /k/→[tʃ]/―/i/+I≠/i/. Sauti /k/ hubadilika na kuwa [tʃ] katika
mazingura ya kufuatiwa na irabu /i/ na irabu isiyofanananayo.
Data (e) salamu, umbo lake la ndani ni /salam/. Mchakato
uliojitokeza katika data hii ni uchopekaji, mchakato huu huusisha kuongeza
sauti mahali ambapo haikuwepo. Katika kiswahili mchakato huu si dhahiri sana
japo hutokea katika maneno ambayo yamekopwa toka lugha nyingine na kuongezwa
sauti wakati wa usanifishaji wake. Kanuni inayojitokeza katika data hii ni,
[Ө]→/I/ /k―≠, sauti kapa [Ө] inabadilika na kuwa irabu katika mazingira ya
kufuatiwa na konsonati halisi.
Data (f) mvua na (g)
mvivu, ambapo maumbo yake ya ndani ni /n+vua/ na /n+vivu/,
mchakato unaojitokeza katika data hizi mbili ni usilimisho pamwe wa nadhali.
Kwa mujibu wa Mgullu (1999:92) anasema tuite fonimu jumuishi /N/ ambayo
hujidhihirisha kwa sura kwa sura
mbalimbali za nazali kutegemea na usilimisho ambao fonimu jumuishi hiyo hupata.
Pia kwa mujibu wa Besha (1994:45) anasema usilimisho huu ni mnyumbuo unaohusu
kuathiriwa kwa sauti zinazofuatana, lakini kwa sharti kwamba sauti hizo ni sehemu
za vipashio tofauti vya kisarufi. Kwa ujuusilimisho pamwe wa nazali ni ile hali
ambayo nazali hufuata mahali pa matamshi
pa konsonati inayofuatia. Hivyo kutokana na data (g) mvivu yenye umbo la ndani
/n+vivu/ kanuni ya hujitokezaji wake ni, /n/→[ᶬ
]/―/v/. Nazali /n/ inabadilika na kuwa [ ᶬ] katika mazingira ya kufuatiwa
na konsonati halisi /v/. Pia katika data (f) mvua, yenye umbo lake la ndani ni
/n+vua/ kanuni ya hujitokezaji wake ni /n/→[ᶬ]/―/v/. Hivyo nazali /n/
imebadilika na kuwa [ᶬ] katika mazingira
ya kufuatiwa na konsonati halisi.
Kwa ujumla kanuni na michakato hii ya kifonolojia imekuwa na
umuhimu mkubwa katika uundaji wa maneno ya lugha malimbali pia kwa kuzingatia
kanuni na michakato hiyo katika maneno ya lugha ya kiswahili pia kuna vighairi
vyake kwani kuna baadhi ya maneno ambayo hughairi kanuni hizo.
MAREJEREO
Besha, R.M. (1984). Utangulizi wa lugha na isimu. Dar es salaam. Macmillan Aidan ltd.
Habwe, J na Karanja P (2004) Misingi ya sarufi ya kiswahili. Phoinex
publisher. Nairobi
Lass, R.(1984). Phonology. Cambridge university press. Cambridge
Massamba, P. B (2012) Misingi ya fonolojia. TATAKI. Dar es salaam.
Mgullu, R. S (1999) Mtaala wa isimu, fonetiki na fonolojia ya lugha ya kiwsahili.
Longman publisher. Nairobi.
TUKI (1990)
Kamusi sanifu ya isimu ya lugha. Chuo kikuu cha Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com