Flower
Flower

Saturday, March 10, 2018

AINA/MBINU/NJIA YA TAFSIRI/KUFASIRI


Waandishi wengi wanakubaliana kwamba kuna njia nne zitumikazo katika tafsiri:
Wataalamu wengi wanakubaliana kwamba kuna aina nyingi za tafsiri kama zilivyo matini nyingi za tafsiri. Kuna mbinu nyingi za tafsiri kama zinavyobainishwa na wataalam mbalimbali lakini Mwansoko (2006) anasema kuna mbinu kuu nne:
        1.      Tafsiri ya neno kwa neno (word for word translation) neno baada ya neno
        2.      Tafsiri sisisi (literal translation)
        3.      Tafsiri ya kisemantiki (semantic translation)
        4.      Tafsiri ya kimawasiliano

    I.     TAFSIRI YA NENO KWA NENO/NENO BAADA YA NENO.

           Tunapotafsiri matini kwa mbinu ya neno kwa neno, hapo tunafanya tafsiri ya matini chanzi kwa kuzingatia maana za msingi za maneno katika lugha chanzi na kutafuta maneno hayo katika lugha lengwa. Katika mbinu hii ya tafsiri maneno na maneno hufasiriwa/hutafsiriwa yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi au za kikamusi bila kujali muktadha wa matumizi. Mpangilio wa maneno katika matini lengwa(ML) hufuata sarufi ya matini chanzi(MC). Matini lengwa, yaani tafsiri mara nyingi huandikwa chini ya kila mstari katika matini chanzi. Kwa mfano:-
                        “wa-toto            wa-dogo        wa-na-imba           kwa         furaha”
                        (pl)child           (pl)small       (pl)s.a.m -   pre-                  for         happness
Plural subject agreement mark

I              like         bananas            more            than              oranges
Mimi    penda      ndizi-wingi       zaidi             kuliko            chungwa-wingi

Faida ya mbinu
1.      Husaidia kufahamu muundo wa kisarufi wa lugha chanzi
2.      Mbinu hii hutumiwa na wanaisimu katika uchambuzi wa sarufi za lugha mbalimbali
Dosari/upungufu/udhaifu wa mbinu
ü  Mbinu hii si nzuri hasa kwa matini ndefu kwa sababu taarifa inayotolewa haina uangavu (haijielezi vizuri)


II.     TAFSIRI SISISI

    Katika tafsiri sisisi maneno hutafsiriwa yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi au za kikamusi katika lugha chanzi.Tofauti na tafsiri ya neno kwa neno tafsiri sisisi hufuata/huzingatia sarufi ya lugha lengwa

ü  Walimpa msukumo mkubwa katika biashara yake.
They gave him/her a big push in his/her business
            They gave him/her a big push in his/her business

ü  One day my dreams will come true
Moja     siku     angu    ndoto      (w.ujao)   kuja      kweli
Siku moja ndoto zangu zitakuja kweli

Faida za mbinu
Husaidia kufasiri dhana au matini zisizotafsirika kirahisi.Mfano; majina/maandishi ya kanga, misemo, nahau nk.
Hasara/udhaifu wa mbinu
Si mbinu nzuri kutafsiri matini ndefu ingawa ni mbinu bora ikilinganishwa na mbinu ya neno kwa neno.

III.     TAFSIRI YA KISEMANTIKI/WAZI

ü  Huegemea zaidi upande wa mwandishi au upande wa matini chanzi
ü  Hulenga kufasiri kila kipengele katika matini chanzi.
ü  Huzingatia sarufi ya lugha lengwa
ü  Huzingatia zaidi maana ya matini chanzi kiasi kwamba huwa na mwelekeo wa kuwa fafanuzi kwa sababu inataka kufasiri kila kipengele kilicho kwenye matini chanzi. Kwa mfano;

®   Tanzania Electric Supply Company Limited
Kampuni tanzu ya ugavi wa umeme Tanzania
®  Alikwenda mpaka nyumbani kwake
She/he went up to her/his home
® Wonders never end
Maajabu kamwe hayaishi

    Faida ya mbinu hii: -

ü  Husaidia sana kufasiri matini elezi
ü  Husaidia kuitajirisha lugha lengwa kwa misemo au semi mbalimbali kutoka katika matini chanzi.mfano
·         Yote kwa yote (All in all)
·         Natambua uwepo wako (I acknowledge your presence)
·         Haijalishi (It doesn’t matter)
·         Mwisho wa siku (At end of the day)
·         Mwisho lakini si kwa umuhimu (Last but not least)
·         Mabibi na mabwana (ladies and gentileman)
·         Mwisho lakini si kwa umuhimu (last but not least)

Hasara ya mbinu hii:

ü  Hukosa vionjo (haivutii) na kumfikirisha sana msomaji
ü   Mbinu hii huwa ni ya mzunguko na ya kifafanuzi mno. Mfano; Tafsiri ya neno Autumn

IV.      FAFSIRI YA MAWASILIANO/KIMAWASILIANO AU TAFSIRI HURU

ü  Mbinu hii huegemea zaidi upande wa hadhira lengwa
ü  Mbinu hii huzingatia utamaduni,itikadi,mazingiranahistoria ya jamii lengwa.
ü   Hulenga msomaji wa matini lengwa apate athari ileile kama aipatayo msomaji wa matini chanzi.

®® Hii ndiyo mbinu ya tafsiri inayotumika kutafsiria matini nyingi zaidi kuliko mbinu zilizotangulia na kwa sababu hii ndiyo mbinu bora zaidi ya nyingine mbinu hii hufaa zaidi kufasiria matini Arifu na Amili.

®© Katika mbinu hii mfasiri hutafuta visawe katika lugha lengwa kama vile misemo na methali ambazo maana zake na mikitadha yake ya kimatumizi hufanana na maana ya lugha chanzi au matini chanzi. Kwa mfano;

a)    Walimpa msukumo mkubwa katika biashara yake
®They gave him a big support in his business
®They helped him a lot in his great deal/in his business
® They asisisted him/her a great deal in his/her business
b)    Tanzania National Electric Supply Company Limited
®Shirika la Umeme Tanzania
c)     Wonder never end
®Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni
d) Christmas comes but once a year
®Mtumaini cha nduguye hufa masikini

e) A stich in time saves nine.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny