Jumatano ya September 13 2017 michezo ya UEFA Champions League hatua ya Makundi iliendelea tena barani Ulaya kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali.
Game ya Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo walicheza dhidi ya Apoel huo ukiwa ni moja kati ya michezo nane ya UEFA Champions League iliyochezwa usiku wa September 13, Real Madridwaliikaribisha Apoel katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amerudi uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kufungiwa mechi tatu LaLiga kwa kosa la kumsukuma refa ila amerudi kwa kishindo na kuifungia Real Madrid magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0.
Cristiano Ronaldo alifunga magoli hayo mawili dakika ya 12 na 51 kwa mkwaju wa penati na baadae Sergio Ramos akafunga goli la tatu, baada ya kufunga magoli mawili sawa na mpinzani wake Lionel Messi sasa wote wanaanza safari ya kuwania ufungaji bora wa UEFA 2017/2018 sawa na Harry Kane, Felipe Perdo, Edinson Cavani, na John Stones wote wakiwa na magoli mawili.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com