Flower
Flower

Monday, September 11, 2017

Inachopanga kufanya Liverpool baada ya Sadio Mane kufungiwa game tatu


Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool Sadio Mane kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Man City uliyomalizika kwa Liverpool kupoteza kwa magoli 5-0, chama cha soka cha England FA kilimfungia Mane mechi.
Sadio Mane alifungiwa mechi tatu baada ya kumchezea faulo mbaya golikipa Ederson iliyofanya imchane usoni na kushonwa nyuzi kadhaa katika jeraha hilo usoni, hata hivyo habari zilizoripotiwa leo ni kuwaLiverpool inajiandaa kukata rufaa kupinga urefu wa adhabu ya kufungiwa mechi tatu Sadio Mane kuwa ni kubwa.
Kama Sadio Mane ataendelea kuitumikia adhabu hiyo ya mechi tatu, ina maana ataikosa michezo mitatu yaLiverpool wa September 15 dhidi ya BurnleyLeicester City na game dhidi ya Newcastle United.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny