Newmark (1982) Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe uleule
ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine.
Jaribio kwa sababu si mara zote unaweza kufanya hivyo kwani unaweza
kushindwa au kufaulu.
*
Udhaifu wa Newmark katika fasili yake ni kwamba hakuzingatia umbo la kazi
yenyewe au mtindo wa kazi yenyewe. Mfano; kadi ya mwaliko, barua nk.
Mwansoko na wenzake (2006) Tafsiri ni zoezi la uhawilishaji
(Transferring) wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi lugha
nyingine.
* Ukiangalia wataalamu hawa wawili
utaona kwamba wanafanana; kwani wanaona kuwa tafsiri hufanywa katika maandishi.
Nida na Taber (1969) wanaona kuwa tafsiri hujumuisha upya ujembe wa
lugha chanzi kwa kutumia visawe asilia vya lugha lengwa vinavyokaribiana zaidi
na lugha chanzi, kwanza kimaana na pili kimtindo. Kwa mfano; “Damu nzito kuliko
maji” – "Blood is thinker than water”. Ndugu yako ni muhimu zaidi kuliko
mtu mwingine. “Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni” – “Wonders never end”
* Nida na Tiber wanaona kuwa
katika tafsiri kitu muhimu ni kuzingatia maana na mtindo.
MFASIRI NI NANI?
Ni mtu yeyote anayejishughulisha na kazi za kutafsiri.
Ni mtu mwenye taaluma au ujuzi wa kutafsiri na ambaye anajishughulisha
na kazi hizo (weledi-Professionalism)
MATINI NI NINI?
Ni wazo au mfululizo wa mawazo ambao unajitosheleza kimaana. Matini
inaweza kuwa neno moja, kirai, kishazi, sentensi, aya, kifungu cha habari nk.
AINA ZA MATINI (Text)
Kuna aina mbili za matini ambazo ni Matini Chanzi/Chasili na Matini
Lengwa/matini tafsiri.
· Matini Chanzi/chasili (MC)
“Source Text” ni matini ambayo iko katika lugha yake ya awali au lugha yake
iliyoandikiwa kabla ya mchakato wa kutafsiri.
· Matini Lengwa/tafsiri (ML)
“Target Text” ni matini iliyotafsiriwa kutoka lugha yake iliyoandikiwa.
Lugha Chanzi/Chasili (LC) ni lugha iliyotumika kuandikia matini chanzi
(Source language)
Lugha Lengwa (LL) (Target language) ni lugha iliyotumika kutafsiria matini chanzi au lugha unayoitumia kufanyia
tafsiri.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com