Wataalamu
mbalimbali wamefasili maana ya kama ifuatavyo
Trudgil(1974)
wanafasili lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano
miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.
Weber (1985)
Lugha ni mfumo wa mawasiliano ya wanadamu ambao hutumika mpangilio maalumu wa
sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi.
Tuki (1990)
Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni
unaofanana ili kuwasiliana.
Sapir (1921)
Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilisha mawazo, maono
na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari.
Kuna mambo muhimu yanayopatikana katika
lugha
*
Lugha ni mfumo.
*
Sauti za lugha ni nasibu.
*
Watumiaji wa lugha ni wa jamii moja wenye utamaduni mmoja.
*
Sauti za nasibu ni za kusemwa na watu
*
Lugha ni njia ya mawasiliano.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com