Wamitila (2002) anafasili riwaya ni kisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa na kupimwa kwa mapana na marefu kifani na kimaudhui.
Kwa ujumla, riwaya ni masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au ploti inayofungamana na wakati au kusawili wakati na yenye visa vingi vinavyotendeka katika wakati fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa visa na wahusika.
Katika uchambuzi wa riwaya ya Adili na Nduguze tutaeleza kwa ufupi sana historia ya kazi hii kama ifuatavyo:-
Riwaya ya Adili na Nduguze ni riwaya iliyotungwa na Shaaban Robert mwaka 1952. Riwaya hii ilitungwa kwa lengo la kushughulikia masuala mbalimbali ya mienendo na tabia za watu. Katika riwaya hii mwandishi anaonyesha jinsi ambavyo katika maisha, wema huweza kushinda ubaya. Mwandishi ameonesha wema au mambo ambayo yalifanywa na watu mbalimbali kama vile, Adili alimuokoa Huria kipindi Hunde anataka kumuua, vivyo hivyo naye Huria baadaye akamuokoa Adili kipindi ametoswa baharini na ndugu zake.
Baada ya kuangalia historia kwa ufupi sana juu ya riwaya hii, tutajikita katika uchambuzi wa vipengele vya fani na maudhui kama ifuatavyo;
Vipengele vya Maudhui
Ntarangwi (2004) anaeleza kuwa maudhui ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi ya kifasihi. Maudhui yana vipengele vyake kama ifuatavyo:-
Dhamira
Wamitila (2002) anaeleza kuwa dhamira ni ile jumla ya maana anayoivumbua mwandishi aandikapo, na jumla ya maana anayoitambua msomaji katika usomaji wake. Dhamira zimegawanyika katika sehemu kuu mbili yaani dhamira kuu na dhamira ndogondogo. Katika riwaya hii kuna dhamira kuu ambayo ni ujenzi wa jamii mpya. Baada ya kupata dhamira kuu, zifuatazo ni dhamira nyingine ndogondogo zinazopatikana katika riwaya hii, ambazo ni kama;
Suala la mapenzi
Katika riwaya ya Adili na Nduguze kuna suala la mapenzi ambapo kuna mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Katika riwaya hii mapenzi ya dhati yamejidhihirisha kwa sehemu kubwa, mfano Adili alikuwa na mapenzi ya dhati kwa ndugu zake japo walimsaliti na kumtenga kama asemavyo mwandishi.. (uk 12)
“Adili alikuwa tayari siku zote kugawana na mtu
yeyote tonge la chakula lililokuwa mikononi mwake”
Hivyo, katika riwaya hii ni dhahiri kuwa suala la mapenzi linajidhihirisha. Vilevile kuna mapenzi ya uongo au usaliti kwa Hasidi na Mwivu kwa Adili.
Suala la kuabudu mizimu/ imani potofu
Katika riwaya hii, masuala ya kiimani yamejitokeza sana, hii inatokana na ukweli kuwa kila mtu anaamini katika kile ambacho huwa anaona ni kitu cha ukweli. Kwa mfano, Mfalme Mtukufu na Malkia wa Enzi hawa waliishi katika mji wa mawe na waliabudu mizimu pasipo kuamini uwepo wa Mungu bali wao waliabudu mizimu. Mwandishi anathibitisha hili kama asemavyo:-
“Walakini, juu ya sifa hizo, Malkia,
Mfalme na raia walikuwa waabudu mizimu.
Mizimu yao ilikuwa miti……(uk 27)
Hivyo, katika upande wa maudhui suala la imani potofu limejadiliwa kwa sehemu kutokana na umuhimu wake katika maisha halisi ya wanajamii.
Suala la matabaka
TUKI (2004) wanaeleza kuwa matabaka ni kundi la watu wenye hali moja linalotokana na jamii yenye mfumo wa kiuchumi ambao hugawa watu. Katika riwaya hii, suala la matabaka limejitokeza kwani kuna pande mbalimbali ambazo zinakinzana juu ya vitu fulani. Suala hili linajidhihirisha kama asemavyo mwandishi:-
Rai, Mfalme wa Ughaibu, alikuwa
mfamle wa namna yap eke yake duniani
“….kutawala suluhu na mapenzi wa wanadamu,
Utunzaji wa wanyama, na utii juu ya viumbe
Wasioonekana kama majini hutaka uwezo mkubwa sana.
Hivyo, katika riwaya ya Adili na Nduguze suala la matabaka lipo kutokana na uwepo wa pande mbili ambazo zinazofautiana kiuchumi na kiuongozi.
Suala la uongozi
Huu ni uwezo, mamlaka au karama ya kuwaonyeshwa watu njia kwa vitendo. Katika riwaya hii, suala la uongozi limejitokeza kwa marefu na mapana na hususani uongozi mzuri. Mfalme Rai alikuwa ni kiongozi bora katika jamii yake kwani aliwaunganisha watu na kuwashawishi kufanya kazi bila kulazimishwa. Haya yanathibitishwa na mwandishi kama asemavyo:-
Hakulazimisha mtu yeyote kutenda tendo fulani,
Lakini alishawishi kila moyo wa mtu kuiga aliyotenda,
Kwa hiari yake mwenyewe,
Alikuwa na mvuto mkubwa juu ya mioyo wa watu….(uk 2)
Hivyo, katika riwaya hii mwandishi anaonyesha namna ambavyo uongozi wa mfalme Rai ulivyotukuka na kila mmoja mmoja aliweza kufurahia na kuipenda nchi aliyokuwa anaiongoza.
Migogoro
Kwa mujibu wa TUKI (2004) wanaeleza kuwa migogoro ni hali ya kutofautiana baina ya pande mbili au zaidi ambayo inaweza kuwa baina ya mtu na mtu, familia na familia au nchi na nchi nyingine. Katika riwaya hii ya Adili na Nduguze, migogoro ya aina mbalimbali imeweza kujitokeza ambayo ni kama ifuatavyo:-
~ Mgogoro kati ya Adili na Ndugu zake. Huu umetoakana na mgawanyo wa mali, ambapo waligawana mali sawa lakini baadaye ndugu zake Adili wakatumia vibaya na kusababisha mgogoro baina yao. Pia, kuna mgogoro wa Adili na Ndugu zake kumtosa baharini ili waweze kumuoa mpenzi wake.
~ Mgogoro wa Hunde na Huria. Huu unasabishwa na jini Hunde ambaye anamtaka Huria kimahusiano aliyekuwa mtoto wa mfalme. Utatuzi wake ni Hunde kushitakiwa na kisheria.
~ Mgogoro kati ya Mrefu na Tukufu. Huu unasababishwa na Mrefu ambaye alichukua jukumu la kumshauri Tukufu kuachana na kuabudu mizimu ili aanze kumtumikia Mungu wa kweli lakini Tukufu akagoma na kusema kuwa Mrefu asipofuata masuala ya kijadi hatafanikiwa. Kuna migogoro mingine mingi kama vile, mgogogro wa Ndugu zake Adili na mpenzi wake Adili.
Ujumbe
Madumulla (2009) anaeleza kuwa ujumbe ni kitu ambacho mwandishi hudhamiria kumtumia msomaji. Kila kazi ya fasihi hubeba ujumbe wake ambao mwandishi hutaka umfikie msomaji wake husika. Katika riwaya hii kuna ujumbe mbalimbali uliyoweza kujitokeza japo tutaonyesha kwa ufupi kama ifuatavyo:-
~ Suala la matabaka katika jamii yoyote ile halikwepeki japo ni muhimu kulipiga vita.
~ Masuala ya imani potofu yanarudisha nyuma ujenzi wa jamii mpya.
~ Uongozi mzuri ni chanzo cha ujenzi wa jamii endelevu.
~ Mapenzi ya kweli katika jamii ni muhimu na husaidia katika kudumisha umoja na mshikamano.
Falsafa ya mwandishi
Msokile (1992) anaeleza kuwa falsafa ni wazo au funzo ambalo mtu huamini kuwa ukweli fulani unaohusu maisha yake pamoja na maisha ya jamii nzima. Katika riwaya hii mwandishi anaamini kuwa suala la uongozi mzuri ni chanzo cha ujenzi wa jamii mpya.
Vipengele vya Fani
Senkoro (2011) anaelezea kuwa fani ni ule ufundi wa kisanaa anaotumia msanii katika kazi yake. Katika kipengele hiki cha fani kimegawanyika katika vipengele vidogo vidogo ndani yake kama ifuatavyo:-
Muundo
Senkoro (keshatajwa) anafasili muundo kuwa ni namna matukio katika kazi ya fasihi yalivyopangwa na kuleta mtiririko wa kazi husika ya fasihi. Katika riwaya hii miundo mbalimbali imetumika kama vile, muundo wa rejea kwani msanii anaanza kwa kusimulia jinsi Adili anavyofanya mambo ya kikatili kwa manyani.
Mtindo
Senkoro (keshatajwa) anaeleza kuwa mtindo ni ule upekee wa uundaji wa kazi ya fasihi na hutofautiana baina ya msanii mmoja na mwingine kulingana na hisia za msanii huyo. Katika riwaya hii, msanii ametumia mtindo kama kipengele kingine cha kifani. Msanii wa kazi hii ametumia mtindo wa masimulizi katika kazi yake kwa kuelezea visa na matukio ya akina Adili na Nduguze; Huria, Hunde na hata visa vya Hasidi na Mwivu. Vilevile, mtindo wa nyimbo umetumika kama asemavyo mwandishi ukurasa wa (42)
Nala sumu ndugu zangu,
Msambe naona tamu,
Takalifu kubwa kwangu,
Tuadhibu yangu damu,
Sina raha ndugu zangu,
Neno hili kwangu gumu
Pia, msanii ametumia mtindo wa barua katika kazi yake ili kuzitofautisha na kazi zingine kama asemavyo mwandishi (Uk. 44) ambapo Mfalme Rai alijaribu kuyaombea manyani msamaha kwa Adili:-
Mawe huwa dhahabu,
Au joha na chuma,
Na mtu anapotubu
Dhambi yake kukoma
Nishani zake thawabu
Na heshima ya daima
Hivyo, katika riwaya ya Adili na Nduguze mwandishi ametumia mitindo kwa namna mbalimbali katika uandaaji wa kazi yake. Kazi hii imekuwa ya kipekee sana tofauti na kazi zingine kulingana na mwandishi kutumia mitindo tofauti inayomtofautisha na wasanii wengine.
Mandhari
Wamitila (2002) anafasili mandhari kuwa ni mahala ama wakati tukio la kifasihi lilivyobuniwa na kutendeka na msanii, na hufanikiwa kujenga hisia ya msomaji au msikilizaji ama mtazamaji kulingana na kazi yake ya fasihi aliyoiandaa. Katika kazi hii mwandishi ametumia mandhari ya ughaibuni kwa kutuonyesha mazingira ya kufikirika, kwani haipatikani katika mazingira ya kiuhalisia. Mandhari yaliyotumika ni kama vile; ughaibuni, mji wa mawe, nyumbani kwa Mfalme, baharini na dukani.
Wahusika
Ntarangwi (2004) anaelezea kuwa wahusika ni viumbe hai au visivyo hai ambavyo vinawakilisha watendaji halisi katika maisha ya kila siku ya jamii husika katika kuonyesha wasifu wa ndani na nje. Kama vile; hali ya kusononeka mhusika, furaha au tabia fulani katika jamii inayotuzunguka.
Katika riwaya hii, mwandishi ameunda majina ya wahusika kulingana na matendo na tabia zao zilivyo. Kuna wahusika ambao waliweza kubadilika na ambao tabia zao hazikubadilika. Ametumia wahusika wengi kama vile; Adili, Hasidi na Mwivu, Mfalme Rai, Ikibali, Mwelekevu, Mfalme tukufu na Malkia Enzi, mfalme kisasi, Huria, Hunde na wengine kama Manyani na Majini.
Matumizi ya Lugha
Huu ni ustadi wa msanii katika kutumia lugha itakayoleta mvuto kwa wasomaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi. Mwandishi wa riwaya hii ametumia lugha ambayo kwa kiasi inaeleweka na wasomaji wake ambayo imejaa misemo, nahau, methali, vitendawili na hata baadhi ya sehemu ametumia tamathali za semi ili kuipamba kazi yake na kuonyesha ustadi wa kuimudu lugha yake anayoitumia katika kuandikia kazi.
Matumizi ya methali
Huu ni usemi wa kisanii na kimapokeo unaofikiriwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumiwa kufumbia au kupigia mfano na huwa unabeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. Kuna baadhi ya methali zimejitokeza katika riwaya hii, ambazo kama zifuatazo:-
Mali bila daftari hupotea bila habari……(uk 12)
Mtu huchuma juani na akala kivulini…..(uk 14)
b) Matumizi ya nahau na misemo
kwa mujibu wa Mwansoko (1994) anaeleza kuwa misemo ni maneno yanayotumiwa na makundi maalumu ya watu katika jamii yaliyojitenga kwa kufuatana na mambo yanayopendelea nafasi yao katika jamii. Katika riwaya hii kuna misemo mingi iliyotumika kama ifuatavyo:-
Damu nzito kuliko maji…..(uk 40)
Busara kubwa kichwani haina faida kama moyoni hamna chembe ya wema(uk 10)
Mwenye subira hukidhiwa haja zake (Uk. 45)
c) Matumizi ya Tamathali za Semi
Msokile (1992) anaeleza kuwa tamathali za semi ni fungu la maneno lililogeuzwa maana yake kamili ili kuwakilisha maana nyingine. Katika riwaya hii, mwandishi ameweza kutumia tamathali nyingi ambazo ni kama ifuatavyo:-
Tashititi
Hii ni tamathali ambayo vitu visivyo na sifa za uhai walizonazo watu hupewa sifa hizo za kuwa hai. Tashititi inaweza kuwa kisu, jiwe, mlima ambapo hupewa sifa ya kutenda kama binadamu. Katika riwaya ya Adili na Nduguze kuna tashititi kama zifuatazo:-
~ Mimea hii ilieneza neema ya vyakula kwa watu na malisho ya wanyama…..(uk 3)
~ Atasema kweli, na manyani yatakuwa mashahidi…..(uk 9)
Tashibiha
Hii ni tamathali ya semi ambayo hufanya kazi ya kulinganisha vitu viwili visivyo na hadhi sawa kwa kutumia viunganishi. Riwaya hii imetumia baadhi ya tashibiha katika kufanikisha ujumbe kufika kwa jamii husika kama vile:-
Tabia yake ijigawa katika theluthi tatu mbalimbali kama rangi ya ngozi ya pundamiliya (Uk. 1)
Alitoshwa baharini kama kitu kilihokuwa hakifai….(uk 3)
Moyo wake ulifumwa na msiba akalia kama mtoto mdogo…(uk 41)
Mjalizo
Hii ni tamathali ya semi ambayo msanii / mwandishi huitumia kutaja vitu au mambo yaliyo katika orodha bila kutumia viunganishi. Tamathali hii imetumika kama;
Sebule hiyo ilikuwa imesakifiwa kwa marmar za rangi tatu, yaani, nyeupe, nyekundu na samawati (Uk. 5)
iv)Tashihisi
ni tamathali ambayo vitu visivyo na sifa walizonazo watu hupewa sifa hizo. Mfano wa tashihisi ni kama; jiwe, mti na hata kichaka kupewa sifa ya kutenda kama binadamu afanyavyo.
Mimea hii ilieneza neema ya vyakula kwa watu na malisho ya wanyama (Uk. 3)
Tabia yake imejigawa katika theluthi tatu mbalimbali kama rangi ya ngozi ya pundamiliya (Uk. 1)
Kufaulu kwa mwandishi katika kazi ya fasihi
Mwandishi wa riwaya hii; Shaaban Robert amefaulu katika kazi yake kwa kutumia lugha ambayo inaeleweka kwa wasomaji wake, iliyojaa; misemo, nahau, methali na maneno mengi ya kilahaja ambayo yanatumika katika lugha ya Kiswahili sanifu.
MAREJELEO
Madumulla, S. J (2009). Riwaya ya Kiswahili, Nadharia, Historia na Misingi wa Uchunguzi.
Dar es Salaam: Mture Educational Publishers Limited
Msokile M (1992). Kunga za Fasihi na Lugha. Dar es Salaam: Educational Publishers
Distributers Ltd
Mwamsoko H.G (1994). Kitangulizi cha Tafsiri: Mkakati, Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam:
TUKI
Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana Collage: Rock Island, IL612.
Publishes Ltd
Senkoro, F. E. M. K (1982). Poetics. Swahili Poetry. Tanzania: Dar es Salaam Press and
Publicity
…………………….(2011). Fasihi. Dar es Salaam: KAUTTU
Shaaban, R. (2010). Adili na Nduguze. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House
TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la Pili). East Africa: Oxford Univesity Press
TUKI (2015). English- Swahili Dictionary. Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Studies
Wamitila, K. w (2002). Uhakiki wa Fasihi Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix
Publishers Ltd

No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com