Katika lugha ya
Kiswahili kuna mitazamo mbalimbali kuhusu maana ya fasihi na wataalamu
mbalimbali wameelezea maana ya fasihi kama ifuatavyo
Wallen
na Wallek 1986 wanadai kuwa Fasihi ni jumla ya
maandishi yote katika lugha fulani. Wataalamu hawa wanadai kuwa maandishi au
machapisho ya aina yoyote ni fasihi.
Hollis
Summer 1989 anadai kuwa Fasihi ni maandishi bora au
jamii ya kisanaa yenye manufaa ya kudumu. Mtaalamu huyu anadai kuwa maandishi
yote yaliyobora ni fasihi, je maandishi yasiyobora sio fasihi?
Kant
na Hegel Eagleton 1983 wanadai kuwa fasihi ni sanaa ya
lugha yenye ubunifu bila kujali kama imeandikwa au la. Jambo la kujiuliza ni
kwamba kama fasihi haijali jambo lililo andikwa au kutoandikwa je maongezi
baina ya watu ni fasihi?
Sengo
na kiango 1973 katika Hisi zetu wanadai kuwa fasihi ni
hisi. Wanadai kuwa mambo yaliyoko kwenye fasihi ni hisia za watu juu ya jambo
fulani katika jamii. Mfano ili mwandishi aweze kuandika jambo fulani husukumwa
na hisia zinazompelekea kuandika jambo
hilo. Mathalani wasanii wa nyimbo husukumwa na hisi zinazowafanya watunge
nyimbo zao.
Kwa ujumla fasihi sanaa
ya lugha yenye ubunifu inayofikisha ujumbe kwa jamii na kusawiri vipengele vya
maisha, mahusiano na hisi za watu katika muktadha fulani.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com