Flower
Flower

Thursday, August 23, 2018

MAWASILIANO

Kazi hii tumeigawa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao umejikita katika kufasili dhana mbalimbali zinazojitokeza katika kazi hii. Sehemu ya pili ni kiini ambacho tumeeleza kufanana na kutofautiana baina ya aina za mawasiliano. Mwisho ni sehemu ya hitimisho la kazi.
Massamba (2009:50), anafafanua kuwa mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa kutumia njia mbalimbali za misimbo ambayo inajulikana kwa pande zote mbili. Fasili hii imeshindwa kuweka wazi hiyo misimbo inayotumika kwani imejiegemeza sana katika lugha ya ishara/vitendo na kutotilia maanani sana mawasiliano mengine.

TUKI (2012:324), wanadai kuwa mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa njia mbalimbali kama vile simu, barua na telegram. Fasili hii inaonekana kuhusisha njia mbalimbali katika mawasiliano kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwa ujumla, mawasiliano ni mchakato wa upashanaji habari kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali zinazoeleweka na watumiaji hao. Kwa mfano njia ya mazungumzo, ishara na maandishi.

Aidha, kwa mujibu wa Shannon na Weaver (1948), wameonesha mchakato wa mawasiliano; mtoa ujumbe→kisafirishaji→njia ya kusafirishia→kipokelea ujumbe →mpokeaji.
Aidha Triganda (2009), anaeleza kuwa kuna aina mbili za mawasiliano ambazo ni mawasiliano ya mdomo na mawasailiano yasiyo ya mdomo. Mawasiliano ya mdomo ni aina ya mawasiliano ambayo yanahusisha sauti katika mchakato wa kimawasiliano. Lakini mawasiliano yasiyo ya mdomo ni aina ya mawasiliano yasiyohusisha ishara na alama katika mchakato wa kimawasiliano. Triganda (keshatajwa), anaendelea kuelezea kuwa mawasiliano yasiyo ya mdomo yanaweza kufanyika pasipo kuhusisha sauti.Vilevile mawasiliano ya mdomo yanaweza kufanyika bila kuhusisha ishara.

Robert na wenzake (2003:28), wanaeleza kuwa, mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo jinsi yanavyotofautiana. Wanadai kuwa mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha tabia, saikolojia na mwingiliano wa kimazingira, kupitia uelewa wa mtu ukihusiana na mtu mwingine anayewasiliana nae. Hii ni tofauti na mawasiliano ya mdomo. Hivyo kutokana na maelezo ya wataalamu mbalimbali kuna aina mbili za mawasiliano.

Aina hizo za mawasiliano zinafanana na kutofautiana. Ufuatao ni ufanano kati ya mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo.
Mosi, aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa habari, taarifa, mawazo, hisia kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mujibu wa Kacharava (2016:103),Both involvestransmition of infotmation from one person to another. Anaeleza kuwa miongoni mwa vipengele vinavyoleta ufanano kati ya mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo ni kuwa aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa habari kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa njia tofauti tofauti kama vile njia ya maandishi, mazungumzo na barua.
Pili, mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yote yanahusisha akili. Massamba (kashatajwa), anadai kwamba mawasiliano haya huusisha akili kwa maana kwamba mawasiliano ya mdomo huusisha masikio kwa ajili yakusikia kinachosemwa kenda kutafsiriwa katika akili/ubongo.Pia huusishamacho ambayo yanapeleka mrejesho kwenye ubongo unaoenda
Nne, zote zina dhima zinazofanana. Kacharava (2016:104),anafafanua kwamba mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana dhima zinazofanana. “Both verbal and non verbal communication are the same Rule or Function such to growth and to consolidate the relationship between the society”. Mfano dhima  hizo ni kukuza au kuimarisha uhusiano miongoni mwa watu katika jamii. 

Hivyo jamii moja huendelea kuwa na uhusiano na jamii nyingine au mtu mmoja na mtu mwingine kutokana na uhusiano wao wa upashanaji habari. Upashanaji huo wa habari unaweza ukatumia ishara kama vile picha, maandishi na sauti. Pia mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yote yanasaidia kukuza utamaduni kupitia njia za upashanaji wa habari.  
Tano, mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana vitatizi vinavyofanana ambavyo vinaweza kukwamisha mchakato wa mawasiliano. Devito (2009:37), “There are several types of noise that might interfere the communication process. Such as semantic interference, psychological, physiological and physical interference.” Anaeleza aina ya vitatizi vinavyojitokeza katika mawasiliano. Kuna kitatizi cha maana mfano neno mouse hurejelea panya, na kifaa kinachotumika kwenye talakilishi. Aidha kitatizi kingine nicha saikolojia mtu anakuwa anawaza mambo mengi kwa wakati mmoja. Mfano mtu anakuwa anashindwa kuelewa kwamba hiyo ishara ina maanisha nini. Pia hata kwenye maamuzi mtu anashindwa kuwa na kumbukumbu halisi kutokana na masuala ya kisaikolojia. Tatumatatizo ya milango ya fahamu kama vile kutosikia vizuri husababisha mtu kushindwa kusikia vizuri wakati wa mazungumzo yanapofanyika. Aidha tatizo la kutoona vizuri linaweza kupelekea mtu kushindwa kuona vizuri na kupelekea mtu asiweze kuziona ishara vizuri na kupelekea mawasiliano kukwama wakati wa mazungumzo hayo.
Sita, mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanaongozwa na kanuni maalumu. Wood (2009:26), “Both Verbal Communication and non verbal communication ar controlled by regurative principles. For example traditional, in Asia home, the elder speak first while youngster listen without interruption or contradiction.” Anaeleza kuwa katika mazungumzo ya mdomo kuna kanuni inayoongoza mawasiliano. Mzungumzaji huanza kuongea kisha msikilizaji humsikiliza na baada yakusikiliza hutoa jibu. Pia katika ishara au mawasiliano yasiyo ya mdomo mmoja huanza kutoa ishara ndipo mwingine anafuata. Wood (keshatajwa), anatoa mfano kuhusu utamaduni wa watu wa bara la Asia ambapo mtu mwenye umri mkubwa huanza kuongea wakati mwenye umri mdogo anakuwa anamsikiliza bila kumkatisha mazungumzo yake. Baada yakumaliza mzungumzaji atampa nafasi msikilzaji kujibu.Hii haina tofauti sana na utamaduni wa kwetu Afrika ambapo mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo huongozwa na kanuni/kaida. Ingawa mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanafana lakini pia yanatofautiana.
Ingawa mawasiliano yam domo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanafanana lakini pia yanatofautiana. Zifuatazo ni tofauti kati ya mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo.
Mosi, mawasiliano ya mdomo yanatumika kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mawasiliano ya yasiyokuwa ya mdomo. Kwa mujibu wa Mehrabian (1983:29), “Approximately 55- 95 of communication is coontributed bynonverbal communication.” Anaeleza kwamba inakadiriwa kuwa asilimia hamsini na tano mpaka tisini na tano ya mawasiliano huchangiwa na mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo. Katika upashanaji habari mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanatumika kwa asilimia kubwa ukilinganisha na mawasiliano ya mdomoambayo  hutumika kwa kiasi kidogo.
Pili, mawasiliano ya mdomo ni rahisi ukilinganisha na mawasiliano yasiyo ya mdomo. Beardsley na wenzake (2003:29),Verbal communication are very easilycompeared to Non verbal communication. Wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyo ya mdomo ni magumu kueleweka ukilinganisha na mawasiliano ya mdomo. Beardsley na wenzake (2003:29), wanaona kwamba mawasiliano yasiyo ya mdomo ni magumu kwasababu ya matumizi ya ishara, picha na maandishi hivyo huwa ni vigumu kuvielewa pindi vinavyotumika kuwasilishia ujumbe. Wakati mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti ambayo ni rahisi kwa msikilizaji kufasiri taarifa au hisia zinazowasilishwa.
Tatu, mawasiliano yasiyo ya mdomo yanahusisha mchanganyiko wa tabia, saikolojia na mwitiko wa mwingiliano wa watu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, wakati mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti. “Non verbal communication is the mixture of behaviour, response, interaction of people from one person to anoooother person.” Beardsley na wenzake (wameshatajwa), wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha vitu vingi ikiwemo tabia, saikolojia ambavyo humsaidia kuelewa ishara, alama na maandishi, wakati ambapo mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti peke yake.
Nne, mawasiliano yasiyo ya mdomo huwa hayabadilikibadiliki wakati mawasiliano ya mdomo yanabadilika. “Non verbal communication is static unlike to vebal communication”. Boman (1969), akinukuliwa na Beardsley (2003:29), anaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo hayabadiliki badiliki. Mfano maandishi, ishara na alama huwa hazibadiliki kulingana na muktadha wa mawasiliano. Wakati mawasiliano ya mdomo yanabadilika kulingana na hali ya msemaji na hali ya msemeshwaji.
Kwa kuhitimisha, uanishaji wa aina za mawasiliano umekuwa na changamoto mbalimbali katika kuzianisha kulingana na wataalamu. Hii inatokana na vyanzo vinavyotumika. Lakini tunaona kwamba kigezo kizuri cha kutumia kuainisha aina za mawasiliano ni jinsi au namna mawasiliano yanavyotumika ambapo ndipo tulipopata aina mbili za mawasiliano.




MAREJELEO
Beardsley, A (2003). Communcation Skills in pharmacy practice. USA: Arizona State                                         University.
Devito, J. A(2009).Interpersonal Communication. Newyork: Hunter college of the City                                       University of New York.
Kacharava, K (2016). Visual and Verbal Communications. Europe: European Scientific Institute.
Massamba, D.P.B (2009). Kamusi ya Isimu na falsafa ya lugha. TUKI: Dar es salaam.
Mehrabian, A (1983). Significance of posture and position to the Communication. Psychological   
                         Bulletin.
Robert, M (2003). Signalers and Receiver in Communication. Philadelphia: University of                           Pennsylvania.
TUKI(2012).Kamusi ya Kiswahili na Kiingereza. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa                                  Kiswahili
Triganda, S. (2009).The Best of literarure Study guides for your classes. Kompasiana: The                         University of Jakarta Publishers limited.
Shannon, E. C na Weaver,W (1948). Handbook of Communication. Amazon: Atlantic Publishers Distribution.

Wood, A. T (2009).Communication in our Lives. Belmont, CA: Thomson Wadsworth.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny