Flower
Flower

Sunday, January 5, 2020

LEKSIKOGRAFIA NA HISTORIA YAKE

LEKSIKOGRAFIA
Ni istilahi iliyotokana na neno la kiyunani Lexicograhos yaani Lexico – neno na Grahos  - Andika.
Ni taaluma inayohusu uandishi wa maneno kwa kuzingatia utaratibu maalumu. Baadhi ya wataalamu wanauona utaratibu huu maalumu ndio Kamusi. Kwao kamusi ni sayansi au Sanaa ya uandishi wa maneno.
Leksikolojia – tawi la isimu linalohusu uandishi wa kamusi. Ni tawi la isimu linalochunguza etimolojia, mofolojia, maana na matumizi ya maneno.
Kwa mujibu wa Dorosawiski (1962) leksikolojia ni tawi la isimu linalochunguza etimolojia, maana na matumizi ya maneno.
Leksikolojia ndio msingi au muhimili mkuu wa leksikografia. Aidha vitu vinavyohitajika katika leksikografia ndio vinavyoshughulikiwa na leksikolojia.
Kazi za leksikolojia
·         Kuchunguza sifa bainifu za maeneno
·         Kuchunguza jinsi maneno mapya yanavyoingia katika lugha.
·         Kuchunguza uhusiano wa kimaana baina ya maneno.
Leksimu – ni kipashio kidogo cha msamiati kinachoweza kusimama peke yake kama kidahizo. Leksimu si kidahizo ni kidahizo pale tu kinapokuwa kwenye kamusi.
Leksikoni – ni maneno yaliyo kwenye kamusi ambayo huwa kichwani mwa mtumia lugha. Msamiati ni jumla ya maneno katika lugha.
Vigezo vya uteuzi wa maneno katika kamusi
·         Umbo la neno
·         Maana ya neno
·         Historia ya neno
·         Matumizi ya neno


Matini zinazohusiana na kamusi ni
·         Faharasa
·         Thesaurusi
·         Saikolopidia
Uhusiano wa leksiografia na Nyanja zingine
·         Fonetiki
·         Fonolojia
·         Mofolojia
·         Semantiki
·         Etimolojia
·         Elimu mitindo
Etimolojia huchambua historia ya neno katika lugha.
Faharasa- ni orodha ya maneno yasiyo fahamika sana ambayo huwekwa mwishoni mwa kitabu au matini ili kuweza kujua maana zake kulingana na muktadha uliotumika na huwa na maneno yasiyopungua 15.
Thesaurusi- ni kitabu chenye orodha ya maneno yaliyopangwa kufuatana na dhana au uwanda wa maneno.
             Mfano. Pua ; inapatikana katikati yam domo na macho au pua ipo usoni mwa mtu.
Lengo ni kumpatia msomaji orodha ya maneno yenye maana ziazokaribiana ili kumuwezesha kuyapembua na kuyapata maneno anayotaka kuyatumia. 
Thesaurusi ya kwanza ilitungwa na Peter Mark Roget na alitumia msingi wa kimaana katika lugha.
Saiklopidia- ni kitabu chenye mkusanyiko wa Makala zinazohusu Nyanja anuai za elimu ambazo hupangwa kialfabeti na kuandikwa maelezo ya kina kwa muhutasari. Hii ni orodha ya maneno yaliyopangwa kialphabeti yakieleza sifa nyingi ya kitu hichohicho. 

Historia ya leksikografia
Kwa mujibu wa Weigand (1984) leksikografia ni kazi ya kisayansi ya kutunga kamusi. Kazi hii hujumuisha uorodheshaji wa msamiati ya lugha inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo yenye kufafanua kila neno lililoorodheshwa kadri ya mahitaji ya mtumiaji wa kamusi aliyetengwa. Hartmani aliungwa mkono na wataalamu rodewing kwa kuona kuwa wajibu wa mtunga kamusi ni kurekodi lugha na sio kutunga mtindo wake.
Hartman (1983) leksikografia ni taaluma fafanuzi inayoweka wazi taarifa za matumizi a maneno pasipo kuweka sheria. Wanalekiskografia waliandika maneno yote yanayopatikana katika lugha bila kujali utamaduni.
Weigand (1984) ufafanuzi wa kamusi ni lazima utolewe kulingana na mahitaji ya jamii na sio mtunzi.
Leksikografia ilianza pale jamii ilipokuwa ikifanya mawasiliano na jamii zingine tofauti na utamaduni wao. Kilele cha maendeleo ya leksikografia ilikuwa ni uanzishwaji wa kamusi mbalimbali. 
Aina za kamusi
Vigezo vya kuainisha kamusi
·         Kigezo cha idadi ya lugha
·         Kigezo cha ukubwa
·         Walengwa wa kamusi
·         Mda wa utunzi wa kamusi
·         Kigezo cha maudhui ya kamusi
·         Matakwa ya kamusi

·         Namna ya uhifadhi

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny