Flower
Flower

Monday, September 11, 2017

AINA ZA ISIMU.


a) Isimu jamii. Trudgil (1980) anafafanua isimu jamii kuwa ni isimu inayojishughulisha na uchunguzi wa uhusiano baina ya lugha na watumiajai wa lugha hiyo. Mambo ambayo huchunguzwa ni sera ya lugha, lahaja, rejesta, usanifishaji,na lugha sanifu.
b) Isimu falsafa. Kwa mujibu wa Tuki (1990) wanasema isimu hii hujishughulisha na kuonesha dhima ya lugha katika kuelewa na kufafanua  dhana mbalimbali za kifalsafa kwa upande mmoja na kudhihirisha hadhi ya falsafa.
C) Isimu tiba. Hujishughurisha na kurekebisha dosari zinazo jitokeza katika lugha kwa kutumia utaalamu wa kiisimu.Taaluma hii huwasaidia watu ambao hawawezi kuzungumza kabisa au wanamatatizo katika uzungumzaji wao. Ni tawi ambalo hutatua matatizo ya kisarufi.
d) Isimu nafsia. Twa hili hujishughulisha na uchunguzi wa jinsi binadamu anavyojifunza lugha. Mfano hueleza hatua mbalimbali ambazo mtoto hupitia wakati wa anapojifunza lugha yake ya kwanza, pia huchunguza matatizo yanayohusiana na ujuzi wa lugha na jinsi ya kuyatatua matatizo hayo. Pia isimu nafsia hueleza kuwa upo uhusiano kati ya akili/ kufikiri na lugha.
e) Isimu linganishi. Isimu hii huchunguza lugha mbalimbali na kuzilinganisha na pia kuzilinganua. Huchunguza lugha katika viowango vyote kama vile fonolojia mofolojia semantiki na sintaksia na kuonesha jinsi lugha hizo zinazofanana na kutofautiana. Isimu hii imesaidia kubainisha makundi ya lugha mbalimbali.
f) Isimu fafanuzi. Hufafanua vipengele vyote vya lugha husika, huelezea jinsi lugha ilivyokuwa zamani, ilivyo sasa. Isimu fafanuzi haitilii mkazo mabadiliko yaliyotokea katika lugha hata kama mabadiliko hayo yapo.
g) Isimu ya kiafrika. Isimu hii huchunguza lugha zinazozungumzwa katika bara la Afrika. Wanaisimu hawa huzifafanua lugha hizi na hatimae kuzigawa katika makundi ya kinasaba, kimuundo, kijiografia na kiuamirifu.

h) Isimu tumizi. Hushugulikia zaidi matumizi ya nadharia, mbinu na matokeo mbalimbali ya kiisimu katika kulezea mambo mbalimbali yanayohusu lugha. Mfano hutumiwa wakati wa kufundishia lugha za kigeni, wakati wa kutafsiri na wakati wa kutafsiri na wakati wa kutengeneza kamusi

1 comment:

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny