ukiushi katika fasihi andishi ya kiswahili
fasili:"ukiushi" linatokana na kitenzi "kiuka" Kamusi ya Kiswahili Sanifu ( 2003) wanafasili kuwa ni:
"fanya isivyostahili au vunja sheria "
dhana hii imefasiliwa na wataalamu mbalimbali katika elimu mitindo kama ifuatavyo:
mucarovisky (1964) akifafanua dhana ya uchomozo ameeleza kuwa : Ukiushi ni hali isiyotarajiwa, isiyokuwa ya kawaida au upekee ujitokezao katika mtindo. pia Leech & short (1981) wanaeleza: ukiushi ni kwenda kinyume na kaida au kanuni za kawaida zilizokubalika katika lugha. Halikadhalika Ban peer (1986) anafafanua: ukiushi hurejelea uteuzi au matumizi ya vipashio vya lugha nje ya taratibu zilizokubalika
kwa ujumla tunaweza kueleza kuwa: ukiushi ni dhana ya kimtindo itumikayo katika usanii wa kazi za kifasihii ambayo humaanisha kuandika kazi ya kifasihi kinyume na taratibu au kanuni za kawaida zilizokubalika katika lugha inayohusika. Hapo awali utanzu wa ushairi ndio uliohusishwa zaidi na ukiushi huo wa kaida za lugha kutokana na mbinu mbalimbali za kukata maneno, kupindua maneno, kubadili miundi ya tungo katika mishororo. n.k mbinu hio katika ushiri inajulikana kama idhini ya kishairi.
Hata hivyo ukiushi huweza kufanyika katika tanzu zote za kiswahili na uandishi wa kawaida usio wa kifasihii
sifa za ukiushi katika kazi ta kifasihi
ingawa tumeeleza ukiushi ni kwenda kinyume na taratibu za lugha ila si kila kiendacho kinyume na taratibu za lugha ni ukiushi
0. ni lazima kuwe na kaida za lugha zinazokiukwa.
0. ukiushi wowote hufanyika kwa kuzingatia ruwaza.
0. ukiushi huo hufanyika ukiwa na maana au dhima maalumu.
0. ubainifu wa maana ya ukiushi hutegemeana na muktadha wa kisa husika katika kazi ya kifasihi.
chochote kijitokezacho katika kazi husika ya kifasihi huku kikiwa hakina sifa hizo hakiwezi kuitwa ukiushi bali huweza kuwa ni makosa ya kiuandishi au kiuchapaji katika kazi husika na makosa hayo hayawezi kuwa na maana yoyote ya kimtindo katika kazi hiyo
Aina za ukiushi
wataalamu mbalimbali wamebainisha aina aniwai za ukiushi Mucarovisk (1964) anaeleza kuwa ukiushi unaohusiana na kaida za kila siku za lugha hujitokeza katika viwango vitatu
0. kiwango cha kifonetiki
0. kimsamiati
0. kisemantiki
nae leech 1976 na wataalamu wengine kama wamitila 2003 waebainisha aina nyingi zaidi za ukiushi ambazo ni
0. ukiushi wakimsamiati*
0. wa kisemantiki
0. wa kifonolojia *
0. kimofolojia *
0. kisintaksia
0. kilahaja*
0. kirejesta
0. kihistoria
0. kigrafolojia
ukiushi wa kimsamiati (ordha au jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha fulani) {kimofolojia, kifonolojia, kilahaja}
ukiushi wa namna hii hufanyika kwa namna mbalimbali zikiwemo
• kuongeza viambishi katika neno
• kutumia msamiati wa lugha uneni
• kutumia msamiati mpya
• kutumia rejesta
• kutumia lahaja
badala ya maneno ya lugha husika
maneno kama hayo hutumiwa ama huzalishwa kwa malengo maalumu yaani kutoa upya fulani, kuweka msisitizo katika ujumbe au kueleza jambo fulani kimahususi mfano:
(wampaje pimdogo(umeamkaje bimdogo), hojaga, hakupatapo kuiona.
kitabu cha Nyota ya rehema na Mohamed s.m. u.k26
ukiushi huu umefanyika ili kumuonesha Sulubu kwamba ni mtu wa kutoka bara ambayo hajui kiswahili fasaha.
matumizi ya maneno ya kilahaja
mfano:
hola (ona), Yuafile (amekufa), kujishawia (kujivuna, kujishaua) kayika shairi la anguko la jibwa u.k 73. Katika diwani ya "Haza macho"mwandishi Wamitila.
mshairi ametumia ukiushi huo ili kuweka msisitizo na kuibua hisia nzito za ujumbe anaouibua katika
shairi tulilolitaja
ukiushi wa kisemantiki
ukiushi huu huhusisha matumizi ya sitiari au lugha ya picha, tashbiha n.k
katika aina hii ya ukiushi neno la kawaida linaweza kuwa na maana tofauti kabisa kutegemeana na lengo la msanii wakati mwingine ukiushi huu huhusisha matumizi ya dhana zinazoonekana kukosa mantiki katika lugha ya kawaida mfano:
Bi.kitunda: tokeni wananwake wakubwa ninyi! mmetawaliwa miili mpaka mioyo eti ninyi wanaume kweli? hata kidogo wanawake tu ninyi
( watu hawa ni wanaume lakini wanaitwa wanawake kisa waliogopa kumsaidia wakati anapingana na wakoloni wazungu) u.k. 9 tamthiliya ya kinjekitile.
ukiushi huu msanii anataka kuonesha kwamba wanaume wa kimatumbi wamekosa ujasiri ni waoga
ukiushi wa kisintaksia
unahusu kwenda kinyume na matakwa ya mpangilio stahiki wa maneno katika tungo au sentensi, matumizi na nafasi ya viunganishi katika tungo na kutoweka nafasi kati ya maneno ya sentensi. kwa mfano:
"mimi nahitaji kulipwa" alisema bubu kabiringa ngumi na kuuma meno mimi itanilipa nini jamii hii? (mfuko mtupu na hadithi nyingine U.k 4)
masahihisho:
⁃ sahihi jamii hii itanilipa nini?
⁃ matumizi ya sentensi ndefu sana
Mohammed (1995)anaeleza urefu wa sentensi huzifanya kudorora na kujikokota katika mtitimo hali hii ya udororaji wa sentensi inasawiri huzuni, wasiwasi, masahibu au jambo lolote lioneshalo bahati mbaya.
matumizi ya sentensi fupi
hutumiwa na wasanii kwa makusudio maalumu
Mohamed 1995 anasema sentensi fupi hutumika:
⁃ kujenga hisia za uchangamfu
⁃ woga au
⁃ wasiwasi
ukiushi wa kihistoria
aina hii ya ukiushi huhusisha matumizi ya maneno ya zamani ambayo hayatumiki tena katika lugha itumikayo sasa mfano maneno ya kiswahili cha zamani:
⁃ shone/mashone
⁃ ashakumsi matusi -mahali
ukiushi wa kigrafolojia
grafolojia ni taaluma ihusuyo uandishi na mpangilio wa maandishi ukiushi huu hufanyika pale msanii anapokiuka kaida stahiki za kiuandishi mfano kuandika maneno bila kuzingatia mipaka, hati ya mistari au kupanga mistari tofauti na namna ilivyozoeleka katika uandishi wa kawaida
dhima za ukiushi katika kazi ya fasihi
• kuvuta umakini.
• kushtua.
• kuibua hisia za msomaji.
• kuwezesha hadhira kubaini maudhui kwa haraka na urahisi.
• kuweka msisitizo au uzito katika maudhui yanayowasilishwa.
• kubainisha mtindo wa mwandishi wa kazi husika.
• huakisi mandhari au utokeaji wa tukio.
• kujenga ujumi(mvuto) wa kazi ya fasihi.
• kuonesha mazingira ya asili ya mtumiaji wa lugha.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com