Ushairi
ni utanzu mkongwe sana katika Fasihi ya Kiswahili.
Lyndon
Harries – Chimbuko au chanzo cha Ushairi ni uislamu au Fasihi ya Kiarabu.
Ushairi huu ulianza karne ya 17 katika maeneo ya pwani ya kaskazini ya Kenya
maeneo ya Lamu. Aliangalia maudhui ya Ushairi wa Kiswahili na kuona kuwa
yanatokana na dini ya Kiislamu na Ushairi wa Kiarabu. Aliangalia mianzo ya
tungo za Ushairi wa Kiswahili na mianzo ilikuwa ni aya mbalimbali za Quruan.
Aliangalia misamiati na kugundua kuwa msamiati mingi ina asili na lugha ya
Kiarabu. Aliangalia hati ya maandishi na kugundua kuwa ni hati ya Kiarabu ndo
ilikuwa ikitumika.
Mulokozi
na Sengo (1995) wanaeleza kuwa kuusishwa kwa ushairi wa Kiswahili na ushairi wa
Kiarabu pamoja na Uislamu kunampelekea Harries kutoa kauli inayomchanganya
mwenyewe.
Jan
Knappert – chanzo cha ushairi wa Kiswahili ni Ngoma na umechanganya utamaduni
wa kiajemi na uislamu na ulianza pwani ya kaskazini mwa Kenya na kuenea mpaka
sehemu za kusini na ulianza karne ya 17.
Kwa
ujumla chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni
utamaduni wa waswahili wenyewe. Asili ya Ushairi wa Kiswahili ni nyimbo
na ngoma za asili za Waswahili wenyewe. Nyimbo hizo zilikuwa zikiimbwa kwenye
harusi, sherehe za jando na unyago wakati wa kazi na wakati wa kubembeleza
mtoto.
Mulokozi
na Sengo (1995) wanadai kuwa asili ya Fasihi ya Kiswahili haiwezi kutenganishwa
na maisha, utamaduni na lugha waliyoibuni. Asili au chanzo cha ushairi wa
Kiswahili inabidi kuangalia fasihi ya waswahili, lugha pamoja na utamaduni wao.
Mulokozi
na Sengo wanakubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni ngoma na nyimbo za
Kiswahili na haukutokana na Uajemi na Uislamu.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com