Flower
Flower

Thursday, January 9, 2020

Nyimbo ya kabila la wakinga ikionyesha jinsi mwanamke anavyosawiriwa kwenye jamii


Nkwera (1978) amefasili nyimbo kuwa ni maneno yananayotamkwa kwa sauti ya muziki. Anafafanua maaana ya muziki kuwa ni mpangilio wa sauti za ala na uimbaji unaoleta athari fulani kwa binadamu kupitia hisi zake na akili zake. Nkwera (keshatajwa) katika fasili yake anasisitiza kuwa nyimbo ni lazima iwe katika sauti za kimuziki ambazo huhusisha sauti za ala.

Njogu na Chimerah (1999) wameeleza kuwa nyimbo zinatokana na ushairi ambao ndio utanzu wa fasihi ulio mkongwe. Ambazo zilianza na hisi za matukio yaliyowakuta watu katika miktadha na mandhari ya maisha yao ya maisha ya raha na furaha, ugumu, kujituma, machungu na ushujaa. Wanafafanua kwa kusema kwamba katika jamii za kiulimwengu nyimbo zilianza pale ambapo binadamu alipobuni lugha, jambo ambalo lilimtoa mtu katika hali ya uhayawani na kuwa kiumbe razini. Hali hii ilimfanya mtu ayaelewe mazingira yake na aweze kutoa mchango wake katika kuyakabili na kuyabadili mazingira hayo.

Wamitila (2003) anaeleza kuwa nyimbo zina mahadhi ya sauti inayopanda na kushuka. Tungo hizi huundwa kwa lugha ya mkato, matumizi ya picha na mapigo ya silabi ambayo hupangwa kwa utaratibu au muwala wenye mapigo ya kimuziki au wizani. Ingawa kanuni ya ala si lazima katika kuainisha nyimbo, inawezekana wimbo ukaambatana na ala, kwa mfano chapuo, vugo, ngoma, marimba, pembe na zumari.

Hamad (2008) anasema nyimbo ni sanaa ya lugha   ya maneno yanayeleza hisia na fikra huwa teule yaliyo finyangwa finyangwa na kusukwa kwa nidhamu na mvuto unaopendezesha muimbaji na kumvutia msikilizaji. Hamad (keshatajwa) katika fasili yake anaeleza kuwa wimbo au nyimbo ni lazima ufinyangwe kwa nidhamu ambayo humvutia na kumpendezesha muimbaji na msikilizji wa kazi husika.

Kwa ujumla nyimbo ni tungo zenye mahadhi ya sauti inayopanda na kushuka. Tungo hizi huundwa kwa lugha ya mkato, matumizi ya picha. Nyimbo zinzdhaima mbalimbali kama vile kuburudisha, kuarifu, kuomboleza kubembeleza mtoto na kuhamasisha watu kufanya jambo fulani.
Ufuatao ni wimbo wa kabila la wakinga pamoja na maana yake na kuelezea ni jinsi gani au kivipi mhusika mwanamke amesawiriwa katika wimbo unaoitwa Ndisaga unaomaanisha Nawaza ulioimbwa na kundi la Sumasesu Theatre Art Group.
Ndisaga
Hioko dada ndesue ekelonga eke,
                                                                            Ndilela ndilela ndejinyo,
                                                                           Ndejinyo ndisaga ndilemwa.
      Avana avadebe vikenda navadedajavo
[ndilela ndilela]
            Navivona hata nasisoni pamiho patwevanu
                                                                           Avamama vasambwikhe,
                                                                           Vikenda navaswambavo,
      Navivona nasisoni pamiho pa kelonga.
[ndejinyo ndilela ndilela]
   Avana avadebe vikenda navadedajavo
[ndejinyo ndisaka ndilemwa]
   Navivona hata nasisoni pamiho patwevanu
                                                                      Avamama vasambwikhe,
                                                                      Vikenda navaswambavo,
                                                                      Navivona nasisoni pamiho pa kelonga.
                                                                      Ndejinyo ndisaga ndilemwa

                                                                         Avana naje syole navinokwa,
Vivomba ovopanga navokalakala mwe
                                                                        Avana naje syole navinokwa,
                                                                        Vivomba ovopannga navokalakala mwe
                                                                        Avana naje syole navinokwa,
                                                                        Vivomba ovopannga navokalakala mwe       
                                                                        Avana naje syole navinokwa,
                                                                       Vivomba ovopanga navokalakala

                                                                      Ndejinyo ndilela ndilela
                                                                      Ndejinyo ndilela ndilela
                                                                     Ndejimyo ndisaga ndilemwa
                                                                     Ndejinyo ndisaga ndilemwa
                                                                    Ndejinyo ndisaga ndilemwa
    [Onye vakilale, mupolekagke avanu vamalaja.
Ovomalaja ovomaja mwe”]

                                                                    Avana vahenza vivomba ovomalaja.
           Esyole navikwemba vasamilwe okota kole votamu
          [mupoleka isyondisova lakini esyole namunokwa
                      Mulenda mukhinakhina, jomwiswa mwisila mupolekha?
Hioko dada tosue tosilile]
                                                                    Avana vahenza vivomba ovomalaja.
           Esyole navikwemba vasamilwe okota kole votamu

Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo

Ndejinyo ndilela ndilela
Ndejinyo ndilela ndilela
Ndejinyo ndilela ndilela

Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo
Omwana ivosavosa masomo

  Avababa ovomalaja vokakile
Vikenda navahenza vadebe
Avababa ovomalaja vokakile
Vikenda navahenza vadebe

  Avamama ovomalaja vokakile
Vikenda navademi vadebe.
Avamama ovomalaja vokakile
Vikenda navademi vadebe.
Lweli ologano losilile
Lweli ologano losilile

Ndejinyo ndilela one ndilela
Ndejinyo ndilela one ndilela
Ndejinyo ndilela one ndilela
   Ndejinyo ndisaga one ndilemwa
Ndejinyo ndisaga one ndilemwa

Ndilela ndilela ndilela ndilee
            Avana avadebe vikenda navadedajavo
             Navivona nasi soni pamiho patwevanu
                              Avamama vasambwikhe vikenda navaswambavo.
            Navivona nasisoni pamiho pa kelonga

Ndejinyo ndisaga one ndilemwa
Ndejinyo ndisaga one ndilemwa
                           [leno mulopekagke isyo visova ove kilale opolikhe
                                 oveokomoleka sana ove. Ila avenge hava, o Roby, roby
                                           Najomwene ipoleka lakini pwale ojonge ojo inyake nda veni
                                                                  Nipolekha omwana ojo. Mupolekhaghe avana Kilale opolike, otesake ejo]

    Avana vahenza vivomba vovomalaja
                       Najesyole navikwemba vasamilwe khole votamu

                                     [hapo po ndikhovakolela no n`dala khela munu non`dala
                                            vamwene mupolikhe ove Kr on`dala vako jiva ve mama Glad
Opolike eeeeh
                               O Robert namwene on`dala vamwene ve mama Eva
                                     Pwale n`demi ojonge lonya lohala elitawa lya mwene
                            Liwanana nelitawa lya mutukha. Vita Bj nyiki?
Sova ove Kr, sova ove Kilale
                                                        Bjzee, eeeh lelyo ojo namwene inya lohala okendakge volevole.
          Najove Farida esavoti jakho nonu.
           Olotakhe najo volevole welolelakhe
Ovomalaja ndebelile haya








TAFSIRI YA WIMBO.
Nawaza
             MUNGU wangu tumekwisha dunia hii
Mwenzenu nawaza sipati jibu
Mwenzenu nawaza sipati jibu.
Mwenzenu nawaza sipati jibu
Mwenzenu nawaza sipati jibu.
Mwenzenu nawaza sipati jibu
Mwenzenu nawaza sipati jibu.


Watoto wadogo wanafanya mapenzi na baba zao
[Nalia nalia]
Hawaoni hata aibu mbele za macho ya watu.
Mama zetu nao wamechanganyikiwa wanafanya mapenzi
na vijana wao,
Hawaoni hata aibu mbele ya uso wa dunia
Watoto wadogo wanafanya mapenzi na baba zao
[nawaza sipati jibu]
Hawaoni aibu mbele za macho ya watu
Mama zetu nao wamechanganyikiwa wanafanya mapenzi
na vijana wao,
Hawaoni hata aibu mbele ya uso wa dunia

Mwenzenu nawaza sipati jibu.
Watoto hata shule hawataki.
Ni watukutu na waongo.
Watoto hata shule hawataki.
Ni watukutu na waongo.
Watoto hata shule hawataki.
Ni watukutu na waongo.

Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nawaza jibu sipati.
[enyi akina Kilale sikilizeni watu ni Malaya, umalaua
umalaya jamani]

wasichana wanafanya umalaya
Shule hawataki wamesahau kuna ugonjwa (Ukimwi)
[mnasikia ninachosema lakini shule hamtaki
Mnasinda mnacheza cheza, mtakufa mtakwisha mmesikia?
Mungu wangu Tumekwisha]
wasichana wanafanya umalaya
Shule hawataki wamesahau kuna ugonjwa (Ukimwi)

Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo

Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nalia nalia

Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo
Mtoto anapuuza masomo

Wababa umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na mabinti wadogo
Wababa umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na mabinti wadogo

wamama umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na wavulana wadogo
wamama umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na wavulana wadogo.
Kweli upendo umekwisha
Kweli upendo umekwisha.

Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nalia nalia
Mwenzenu nawaza jibu sipati
Mwenzenu nawaza jibu sipati
Mwenzenu nawaza jibu sipati
Mwenzenu nawaza jibu sipati

{nalia nalia}
Watoto wadogo wanafanya mapenzi na Baba zao
Hawaoni hata aibu mbele ya macho ya watu
Wamama nao wamechanganyikiwa wanafanya
mapenzi na vijana wao
Hawaoni hata aibu mbele ya uso wa dunia
Watoto wadogo wanafanya mapenzi na Baba zao
Hawaoni hata aibu mbele ya macho ya watu
Wamama nao wamechanganyikiwa wanafanya
mapenzi na vijana wao
Hawaoni hata aibu mbele ya uso wa dunia

Mwenzenu nawaza jibu sipati
Mwenzenu nawaza jibu sipati
[sasa sikilizeni ninachoongea mnasikia
we Kilale unasikia lakini wewe unasikia sana.
Ila hawa wengine hawa, Roby roby nae anasikia,
ila huyu mwingine hasikii huyu sijui ni nani hasikii huyu
msikiage mmesikia watoto sikieni Kilale
Umesikia sema ndiyo, eeeh
Hapo nitawaolea wake kila mmoja na mke wake
mmesikia eeeh!
Wewe Kr mke wako atakua mama Glad
Umesikia eeeh,
Na Robert nae mke wake atakuwa mama Eva
Yupo huyu mvulana huyu anaakili jina linafanana na jina la gari.
Anaitwa Bj nani? Sema wewe Kr, sema wewe Kilale
Bjzeee. Eeeh hilo hilo nae anaakili endelea hivyohivyo.
Nawewe Farida sauti yako nzuri endelea hivyohivyo,
ujiangalie nyie wote umalaya nimekataa, mmesikia haya.]
Kutokana na wimbo tajwa hapo juu mwanamke amesawiriwa katika mitazamo tofautitofauti kwa kupitia wimbo tajwa. Ifuatayo ni mitazamo mbalimmbali ambayo mwanamke amejadiliwa au jinsi mwanamke alivyo chorwa kwa kupita wimbo wa Ndisaga ambao maana yake ni Nawaza.
Mosi mwanamke amesawiriwa kuwa amekosa maadili, Mastin (2008) anasema kuwa katika jamii kuna miongozo ambayo huiongoza jamii kuhusu lipi la kufanya na lipi si la kufanya. Anaendelea kusema mwenendo wa mtu katika jamii ni lazima ufuate yale mambo yanayokubalika katika jamii, na yale ambayo hayakubaliki ni vema yasifanywe. Hivyo mambo haya yakifanywa huonekana kuwa ni ukosefu wa maadili ya jamii inayohusika. Mathalani katika jamii ya wakinga hali ya wanawake kujihusisha katika mapenzi na vijana wao au watoto waliowazaa ni ukosefu wa maadili na wanawake ambao wanajihusisha na suala hii huonekana kuwa hawana upendo wa dhati kwa watoto wao. Hali hii inajidhihirisha pale ambapo waimbaji wanapoimba kama ifuatavyo;
                                                                          wamama umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na wavulana wadogo
wamama umalaya umezidi wanafanya mapenzi
na wavulana wadogo.
Kweli upendo umekwisha.
Hivyo basi katika wimbo huu waimbajimwanathibitisha ni kwa jinsi gani wanawake wameonekana kutokuwa na maadili kwani hata katika jamii nyingine zinazotuzunguka suala la mama au mwanamke kujihusisha na mapenzi na vijana wadogo halikubaliki.
Pili mwanamke amesawiriwa kuwa ni chombo cha starehe, Mulokozi (1982) anaeleza kuwa ushairi wa Kiswahili uliathiriwa na mfumo wa Kimwinyi, mfumo ambao ulithamini sana anasa, mapambo na kumchukulia mwanamke kama chombo au kitu cha kuondosha hamu ya mwanaume ya kimapenzi. Kutokana na hali hii ya wanaume kuwatumia wanawake kwa ajili ya kuondoa hamu ya kimapenzi aliyonayo mwanaume, inathibitisha kuwa wanawake wamekuwa wakitumiwa kwa malengo ya kundoa hamu ya kimapenzi ambayo mwanaume anakua ameipata kwa wakati huo. Hali hii inathibishwa katika wimbo tajwa kwani wanaume wameonekana wakijihusisha na mapenzi na watoto wadogo inajitokeza pale ambapo waimbaji wanaimba kama ifuatavyo;
                                             Watoto wadogo wanafanya mapenzi na Baba zao
                                                                                             Hawaoni hata aibu mbele ya macho ya watu.
 Katika wimbo huu mwanaume anaonekana akijihusisha katika mapenzi na mtoto mdogo, kutokana na hali hii inathibitisha kuwa mwanamke amekuwa akitumiwa na mwanaume kama chombo cha starehe kwa malengo ya kuondoa hamu alizonazo za kimapenzi.  Hali hii inapelekea maamuzi ya kujihusisha na mapenzi na watoto wadogo ambao ni sawa na watoto wao.
Mwanamke amesawiriwa kama mzazi na mlezi, Balisidya (1982) anaeleza kuwa mwanamke amepewa nafasi ya umama ambapo majukumu yake ni kulea familia. Anaendelea kusema kuwa kuanzia utotoni mwanamke hulelewa akijua jukumu lake kuu ni kulea familia. Hivyo basi kutokana na hali hii ndiyo sababu mtoto wa kike akiwa mdogo hufanya majukumu mablimbali ambayo yanamuhusu mama. Vilevile katika michezo mbalimbali ambayo wanacheza hufanya hivyo, pia hata zawadi ambao hupewa na wazazi wao zinaakisi majukumu ambayo anatakiwa kuyafanya. Mwanamke anadhihilishwa kuwa ni mzazi pale ambapo waimbaji wanadai kuwa anajihusisha katika mapenzi na kijana mdogo ambaye ni sawa na mtoto wake.
                                                   Wamama nao wamechanganyikiwa wanafanya
mapenzi na vijana wao
Hawaoni hata aibu mbele ya uso wa dunia.
Hivyobasi wimbotajwa unadhihilisha kuwa mwanamke ni mzazi na mlezi, vilevile suala la uzazi linatiliwa mkazo sana kwasababu katika jamii zetu mwanamke ambaye hana uwez wa kuzaa hathaminiwi katika jamii.
Fauka ya hayo mwanamke amesawiriwa kuwa ni mali ya mwanaume, Wamitila (2002) anaeleza kuwa mwanamke ni mali ya mwanaume kwani hali hii hutokana na ndoa kwani asasi hii imejengwa kwenye imani ya uwezo mkubwa aliokuwa nao mwanaume, ambapo anaishi kwa kumwangalia mke kama chombo tu, kitu kikubwa kinachopelekea hali hii ni kutolewa mahali. Hali hii inajidhihirisha pale ambapo waimbaji wanasema kuwa watoto wa kiume watatafutiwa wake wa kuwaoa. Mwanamke anaonekana kuwa ni mali ya mwanaume pale waimbaji wanapoimba;
                                                                               Hapo nitawaolea wake kila mmoja na mke wake
mmesikia eeeh!
Wewe Kr mke wako atakua mama Glad
Umesikia eeeh,
Na Robert nae mke wake atakuwa mama Eva
Yupo huyu mvulana huyu anaakili jina linafanana na jina la gari.
Anaitwa Bj nani? Sema wewe Kr, sema wewe Kilale
Bjzeee. Eeeh hilo hilo nae anaakili endelea hivyohivyo.
Hivyobasi wanaimbaji wanathibitisha kuwa ni kweli mwanamke ni mali ya mwanaume baada ya kuolewa na mwanaume huyo hivyo mwanamke huyo anakua chini ya maamuzi ya mwa naume aliye muoa.
Vilevile mwanamke amesawiriwa kuwa hapendi elimu, Takwimu za mitandao ya jinsia (TGNP 2001) zinabainisha kuwa 25% ya wasichana huacha shule kabla ya kumaliza masomo yao kwa sababu za kuolewa, mimba, utoro, uchumi duni, mazingira mabaya ya kielimu na mila potofu. Katika usawiri huu mwanamke amesairiwa kuwa hapendi elimu, kwani ameonekana akitoroka shule na kwenda kwa wanaume ambao hali hii inathibisha kuwa mwanamke ameonekana kutokuwa tayari kupata elimu kwani amekuwa akidanganya na wanaume. Hali hii imejidhihirisha pale ambapo waimbaji wansema;
          wasichana wanafanya umalaya
                                           Shule hawataki wamesahau kuna ugonjwa (Ukimwi)
                                      [mnasikia ninachosema lakini shule hamtaki
                                                  Mnasinda mnacheza cheza, mtakufa mtakwisha mmesikia?
Mungu wangu Tumekwisha]
wasichana wanafanya umalaya
                                                                             Shule hawataki wamesahau kuna ugonjwa (Ukimwi.)
Hivyobasi wasichana wengi ambao wamekuwa wakitoroka shule na kwenda kufanya umalaya ambao mwishowake ni kupata magonjwa ambayo ni hatarishi kwa maisha yao.
Mwanamke amesawiriwa kuwa ni Malaya, katika wimbo huu mhusika mwanamke anaonekana kuwa ni Malaya kwani amekuwa akijihusisha na mapenzi na watu wazima ambao ni sawa na wazazi wao hivyo hali hii imepelekea wanawake wengi ambao wanapatikana katika jamii zinazotuzunguka kudharauliwa kwani wanajihusisha na mambo ambayo si mazuri na yanapigwa vita katika jamii. Hali hii inathibitishwa pale ambapo waimbaji wanasema;
                                                             wasichana wanafanya umalaya
Shule hawataki wamesahau kuna ugonjwa (Ukimwi).
Hivyo basi kutokana na umalaya ambao unafanywa na wanawake hawa imepelekea idadi kubwa ya wanajamii kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Kwa ujumla mhusika mwanamke ameonekana kudhalilishwa na kugandamizwa katika wimbo huu kwani mhusika huyu amesawiriwa katika upande hasi tu kwani si kweli kwamba mwanamke hana mchango chanya katika jamii hii. Hivyo basi mwanamke huyu kutetewa kwa kupitia nadharia ya ufeministi ambapo nadharia hii imejikita katika kumkomboa mwanamke katika mambo mbalimbali ambayo yanamkabili. Nadharia hii iliasisiwa na Mary Willstone Craft mnamo 1792     


MAREJELEO.( jina LA kitabu lazima liwe kwenye hati mlalo)
Balisidya, M. L. (1982). The Image of the Women in Tanzania Oral Literature. Dar es Salaam: Kiswahili Juzuu Na.49/2, TUKI.
Hamad, A. (2008), Matumizi ya Ushairi na Muziki wa Kiswahili katika Maisha ya kila Siku Pwani
                              ya Afrika ya Mashariki. Zanzibar: Bakiza.
Mastin, L. (2008). A Cultural Journey through the English Lexicon. Harvard: Havard University
                              Press.
Mulokozi, M. M. (1982). “Protest and Resistance in Swahili Poetry 1600-1885”, katika Kiswahili 45(1), 25-54.
Njogu, K. na Chimerah, R. (1999), Ufundishaji wa Fasihi Nadharia na Mbinu. Jomo Kenyatta:
                                                        Foundation Nairobi, Kenya.
Nkwera, F. V. M. (1978), Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Dae es salaam: DUP.
TGNP, (2001). Kuelekea kwenye Usawa: taswira za mwanamke Tanzania. Dar es Salaam SARDC.
Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Misingi na Vipengele Vyake.Nairobi, Phoenix Publishers.
 Wamitila, K. W.  (2003), Kamusi ya Fasihi na Nadharia. Focus Publications Ltd.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny