Maana ya ushairi.
Massamba (2003) akimnukuu Shaaban Robert (1968) anasema Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina na mizani, ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari.
Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, Nadharia na Tahakiki anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.
Kezilahabi, (1974) katika kitabu chake cha Kichomi anadai ushairi ni tukio, hali, au wazo, ambalo limeoneshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonesha ukweli fulani wa maisha.
Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.
Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.
Baada ya kuangalia tofauti ya ushairi ifuatayo ni tafsiri ya ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa kiswahili umeelezwa na Senkoro (1988) kuwa ni ule ushairi unaotumia lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha mawazo, fikra na vionjo vya moyo wa watu wanaotumia lugha ya Kiswahili.
Ushairi wa kiswahili umefafanuliwa tena katika mitazamo mingine miwili. Mtazamo wa Kimapokeo na mtazamo wa Kisasa.
Katika mtazamo wa Kimapokeo wanadai kuwa ushairi wa kiswahili ni ule unaotungwa kwa kufuata kanuni za urari wa vina na mizani, ambazo ni kanuni za ushairi wa Kiswahili. Miongoni mwao ni wazee na vijana wa UKUTA ( Chama cha usanifu wa Kiswahili na ushairi Tanzania) Amri Abedi.
Mtazamo wa wanausasa; Ushairi wa Kiswahili si lazima ufuate kanuni za utungaji wa mashairi. Vina na mizani si vya lazima katika ushairi. (Kezilahabi, E, Mulokozi, M.M na K. Kahigi) maelezo haya yanayofafanua maana ya ushairi wa Kiswahili yana mapungufu kadhaa kama ifuatavyo;
Wanamapokeo wameshindwa kuelezea vipengele vya maudhui. Wamejikita zaidi katika vipengele vya kifani (urari wa vina na mizani) hawajaeleza waswahili ni watu gani? Mashairi haya yanazungumzia mawazo yapi?
Wanausasa wamepinga hoja tu ya wanamapokeo kuwa ushairi wa kiswahili si lazima ufuate kanuni za urari wa vina na mizani. Hawajatoa maana yao kuhusu ushairi wa Kiswahili.
Kwa hiyo, ushairi wa Kiswahili ni utungo unaotumia lugha ya kiswahili kuelezea maisha ya waswahili (watumiaji wa lugha ya kiswahili) katika Nyanja mbalimbali za maisha, wenye kusheheni fani na maudhui yanayohusu watumiaji wa kiswahili
Ama kuhusu Muhula ni kipindi fulani katika mwaka kinachohusishwa na tukio fulani pia huzingatia kigezo cha mwaka muafaka.
Mihula ya ushairi wa kiswahili. Kwa mujibu wa Kezilahabi (1983) amebainisha Mihula ifuatayo;
Muhula wa Urasimu (hadi 1885). Katika kipindi hiki kanuni za utunzi ziliwekwa na ushairi ulitawaliwa sana na mitazamo ya kidini na Kimwinyi. Mfano; wa tungo za ushairi zilizokuwepo kipindi hiki ni utenzi wa tambuka 1728 kilichoandikwa na Bwana Mwengo, utenzi wa Hamziyyah 1690 Sayyid Abdarus , utenzi wa Al-Inkishafi utenzi uliojadili maswala ya matatizo na mazingira yaliyohusu Afrika Mashariki (1810-1820). Uliandikwa na Sayyid Abdalah A. Nassir. Makala za semina ya Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili (uk. 148-150)
Muhula wa Utasa 1885-1945. Kipindi hiki ni kipindi cha mabadiliko ya kiutawala na kielimu. Kubadilika kwa hati ya maandishi kutoka Kiarabu kwenda Kirumi. Kipindi hiki maandishi machache yaliandikwa wakat huu, mengi yakiwa maandishi ya Hemed Abdallah. Baadhi ya tenzi zilizopatikana ni Utenzi wa Vita vya Majimaji. Kanuni za uandishi wa mashairi zilianza kupotea. Makoloni ya Ulaya yalikuwa yakigawanwa Afrika (uk. 149-150)
Muhula wa Urasimi mpya (1945-1960) kipindi hiki kilikuwa ndicho kipindi cha kufufua kanuni za utunzi. Shaaban Robert, Amri Abeid Khamis Amani, M. Mnyampala, Ahmmed Nassir na wengineo. Kipindi hiki ndipo kitabu cha sheria za kutunga mashairi kiliandikwa wakati ambao kilikuwa kinahitajika sana ili kuweka kiungo kizuri na wakati uliopo. Yaani kueleweka vizuri katika wakati uliopo (1954)
Mtindo uliotumika sana ni ule wa mizani 16 yaani 8+8 kwa kila kipande cha mshororo katika mishororo minne . Mtindo uliotumika sana na Muyaka bin Haji katika karne ya 18
Wanamapokeo waliamini kuwa shairi liliandikwa ili liimbwe wakati huo mghani Radioni Athumani Khalfani alikuwa amezoea kuimba mtindo huo na katika mahadhi ya aina moja.
Muhula wa Usasa (1967-hadi leo) ni muhula wa mtazamo mpya kimawazo kisanaa, hivyo kuna mgogoro katika uwanja wa ushairi. Kipindi hiki washairi walikuwa wanatafuta uhuru wa kisanaa.
Mgogoro juu ya kanuni uandishi wa ushairi uliongezeka zaidi.
Muainisho huu wa mihula ya ushairi kwa mujibu wa Kezilahabi, unamapungufu yafuatayo yaliyobainika;
Hujahusisha usimulizi na usimulizi, inaaminiwaka kuwa asili ya ushairi wa kiswhili ni tungo simulizi hasa nyimbo zinazofungamana na ngoma. Wataalam wanaounga mkono hoja hii ni Chiraghdin (1971), Shariff (1988), Nassir (1977) na Ohly (1985).
Pia haja zungumzia ushairi kabla ya karne ya 17. Kutokana na wataalam inaonekana ushairi wa kiswahili ulianza kutungwa na kughanwa kwa ghibu/kuandikwa karne ya 10BK.
Hajabainisha wazi muhula wa Utasa uko vipi? Kwa sababu bado washairi wengi walikuwepo kutoka Tanga, Mombasa mfano; Shaabani Robert.
Kwa mujibu wa Anord, R. (1973) mtaalam huyu ameainisha mihula ya ushairi katika vipindi vitatu kama ifuatavyo;
Kipindi cha kabla ya Ukoloni: yeye alitumia mtazamo wa matabaka. Ushairi uliokuwepo ni ule ulioakisi hali ya watu, mamwinyi na ufalme. mfano; ushairi wa Mwanakupona ulisisitiza kuwatukuza mamwinyi na wafalme. Ushairi huu wa Mwanakupona uliandikwa na Bi Mwanakupona binti Mshamu.
Muhula wa Upinzani: ni kipindi ambacho upinzani ulijitokeza katika utetezi wa Uislam na mila za jadi dhidi ya Ukristo baada ya vita vya majimaji. Kipindi hiki ushairi ulipo na hadi kilipofika kipindi cha mwaka (1930). Kipindi hiki kiliwakilishwa na Shaaban Robert.
Kipindi cha baada ya Uhuru: hiki ni kipindi ambapo washairi wengi walitunga mashairi kushughulikia masuala ya ujenzi wa jamii mpya. Hii ni kutokana na mabadiliko ya fani ya ushairi. Mfano; mashairi ya Mohammed S. Khatibu ya Fungate la Uhuru na Wasakatonge yanasisitiza juu ya ujenzi wa jamii mpya.
Mapungufu ya Anord.R (1973) katika uainishaji wa mihula ya ushairi wa kiswahili;
Hajaonesha muda halisi kwani anaweka muda katika majumuisho. Mfano; anasema Kipindi kabla ya uhuru kuanzia lini hadi lini, kipindi cha upinzani ni lini hadi lini na kipindi baada ya uhuru kuanzia mwaka gani hadi mwaka gani na lini?
Hajahusisha ushairi wa kiswahili na usimulizi kama ndicho chanzo (asili) ya ushairi wa Kiswahili, kwani nyimbo zilizofungamana na ngoma.
Kwa mujibu wa Ohly,R. (1973) mtalaam huyu amegawa mihula ya ushairi katika vipindi vifuatavyo;
Kipindi cha kabla ya mwaka 1888 kwa mujibu wa Ohly; anasema kipindi hiki kilibainisha mashairi/ushairi wa aina tatu. Ushairi wa Kidini uliozungumzia masuala ya kidini. Mfano; utenzi wa Hamziyya, pamoja na ule wa Inkishafi. Ushairi wa kawaida ni ushairi ambao ulikuwa haufungamani na upande wowote isipokuwa unatoa maadili ya dunia. Ushairi wa tungo za Jadi ambazo zipo 13 baadhi ya hizi tungo za jadi ni shairi, utenzi, wimbo, ukwafi, zivindo, kimai, Hamziyya, Inkishafi au Dura mandhuma.
Kipindi cha 1888-1918; mtalaam anaeleza kuwa katika kipindi hiki kumekuwapo na ushairi wa maelezo usiofungamana na siasa. Ushairi wa kutathimini, ushairi wa kupinga ukoloni mfano; Saadan Kandoro, Amri Abeid pamoja na Shaaban Robert. Mashairi ya vikaragosi ambayo ni ya wale wenye hali ya chini/duni. Mfano; mashairi ya Shaaban Robert, mashairi ya S. A. Kandoro.
Kipindi cha 1918-1949; Ohly anasema kuwa kipindi hiki kilitawaliwa na fasihi ya ukoloni. Mikondo ya ushairi iliyokuwepo kipindi hiki ni ushairi wa maadili, ushairi wa malimwengu, na tafsiri kama aliyoifanya Nyerere J.K. (1968) katika ushairi wa kidrama wa kazi ya Shakespeare ambazo ni kazi za mabepari wa Venis. Mfano wa ubeti;
Nerissa: Naam nitampa bure bila ficha,
Poveeni na Jesika kutoka kwa myahudi,
Hati maalum ya hiba baada ya kifo chake,
Ataacha kwenu nyingi kila atakacho.
Mapungufu ya uainishaji wa Ohly (1973) yanakumbwa na changamoto zifuatazo;
a. Hajatueleza uhusiano uliopo kati ya ushairi simulizi na ushairi aliouainisha katika vipindi vyake.
b. hajaeleza baada ya muhula wa 1918-1949 mashairi yaliyoendelea mapaka leo yana maudhui gani
Baada ya kuangalia wataalam hawa katika kuainisha vipindi vya ushairi tunabaini kuwa mihula ya ushairi inaweza ikagawanywa kama ifuatavyo;
Muhula wa usahiri simulizi mpaka 1500. Muhula huu unatueleza kuwa asili ya ushairi unaonyesha kuwa ni Ngoma na nyimbo ambazo zinafungamana na ngoma. Mfano; utenzi / tungo za Fumo Liyongo.
Muhula wa Urasimu 1500-1890; kipindi hiki cha ushairi kilitambulika kwa kuwepo kwa tungo za utenzi wa Tambuka 1728, Utenzi wa Hamziyya 1644 na utenzi wa Al-Inkishafi 1820. Hiki kipindi ambacho kanuni za utunzi wa ushairi zilitumiwa kwa kiasi kikubwa. Kutokana na sababu hiyo pia kipindi hiki kilipewa jina la kipindi cha Utasa hii ni kwa mujibu wa Kezilahabi.
Muhula wa Mzinduko na Urasimi mpya 1946-1967 kutoka kipindi cha utasa ufufuo wa kanuni na mwongezeko wa kazi za ushairi zilionekana. Mfano; 1957 kitabu cha sheria za kutunga mashairi cha Amri Abeid kilichapishwa. Washairi kama vile M. M. Mlokozi na M. Mnyampala, Kandoro. S. Hivyo ikaonekana kazi za ushairi zimezinduka.
Muhula wa Mageuzi na Majaribio 1968-hadi leo. Kipindi hiki kinaonesha majaribio na migogoro mbalimbali juu ya kujadili kanuni za kutunga mashairi (ushairi). Majaribio hayo yamefanya kuzuka kwa ushairi mpya ujulikanao kama ushairi wa Mavue (masivina, huru, mlegezo) aina ya Bongo Flava, ambapo kuna uimbaji na utendaji.

No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com