Massamba
(2009:50) anafafanua kuwa mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa kutumia njia
mbalimbali za misimbo ambayo inajulikana kwa pande zote mbili. Fasili yake
imeshindwakuweka wazi fasihi yake kwani imejiegemeza sana katika lugha ya
ishara/vitendo na kutotilia maanani sana mawasiliano mengine.
TUKI
(2012) wanafafanunua kuwa mawasilianoni upashanaji wa habari kwa njia
mbalimbali kama vile simu, barua na telegram.
Kwa
hiyo mawasiliano ni mchakato wa upashanaji habari kutoka kwa mtu mmoja kwenda
kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali zinazoeleweka na watumiaji hao. Kwa mfano
njia ya mazungumzo, ishara na maandishi.
Aidha,
kwa mujibu wa Sherion na Warren (1945) wameonesha mchakato wa mawasiliano……….
Tridanda
(2009) anaeleza kuwa kuna aina mbili za mawasiliano ambazo ni mawasiliano ya
mdomo na mawasiliano ya mawasailiano yasiyo yam domo. Mawasiliano ya mdomo ni
aina ya mawasiliano ambayo yanahusisha sauti katika mchakato wa kimawasiliano.
Ilihali mawasiliano yasiyo ya mdomo ni aina ya mawasiliano yasiyohusisha ishara
na alama katika mchakato wa kimawasiliano.
Anaendelea kuelezea kuwa mawasiliano
yasiyokuwa yam domo yanaweza kufanyika pasipo na kuhusisha sauti. Vilevile,
mawasiliano ya mdomo yanaweza kufanyika bila kuhusisha ishara.
Aidha
mtaalamu Robert na wenzake (2003:28) wanaeleza kuwa, mawasiliano yam domo na
yasiyikuwa ya mdomo jinsi yanavyotofautiana; Anadai kuwa mawasiliano yasiyokuwa
ya mdomo yanahusisha mchakato wa tabia, saikolojia na mwingiliano wa
kimazingira, kupitia uelewa wa mtu ikihusiana na mtu mwingine anayewasiliana
nae. Anaendelea kuwa hii ni tofauti na mawasiliano ya mdomo. Hivyo kuna aina
mbili za mawasiliano ambazo zinafanana na kutofautiana.
Ufuatao
ni ufanano kati ya mawasiliano yaliyo ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo:
Kwanza
aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa habari, taarifa, mawazo, hisia kutoka
kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mujibu wa Kacharava na Kamerlelidza (2016:103)
wanaeleza kuwa miongoni mwa vipengele vinavyoleta ufanano kati ya mawasiliano
yam domo na yasiyo ya mdomo ni kwamba aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa
habari kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa njia tofauti tofauti
kama vile njia ya maandishi, mazungumzo na barua.
Pili
mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yote yanahusisha akili. Kwa
mujibu wa Massamba (kashatajwa) anadai kwamba mawasiliano haya huusisha akili
kwa maana kwamba mawasiliano yam domo huusisha masikio kwa ajili yakusikia
kinachosemwa kenda kutafsiriwa katika akili/ubongo. Pia huhusisha macho ambayo
yanapeleka mrejesho kwenye ubongo unaoenda kutafsiri habari inayowasilishwa.
Pia
aina zote mbili za mawasiliano zinahusisha mtoa ujumbe na mpokea ujumbe. Kwa
mujibu wa Shennan na Werren (1948) wanaeleza kwamba katika mchakato wa mawasiliano
kuna kuwa na watu ambao wanakamilisha mchakato wa mawasiliano. Tazama mchoro
ufuatao……..katika mchoro huo unaonesha kwamba katika mawasiliano ya mdomo na
yasiyo ya mdomoiliyakamilike lazima kuwe na wahusika wa namna hiyo ambao ni
mtoa ujumbe na mpokea ujumbe.
Nne,
zote zina dhima zinazofanana (kashatajwa) uk. 104 wanafafanua kwamba
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana dhima zinazofanana. Mfano dhima wa
hizo ni kukuza au kuimarisha uhusiano miongoni mwa watu katika jamii. Hivyo
jamii moja huendelea kuwa na uhusiano na jamii nyingine au mtu mmoja na mtu
mwingine kutokana na uhusiano wao wa upashanaji habari, ambapo upashanaji huo
wa habari unaweza ukatumia ishara kama ile picha, maandishi na sauti. Pia
mawasiliano hukuza utamaduni kwa mfano mawasiliano yam domo na yasiyo yam domo
yote yanasaidia kukuza utamaduni kupitia njia za upashanaji wa habari.
Mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana
vitatizi vinavyofafa, kwa mujibu wa Devito (2009:37). Anaeleza kazi ya vitatizi
vinavyojitokeza katika mawasiliano. Kuna kitatizi cha maana mfank mouse
huju...panya. Pia ishara au picha huongelea maana mbalimbali kulingana na
wakati . Aidha kitatizi kingine ni cha saikolojia mtu anakuwa anaweza mambo
mengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano mtu anakuwa anashindwa kuelewa kwamba hiyo
ishara inamaanisha nini, pia hata kwenya maamuzi mtu anashindwa kuwa na
kumbukumbu halisi kutokana na masuala ya kisaikolojia. Pia matatizo ya milango
ya fahamu kama vile kutosikia vizuri husababisha mtu kushindwa kusikia vizuri
wakati wa mazungumzo yanapofanyika. Aidha tatizo la kutoona vizuri linaweza
kupelekea mtu anaweza kuziona vizuri na kupelekea mtu asiweze kuziona ishara
vizuri na kupelekea mawasiliano kukwama wakati wa mazungumzo hayo.
Mawasiliano
ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanaongozwa na kanuni maalumu. Wood
(2009:26) anaeleza kuwa katika mazungumzo ya mdomo kuna kanuni inayoongoza
mawasiliano kwani mzungumzaji huanza kuongea kisha msikilizaji humsikiliza na
baada yakusikiliza hutoa jibu. Vivyo hivyo
ishara au mawasiliano yasiyo ya mdomo mmoja huanza kutoa ishara ndipo
mwingine anafuata. Wood anatoa mfano wa utamaduni wa watu wa bara la Asia
ambapo mtu mwenye umri mkubwa huanza kuongea wakati mwenye umri mdogo anakuwa
anamsikiliza bila kumkatisha mazungumzo yake na baada yakumaliza mzungumzaji
atampa nafasi msikilzaji kujibu. Aidha anaendelea kueleza kuwa hata katika
sehemu za kazi mtu mwenye nyazifa ndogo huendelea kumsikiliza mpaka atakapo
maliza ndipo atakapo pewa nafasi ya kutoa mwitiko au mrejesho wa kile
kilichosemwa.Hii haina tofauti sana na utamaduni wa kwetu Afrika ambapi
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo huongozwa na kanuni/kaida. Licha yakuwa
na mfanano wa mawasiliano ya mdomo.
Ingawa
mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanafana lakini pia
yanatofautiana. Zifuatazo ni tofauti kati ya mawasiliano kati ya mawasiliano ya
mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo.
Mawasiliano
ya mdomo yanatumika kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mawasiliano ya yasiyokuwa
ya mdomo. Kwa mujibu wa Mehrabian (1983:29) anaeleza kwamba inakadiriwa kuwa
asilimia hamisi na tano mpaka tisini na tano ya mawasiliano huchangiwa na
mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo katika upashanaji habari ambapo waliosoma
mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanatumika asilimia kubwa ukilinganisha na
mawasiliano ya mdomo hutumika kwa kiasi kidogo kuliko yale ya mdomo.
Mawasiliano
ya mdomo ni rahisi ukilinganisha na mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo. Kwa mujibu
ww Beardsley na wenzake (2003:29) wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya
mdomo ni magumu ukilinganisha na mawasiliano ya mdomo, wanaona kwamba sababu
inayofanya mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo kuwa magumu yanasababishwa na
ishara, picha, maandishi kuwa magumu kuvielewa pindi vinavyotumika kuwasilishia
ujumbe, wakati mawasiliano yanahusisha sauti ambayo ni rahisi kwa msikilizaji
kufasiri taarifa au hisia zinazowasilishwa.
Pia
mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha mchanganyiko wa tabia, saikolojia
mwitiko wa mwinguliano wa watu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine
wakati mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti. Beardsley na wenzake
(wameshatajwa) wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha
vitu vingi ikiwemo tabia, saikolojia ambavyo humsaidia kuelewa ishara, alama na
maandishi wakati ambapo mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti peke yake.
Vilevile
mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo huwa hayabadilikibadiliki wakati mawasiliano ya
mdomo yanabadilika. Boman (1969) akinukuliwa na Beardsley (2003:29) anaeleza
kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo hayabadiliki badiliki. Kwa mfano
maandishi, ishara na alama huwa hazibadiliki kulingana na muktadha wa
mawasiliano. Wakati mawasiliano ya mdomo yanabadilika kulingana na hali ya
msemaji na hali ya msemeshwaji.
Kwa
ujumla uanishaji wa aina za mawasiliano umekuwa na changamoto mbalimbali katika
kuzianisha kulingana na wataalamu. Hii inatokana na vyanzo vinavyotumika.
Lakini tunaona kwamba kigezo kizuri cha kutumia kuainisha aina za mawasiliano
ni jinsi au namna mawasiliano yanavyotumika ambapo ndipo tulipopata aina mbili
za mawasiliano.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com