Flower
Flower

Sunday, October 13, 2019

NADHARIA YA ONTOROJIA KATIKA FASIHI

Nadharia, Kwa mujibu wa TUKI (2004), Wanasema nadharia ni mawazo, maelezo, mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo fulani.
Nao Njogu na Rocha (2008), wanasema nadharia ni kioo cha kumulika kila jambo au tendo limuhusulo binadamu ulimwenguni  inakuwa ngumu gizani.
Pia Wamitila (1996), Anasema kuwa, nadharia ni maarifa ya kitaalamu ambayo msomaji au mhakiki anapaswa kuyajua na kuyafahamu kabla ya kuanza kazi zake.
Hivyo basi sisi tunakubaliana na TUKI, kwa kusema nadharia ni mawazo, maelezo,mwongozo uliopagwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo fulani.
Ama kuhusu Ontologia huu ni moyo wa falsafa. Ontologia ni tawi la falsafa ambalo huchunguza asili ya vitu, (binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke wapi?,shetani ni nini?) Pia huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo hai na vitu visivyokuwa hai, vinavyoonekana na visivyoonekana.
Maana ya Ontologia tunaweza kusema ni falsafa ya utafiti wa asili nya kuwa wakati wa kuwepo au ukweli.wanaendelea kusema neno ontolojia asili yake ni kigiriki.
Ontolojia, pia ni nadharia ya vitu na mahusiano yao,inatoa vigezovya kubainisha aina tofauti ya vitu (halisi na kufikirika,uwepo na haipo,kweli na bora,kujitegemea na tegemezi) na mahusiano yao.
Naye Mihanjo A, (2010) akimnukuu Anselm katika nadharia yake ya kiontolojia,anselmamethibisha ontolojia kwa kuonyesha uishi wa Mungu.Anselm ameelezea na kuonyesha asili na uishi wa Mungu.
Kwaujumla Ontolojia  ni tawi la falsafa ambalo huchunguza asili ya vitu,(binadamu ametoka wapi?,dunia imetoke wapi?,shetani ni nini?)pia huchunguza uwepo wa vitu mbalimbali,vitu vilivyo hai na vitu visivyokuwa hai,vinavyoonekana na visivyoonekana.
Mkondo tulioutumia ni mkondo wa falsafa za kijamii na kisiasa . Mkondo huu unazingatia na kuangalia falsafa za jamii na siasa. Mkondo huu umefafanuliwa na kuelezwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Keneth  Kaunda na Kwame Nkurumah.
Tukianza na ; Mwalimu Julius Kambalage Nyerere ambaye anatetea mkondo huu kwa vigezo vifuatavyo;
Anadai kuwa ujamaa wa kiafrika ni kama Afrika pana ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa kifamilia na kuishi vizuri na watu vilevile anadai kuwa si ujamaa wa kimax ambao unatetea mgogoro wa kitabaka.Yeye anaona asili ya ujamaa ni jamii za kiafrika.
Sera ya mipango inajadiliwa na kurekebishwa na watu wote.Kila mtu alifanya kazi  katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu alipata matunda kulingana na kazi yake.
Anaendelea kusema, ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu.Hivyo wito wake ni kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Mtaalamu mwininge ni Kwame Nkurumah ambaye ametumia vigezo vifuatavyo;
Anadai kuwa ujamaa ulikuwa msingi  wa jamii za kiafrika kuliko ubinafsi hivyo ubepari utaiharibu Afrika, Afrika haita kuwa huru ikiwa itaendelea kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.
Huyu aliathiriwa na falsafa ya kimarx na renin lakini hakutaka kuitumia kama ilivyo alitaka uimalishwe ujamaa wenye asili ya kiafrika na vipengele vya kiislam na kikristo vya ulaya.
Keneth Kaunda alisema waafrika walifanikiwa  kuushinda ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu katika kufikia ukamilifu wa utu binadamu lazima alenge kufanana na mungu. Mungu ni usawa wa kila kitu,mungu ni amani,upendo na utu,utu unavileta pamoja dini na siasa na kuzaa taifa la watu wanaopendana.
Anamalizia kwa kusema kuwa nguvu katika kujikomba si mbinu sahihi ya ukombozi bali nguvu inaweza kutumika katika kujilinda  aliandika  African humanism.
Baada ya kueleza mkondo na vigezo vya wataalam wa falsafa za kijamii na siasa ,tunachambua riwaya ya kufikirika ambayo ni kazi ya fasihi ya kiafrika kwa kutumia mkondo wa falsafa za kijamii  na kisiasa.
Riwaya ya kufirika ameandikwa na Shahban Robert chapa ya nne mwaka (2008) kufikirika ni riwaya inayohusu maisha na maswaibu yaliyo mkuta mfalme na malkia wa kufikirika kwa kuchelewa kupata mototo.
Uchambuzi wetu unaanza kama ifuatavyo;
Suala la imani, imani ni kuwa uhakika wa mambo yatarajiwayo. Nyerere anasema kuwa kila mtu alifanya kazi katika ardhi ya jamii nzima na kila mtu alipata matunda ya kazi yake. Katika riwaya hii( uk3-4), unaonyesha jinsi ,mfalme anavyoamini kuwa na watoto wengi ndio nguvu ya ufalme wake pia mfalme aliamini waganga, kafara,ramli,hirizi,mazinguo,mashetani na watabiri.(Uk 8-11), ndio maana mfalme aliwaita waganga wote wafike kwake ili waweze kuagua na kutabiri juu ya utasa na ugumba wao.
Utawala, katika riwaya hii mwandishi ameeleza suala la utawala kwa kumtumia mfalme kama mfano wa mtawala mwenye uongozi mbovu wenye mabavu (uk 4) mfalme alipoamua waitwe waganga wote wa jadi mfano waganga wa mashetani,makafara,watabiri,hirizi,wa mizizi,mazinguo na mashetani asiye hudhulia apewe adhabu pia katika uk(23-25) mfalme anamfukuza mwalimu kazi.
Suala la ukombozi,ukombozi ni hali ya kujitoa kutoka hali  fulani kwenda hali nyingine .Katika riwaya hii kuna ukombozi wa kisiasa,mwandishi amemtumia mjinga,ameonyesha jinsi mjinga alivyosimama kisheria dhidi ya kifo kilichokuwa kinawakabili,kifo  ambacho hakikuzingatia utu wa binadamu (uk38.)KenethKaunda ansema, waafrika walifanikiwa kuushinda ukoloni kwa sababu ya utu sio nguvu,katika kuufikia ikamilifu wa utu binadamu lazima alenge kufanana na Mungu.
Matabaka katika jamii, matabaka ni mgawanyiko wa makundi ya watu  (kiuchumi,kisiasa,kielimu na kijamii) katika jamii. Katika riwaya hii kuna matabaka makuu mawili,tabaka la kwanza ni tabaka tawala,ambalo liliundwa na viongozi wa serikali, wanasheria,mahatibu na wafanya biashara,tabaka tawaliwa lilikuwa ni wakulima,(tabaka la mwisho),(uk 35-36).Matabaka katika jamii hayafai kwani huondoa umoja,Nyerere anapinga matabaka hivyo wito wake ni kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Athari za uongozi mbaya, huu ni uongozi usiofuata haki za raia wake, baada ya maamuzi ya mfalme kuwaruhusu waganga mfano;waganga wa mizizi walichimba mzizi ya mti,walitoa magome na kukata matawi ya miti,hali iiliyopelekea ukame wa  nchi na uharibifu wa mazingira na makazi ya wanyama,waganga wa kafara walitumia pia kwa moto na walihitaji damu za wanyama kwa ajili ya kafara,hivyo wanyama wengi walikufa.Ni vizuri kufikiri jambo kabla ya kutenda.
Umuhimu wa uzazi, katika riwaya hii mfalme aliona fahari yake yote si kitu kwani alikosa kuwa na mtoto (uk 1-3) anasema, Nina majeshi ya askari walioshujaa, waongozi hodari raia wema,watii ambao hawalingani na Taifa lolote jingine katika maisha yake yote nashukuru kwa Bwana vitu vya faraja,visivyokwisha lakini nina sikitiko kubwa kwa kukosa mtoto. Jamii ya kufikirika waliamini kuwa na watoto wengi ndio ujenzi wa nguvu wa Taifa lao. (uk 3) Mfalme anaamini watoto ndio nguvu ya ufalme wake.
Mapinduzi ya kisiasa,na kiutamaduni,mapinduzi ni kufanya mabadiliko, yaani kuondoa utawala au siasa ya kwanza na kuingia siasa mpya.katikas riwaya hii mjinga alitumia utu wake kufanya mapinduzi kwa kumsaidia mototo wa mfalme kupata dawa hospitalini,na kupona,wanakijiji wa kufikirika walizoea utamaduni wa kuwaamini waganga wa jadi na sio hospitali.Pia katika siasa mjinga alijaribu kutetea haki na sheria ya utu,kwa kuzuia kafara ya watu kutalewa kwani haina umuhimu.
Kazi nyingine ya fasihi  ipatikanayo Afrika ni ushairi wa fungate ya uhuru.Fungate ya uhuru ni diwani iliyoandikwa na Mohamed S. khatibu mwaka (1988). Diwani hii inajadili mambo yanayokwamisha ujenzi wa jamii mpya katika nchi zetu za Afrika. Katika diwani hii tutachambua mambo hayo kwa kutumia mkondo wa jamii na siasa. Uchambuzi wetu unaanza  kama  ifuatavyo;
Kuwa na uongozi bora ,uongozi mbaya ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya.Katika diwani hii inaonyesha jinsi viongozi wanavyotumia  madaraka yao vibaya kuwanyonya wananchi wa kawaida.Nyerere anasema sera ya mipango inajadiliwa nakurekebishwa na watu wote.Pia ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu,hivyo yeye anasisitiza kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Diwani inaonyesha kuwa uongozi mbaya ni kikwazo cha ujenzi wa jamii mpya(uk15-16) shairi la Viongozi wa Afrika,hapa mwandishi amekemea viongozi wanaotumia madaraka vibaya.Mashari mengine yanayozungumzia uongozi mbaya ni Fungate, Waja wa Mungu, Wizi, Utawala, Njama, ujamaa.
Kupinga vita ukoloni mamboleo,ukoloni mamboleo ni ile hali ya nchi kupata uhuru kisiasa lakini njia nyingine za uchumi hutawaliwa au hubaki mikononi mwa mabepari aunyingine.Kwame Nkurumah anasema ujamaa ni msingi wajamii za kiafrika kuliko ubinafsi,hivyo ubepari utaiharibu Afrika,Afrika haitakuwa huru ikiwa itaendelea kuwa chini ya ubepari wa kimagharibi.Katika shairi la Ruya,anonyesha kuwa wazungu ndio waliondoka katika ardhi ya Afrika lakini unyoyaji bado upo.Pia katika shairi la kunguru,mwandishi ameonyesha athari za ukoloni mamboleo.
Kufanya mageuzi,mageuzi huleta mafanikio katika ujenzi wa jamii mpya.Keneth Kaunda anasema waafrika walifanikiwakuushinda ukoloni kwa sababu ya utu na sio nguvu,pia nguvu katika kujikomboa si mbinu sahihi ya ukombozi bali nguvu inaweza kutumika katika kujilinda.Mwandishi naye ametoa njia mbalimbali ili kufanikisha ukombozi katika shairi la Unganeni,pia mwandishi anapendekeza kutumia silaha katika mageuzi ikiwa unyonyaji hautaondoka kwa njia ya amanimfano katika shairi la Siku itafika (uk 30) na Nikizipata bunduki).

Umoja na Ushirikiano, hii ni mbinu mojawapo ambayo mwandishi amependekeza  kama mojawapo ya njia ya ujenzi wa jamii mpya.Nyerere asisitiza watu kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Katika shairi la unganeni (uk 1) mwandishi anawataka waafrka wote tuungane ili kuendeleza mapambano ya kuleta haki na usawa.

Kujenga nchi itayofuata mfumo wa ujamaa, Nyerere anasema,ujamaa wa kiafrika ni kama Afrika pana, ujamaa ambao unakuwa mwendelezo wa kifamilia na kuishi vizuri na watu na sio ujamaa wa kimax unaotetea migogoro yakitabaka,mwandishi anashauri ujamaa kuwa ni sululisho la wanyonge,shairi la Ujamaa shairi hili linajadili wapinzani wa ujamaa.Mwandishi ansema ujamaa umeumbuliwa,umethiliwa,umekashifiwa na umesalitiwa.

Kupiga vita wizi wa mali ya umma,sehemu nyingi zimeoza kwa wizi,ikulu na viongozi wamejiunga na wahalifu.Katika shairi la Wizi na Kunguru (uk19) ameeleza wezi waliotimuliwa na kutawanywa, shairi la Joka la mdimu mwandishi anatanabaisha watu kuhusu uwezekano wa wakoloni kurudi kwa umbotofauti lakini athari ni zile zile,pia katika shairi la Naona (uk 33) anoonyesha taabu wazozipata wakulima na malipo duni wanayopewa kwa mazao yao.

Kitabu cha tamthiliya ya Nguzo mama iliyoandikwa na Penina Mhando(1982).Tamthiliya hii inasawiri na kuyaelezea matatizo mbalimbali yanayowakabili na kuwaelemea wanawake wengi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.Kwa kutumia mkondo wa kisiasa na kijamii tumechambua tamthiliya hii kama ifuatavyo;

Uongozi mbaya, katika tamthiliya hii mwandishi ameonyesha umuhimu wa uongozi bora, na kiongozi bora. Nyerere anasema ujamaa ni tofauti na ubepari unaolenga kumnyonya mtu, anasisitiza kuwa kuishi katika umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.Katika kijiji cha patata kulikuwa hakuna ujamaa. Katika jamii kiongozi anaweza kuipeleka jamii yake kwenye neema au kwenye mdomo wa simba kutegemeana na uongozi wake anavyoupeleka (uk 22), kijiji cha patata kilikuwa na uongozi mbaya wa kidikteta, mfano; Mwenyekiti, kamati ya halmashauri,wanatumia vitisho kumlazimisha Bi nane kusema asichokijua (uk24).

Uvivu na Uzembe, huwa haufai katika jamii,katika mkondo huu Nyerere anasema kila mtu alifanya kazi katika ardhi na kila mtu alikula matunda ya kazi  yake hivyo mtu akiwa mzembe atakula matunda ya uvivu na uzembe ambayo si mema.katika kijiji cha patata watu hawa walikuwa ni wavivu na wazembe,ndio maana ilipekea kufifia na kushindwa kuinua  Nguzo mama. Wanawake hawa walikuwa hawawajibiki, mfano;(uk 34)

Mapenzi na ndoa, katika Nguzo mamakuna mapenzi yasiyokuwa ya kweli,yanayoyojali pesa na usaliti kati ya wanandoa.Mapenzi haya hayana utu kwani ndani ya utu kuna amani na upendo wa kweli.Usaliti huleta hali ngumu katika familia mfano;familia ya Bi tano wanalala njaa kwa kukosa chakula na mahitaji muhimu kwa kuwa Maganga baba yao anamaliza pesa zote kwa wanawake.mfano ;

Wee Bi sita mshenzi unanichukulia mume wangu hivihivi kimachomacho(uk 39)
Umoja na ushirikiano, hiki ni kitu muhimu sana katika jamii Nyerere anasisitiza kuwa na umoja kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni .Asili ya ujamaa ni Afrika na si ujamaa wa kimarx unaotetea matabaka.Kijiji cha patata watu wake walikosa umoja na ushirikiano ndio maana walishindwa kuinua nguzo mama kwani kila mtu anajali mambo yake Bi moja anaacha kazi anaenda kuangalia khanga (uk 34
Dhuluma, hii imeghubika jamii yetu ya leo,katika tamthiliya hii ya Nguzo mama mwandishi amejaribu kutuonyesha jinsi jamii ya Patata kama zilivyo jamii iliyooza kwa dhuluma hasa pindi wanawake wanapofiwa na waume zao,mfano Bi saba anaoonyesha jinsi gani wanawake wengi wa kiafrikawanavyodhulumiwa mali na ndugu wa mwanaume zao pindi wanapofariki.Bi saba  baada ya kufiwa tu shemeji  walikuja kugawana vitu.mfano( uk 43);
.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kumba riwaya hii ya kufikirika,tamthiliya ya nguzo mama na ushairi wa fungate ya uhuru zimeweza kuchambuliwa vizuri na tawi hili la ontolojia.Tumeweza kuona ni jinsi gani vitu halisi na vingine vya kufikirika vikitendeka katika kazi hizi,vilevile suala zima la falsafa za kijamii na siasa kama zilivyokwisha elezewa hapo mwanzo.Ujamaa unaonekana kuwa ni hali inayopelekea maendeleo katika jamii,ontolojia ya kiafrika hutumika kuchambulia kazi za fasihi za kiafrika.

MAREJEO
1.Mihanjo A,(2010)Falsafa na ufunuo wa maarifa.Toriam.Morogoro Tanzania.
2.Mohamed S.k (1988)Fungate ya uhuru.Dar-es-salaam university place(DUP).
3.Muhando p (1982) Nguzo mama. Dar-es-salaam university place(DUP).
4.Njogu na Chimera R(1999)Ufundishaji wa fasihi,Nadharia na Mbinu.Jomo Kenyatta.Nairobi
5.Tuki(2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu.Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.Dar-es-salaam.
6.Robert,S.(2008) Kufikirika.Mkuki na nyota:Dar-es-salaam Tanzania.
7.Wamitila K.W (1996) Utangulizi wa Kiswahili.Chuo kikuu cha Dar-es-salaam.Dar-es-salaam.

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny