Nadharia ya urasimi
Kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni wakati maalumu ambapo misingi ya kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwa vipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina maana kwamba kila jamii ina urasimi wake. Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo kati ya karne ya 18 na karne ya 18. Nao urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya karne ya nne (KK) na takriban karne ya nne (BK). Ieleweke kuwa si sahihi kuamini kama baadhi wanavyodhani kuwa unapozungumzia urasimi, huwa na maana ya msingi ya kitaaluma iliyowekwa na Wagiriki na Waroma wa kale.
Sifa za urasimi kwa ujumla
Pamoja na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila jamii ina urasimi wake, lakini bado tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi mahali popote ulipo. Kwa mfano:
Kazi ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana kuwa wazo linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya Kinjozi (mf. Nagona, Mzingile, Bina-Adamu, Walenisi) haitumiwi. Uhalisia unasisitizwa.
Kazi nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora. Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila unapoisoma wazo jipya hupatikana.
Fani na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na jinsi kinachoelezwa.
Katika urasimi wa Kigiriki watu mashuhuri ambao walikuwa wanarejelewa sana ni kama Plato, Aristotle, Horace na Longino. Kazi maarufu kwa upande wa Tamthilia inayoweza kutumika kama mfano wa urasimi wa enzi hizo ni kama ile ya Sofokile iitwayo Mfalme Edipode (1971) iliyotafsiriwa na Samuel Sateven Mushi.
URASIMI WA KISWAHILI
Njogu na Wafula (2007) wanasema kuwa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili zipo. Hata hivyo uhakiki wa kirasimi kuhusu kazi hizo ni nadra kupatikana. Msomaji wa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili anapaswa kuhitamidi uhakiki wake kutokana na utunzi wenyewe. Urasimi wa Kiswahili ulifikia kilele chake katika karne ya 18 na 19. Kazi zinazodhaniwa kuhusishwa na urasimi wa Kiswahili ni pamoja na hizi: Utenzi wa Al-Inkshafi, Utenzi wa Hamziyya, Utenzi wa Mwanakupona. Kazi za watunzi wa mashairi ya unne (tarbia) kama Muyaka wa Muhaji, Mohammed Mataka na Ali Koti, Sheria za kutunga mashairi na Diwani ya Amri (1954) (Amri Abeid).
Kazi zingine za kirasimi kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007:21) ni kama vile riwaya za; Kiu (M.S.Mohamed, 1972), Utengano (S.A. Mohamed, 1980), Harusi za Buldoza na Hadithi nyingine (S.A. Mohamed, 2005)
Pia tamthilia kama: Kinjeketile, Mashetani (E.N. Hussein, 1969, 1971), Kilio cha Haki (A.M Mazrui, 1982), Sauti ya Dhiki (A.Abdalla, 1973).
Sifa ya fasihi ya Kiswahili katika misingi ya Kirasimi
Huu ni wakati ambapo misingi ya ushairi andishi wa Kiswahili ilipowekwa.
Mengi ya mashairi ya kirasimi yalipokezwa kwa mdomo na uhakiki pia ulifanywa kwa njia ya kimasimulizi.
Mashairi yalitumia lugha teule
Warasimi wa Kiswahili walitumia lugha rahisi iliyoeleweka na ujirani wao bila shida yoyote.
Masimulizi marefu kama vile utenzi yana mwazo, katikati na hatimayake.

No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com