.
WIMBO.
Ni utungo wenye mishororo au mistari mitatu. Mistari hii inaweza ikawa katika
mikondo tofautitofauti. Utungo huu unaweza kuwa na kina kimoja mwishoni mwa
kila mshororo, na mishororo ya nyimbo huundwa kwa vipande viwili,
SHAIRI.
Ni utungo ambao kila ubeti una mishororo mine na kila mshororo una vipande
viwili vya mizani nane kwa nane.
UTENZI. Ni
utungo wenye mizani pungufu ya kumi na mbili kwenye mistari au mishororo, vina
vyake hubadilikabadilika kila ubeti. Kina cha mstari wa mwisho wa kila ubeti
hakibadiliki na huitwa BOHARI. Husimulia visa virefu vya kihistoria, hadithi au
mawaidha marefu mfano utenzi wa Mwanakupona na utenzi wa vita vya wadachi.
ZIVINDO. Ni mashairi
yenye kufafanua maana za maneno.
TUMBUIZO.
Ni utungo ambao hauna idadi maalumu ya mshororo wala mizani na urefu wa kila
mstari hufuata pumzi ya msemaji na huwa na vina vya mwisho na mara chache huwa
na vina vya kati bila mpangilio maalumu.
HAMZIA. Ni utungo wenye mishororo miwilimiwili na
vina viko mwishoni mwa beti tu. Hamzia ni arudhi ya kiarabu inayorejelea shairi
lolote linaloishia katika hamzia. Ni shairi lolote linaloishia katika sauti ya
glota. Kila ubeti una mishororo miwili tu na una silabi kumi na tano kwa kila
mshororo.
INKISHAFI.
Ni utungo ambao umetokana na utenzi wa Inkshafi wa Said Abdalah bin Al bin
Nasir. Utungo huu unafunza dini na hutumika kutoa mafunzo ya kidunia. Una
mishororo mine na mizani kumi na moja kwa kila msitari.
UKAWAFI. Ni
utungo wenye vipande vitatu, ukwapi, utawa na mwandamizi. Ukwapi ni kipande cha
kwanza cha mstari, utawa ni kipande cha pili katika mstari na mwandamizi ni
kipande cha tatu. Kila ubeti huwa na mishororo mitatu, mine au mitano na mizani
hutofautiana kwani kila kipande huwa na idadi yake ya mizani. Maudhui ya tungo
hizi huusu dini na masuala ya kidunia.
WAJIWAJI.
Ni utungo ambao una mishororo mitano kila ubeti. Mshororo mmoja una mizani 15.
Ni utungo unaotungwa na watu wawili. Huhusu dini na mashujaa au bingwa wa kitu
fulani.
WAWE. Ni ushairi wa kilimo hivyo maudhui yake huusu
kilimo. Asili yake ni kaskazini ya mwamba wa pwani maeneo ya lamu na pate.
Ushairi huu huibwa wakati wa kukata vitu, kuchoma magugu na kupanda mavuno.
Unadhima ya kutiana nguvu na moyo.
KIMAI.
Ni utungo unaohusu mambo ya bahari na usfiri wa baharini. Hizi ni nyimbo za
uvuvi au kazi z uvuvi, haina idadi maalumu ya mizani na haina vina.
NGONJERA.
Ni utungo wa majibizano kuhusu mada fulani.
KIKWAMBA.
Huu ni utungo ambao neno moja hutumia katika kila mwanzo wa mishororo ya ubeti.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com