Katika kujibu swali hili tunaligawa katika ehemu
kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao utakuwa na fasili na dhana ya
mofofonemiki na historia ya kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki. Sehemu ya
pili ni kiini cha swali ambapo tutaeleza sababu za kuibuka kwa nadharia ya
mofofonemiki na sababu za kushindwa kwa nadharia hii.Tukianza na utangulizi:
Dhana ya Mofofonemiki hutumika kwa maana sawa na
Mofofonolojia. Kwa mujibu wa Massamba (2012:105),anasema nadharia ya
Mofofonemiki ilipendekezwa mwanzo na Nicholaj Trubetzkoy katika mkutano mkuu wa
kwanza wa wanafilolojia wa Ki-slava ambao ulifanyika Prague mwezi Oktoba 1929.
Mofofonolojia kwa mujibu wa Trubertzkoy 1929 kama anavyonukuliwa na Massamba
(2012:105), ni tawi la simu ambalo linashughulika na matumizi ya mofolojia
katika kufafnua tofauti fulani za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezwa kwa
kutumia data za kifonetiki peke yake.
The New Oxford American Dictionary (2010) imefafanua
Mofofonolojia kuwa tawi la isimu linalojishughulisha na uwakilishi wa
kifonolojia wa mofimu. Kwa maneno mengine ni kuwa tawi hili la isimu linahusika
na kudhihirisha uhusiano wa kiutegemezi uliopo baina ya fonolojia na
mofonolojia.
Kwa ujumla, Mofofonolojia ni kiwango cha kiisimu
kinachojishughulisha na uhusiano wa kifonolojia na jinsi kinavyohusiana moja
kwa moja na mofolojia.
Nadharia ya Mofofonemiki iliibuka
kutokana na matatizo yaliyoibuka katika kuchanganua baadhi ya vipengele
vya kifonolojia ambavyo vilihitaji maelezo zaidi kuliko ya yale ya kifonolojia. Hii ndiyo sababu kubwa
iliyomshawishi Nikolaj Trubertzkoy kupendekeza kiwango cha Kimofofolojia
ambacho ni tofauti na fonolojia na mofonolojia. Mofofonolojia. Baadhi vipengele
hivyo ni pamoja na vifuatavyo;
Kuchunguza ubadilikaji wa sauti ambao una uamilifu
wa kimofolojia. Massamba (2012) anaelezea kuwa mabadiliko ya sauti yanayotokea
katika baadhi ya maneno baada ya sauti fulani kufuatiwa na kiambishi cha
unominishaji (i). Mofofonemiki imeonesha mabadiliko ya sauti ya kifonolojia na
umbo la neno kimofonolojia.
Kwa mfano; Jenga- mjenzi
Mpendi -mpenzi
Fuata -fuasi
Katika mfano huo hapo juu kinominishi (i)
kimebadili umbo la neno kutoka kitenzi kuwa nomino. Hivyo mofofonemiki
imeonesha uhusiano wa kifonolojia na mofolojia.
Kuchunguza athari za mfuatano wa sauti mbili
zinazofanana (Kudondoshwa kwa irabu). Kwa mujibu wa Mugullu (2010:90) anasema
irabu hudondoshwa zaidi zinazofanana huwa zinavutana. Hii ni kuonesha kuwa yapo
mabidiliko yannapotokea iwapo irabu mbili zinazofanana zinapokaribiana.
Kwa mfano; Wa + anafunzi – wanafunzi
Wa+alimu –
walimu
/ a / [Q]/ a
Mabadiliko haya ya kuachwa kwa irabu iliyokuwa
awali hayawezi kuzungumzwa kifonolojia pekee kwa kuwa yanaathiri umbo la neno
zima.
Kuchunguza mabadiliko yanayotokea iwapo sauti mbili
zinapoungana. Katika lugha ya Kiswahili tunaona kuwa irabu zinapoungana na
kuunda neno jipya. Yapo mabadiliko makubwa mawili tunayoyaona, kwanza ni
mvutano wa irabu, kwa mujibu wa Mgullu (1999: 89) nasema badiliko hili hutokea
pale irabu ya juu ya chini zinapoathiriana kimatamshi hasa eneo la kutamkia.
Athari ya mvutano huu ni kuundwa kwa sauti ambayo ambayo haikuwepo hapo awali
na iliyo tofauti na sauti za awali. Kwa mfano irabu ‘a’ na ‘i’ zinapovutana
hutengeneza sauti E. tukichunguza mofimu. Tunachunguza mifano
ifuatayo;Tukichunguza mifano ifuatayo;
Ma+ino – meno
Wa + ingi – wengi
Ma+iko – meko
Katika mifano hiyo hapo juu mvutano wa irabu ama
sauti /a/ na /r;/ ni kuundwa kwa neno /e/ unaleta athari katika maumbo ya
maneno husika. Hakika hili lisingeweza kuzungumziwa bila kuhusisha nadharia ya
mofofonemiki.
Badiliko la pili linalotokea ni uyeyushaji. Ambapo
kwa mujibu wa Mgullu (1999) anaeleza kuwa uyeyushaji ni mchakato wa kifonolojia
ambao unaelezea mabadiliko ya sauti
(irabu) na kuwa kiyeyusho (w na y) irabu yoyote ya juu (iwe /i/ au /u/ ikifuatana na irabu zisizofanana
nazo katika neno, irabu hiyo hubadilika na kuwa kiyeyusho. Mathalani katika
data ifuatayo inaonesha mchakato wa uyeyushaji.
U+imbo – wimbo
U+oga – woga
Fi+eka – fyeka
Katika badiliko hilo la kifonolojia tunaona
mofu/maumbo ya awali ya maneno yakiathiriwa au pengine kubadilika.
Walichunguza ubadilikaji wa sauti ambao usingeweza kuelezewa
kwa kutumia data ya kifonolojia pekee. Massamba (2012) aneleza kuwa
mofofonemiki iliweza kuonesha kipashio cha umbo kiini kama kiwakilishi cha
mofimu. Hivyo wanafonemiki walitoa mapendekezo baada ya wanamuundo kushindwa
kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi kwa kutumia kigezo cha kifonetiki pekee.
Kwa mfano; Walishindwa kujua sauti /k/ ni alofoni
ya /C/ au /C/ ni alofoni ya /k/ kwa mfano katika lugha ya
MARAJELEO
Mgullu,
R. S (1999), Maatala wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya
Kiswahili:
Longhorn
Publisher: Nairobi.
Massamba, D. P. B (2012), Misingi ya
Fonolojia. TUKI: Dar ea salaam.
Mgullu,
R. S (2010), Mtaala wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Monolojia ya Kiswahili:
Longhorn
Publisher: Nairobi.
The New Oxford American Dictionary. (2010), Oxford
University Press. New York.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com