Massamba
(2009:50), anafafanua kuwa mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa kutumia njia
mbalimbali za misimbo ambayo inajulikana kwa pande zote mbili. Fasili hii
imeshindwa kuweka wazi hiyo misimbo inayotumika kwani imejiegemeza sana katika
lugha ya ishara/vitendo na kutotilia maanani sana mawasiliano mengine.
TUKI
(2012:324), wanadai kuwa mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa njia mbalimbali
kama vile simu, barua na telegram. Fasili hii inaonekana kuhusisha njia
mbalimbali katika mawasiliano kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Kwa
ujumla, mawasiliano ni mchakato wa upashanaji habari kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali zinazoeleweka na watumiaji hao. Kwa
mfano njia ya mazungumzo, ishara na maandishi.
Aidha,
kwa mujibu wa Shannon na Weaver (1948), wameonesha mchakato wa mawasiliano;
mtoa ujumbe→kisafirishaji→njia ya kusafirishia→kipokelea ujumbe →mpokeaji.
Aidha
Triganda (2009), anaeleza kuwa kuna aina mbili za mawasiliano ambazo ni
mawasiliano ya mdomo na mawasailiano yasiyo ya mdomo. Mawasiliano ya mdomo ni
aina ya mawasiliano ambayo yanahusisha sauti katika mchakato wa kimawasiliano.
Lakini mawasiliano yasiyo ya mdomo ni aina ya mawasiliano yasiyohusisha ishara
na alama katika mchakato wa kimawasiliano. Triganda (keshatajwa), anaendelea
kuelezea kuwa mawasiliano yasiyo ya mdomo yanaweza kufanyika pasipo kuhusisha
sauti.Vilevile mawasiliano ya mdomo yanaweza kufanyika bila kuhusisha ishara.
Robert na wenzake (2003:28), wanaeleza kuwa,
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo jinsi yanavyotofautiana. Wanadai kuwa
mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha tabia, saikolojia na mwingiliano wa
kimazingira, kupitia uelewa wa mtu ukihusiana na mtu mwingine anayewasiliana
nae. Hii ni tofauti na mawasiliano ya mdomo. Hivyo kutokana na maelezo ya
wataalamu mbalimbali kuna aina mbili za mawasiliano.
Aina
hizo za mawasiliano zinafanana na kutofautiana. Ufuatao ni ufanano kati ya
mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo.
Mosi,
aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa habari, taarifa, mawazo, hisia kutoka
kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mujibu wa Kacharava (2016:103),Both
involvestransmition of infotmation from one person to another. Anaeleza kuwa
miongoni mwa vipengele vinavyoleta ufanano kati ya mawasiliano ya mdomo na
yasiyo ya mdomo ni kuwa aina zote mbili zinahusisha upashanaji wa habari kutoka
kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa njia tofauti tofauti kama vile njia
ya maandishi, mazungumzo na barua.
Pili,
mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yote yanahusisha akili.
Massamba (kashatajwa), anadai kwamba mawasiliano haya huusisha akili kwa maana
kwamba mawasiliano ya mdomo huusisha masikio kwa ajili yakusikia kinachosemwa
kenda kutafsiriwa katika akili/ubongo.Pia huusishamacho ambayo yanapeleka
mrejesho kwenye ubongo unaoenda
Nne,
zote zina dhima zinazofanana. Kacharava (2016:104),anafafanua kwamba
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana dhima zinazofanana. “Both verbal and non verbal communication
are the same Rule or Function such to growth and to consolidate the relationship
between the society”. Mfano dhima
hizo ni kukuza au kuimarisha uhusiano miongoni mwa watu katika jamii.
Hivyo
jamii moja huendelea kuwa na uhusiano na jamii nyingine au mtu mmoja na mtu
mwingine kutokana na uhusiano wao wa upashanaji habari. Upashanaji huo wa
habari unaweza ukatumia ishara kama vile picha, maandishi na sauti. Pia
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yote yanasaidia kukuza utamaduni
kupitia njia za upashanaji wa habari.
Tano,
mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo yana vitatizi vinavyofanana ambavyo
vinaweza kukwamisha mchakato wa mawasiliano. Devito (2009:37), “There are several types of noise that might
interfere the communication process. Such as semantic interference, psychological,
physiological and physical interference.” Anaeleza aina ya vitatizi
vinavyojitokeza katika mawasiliano. Kuna kitatizi cha maana mfano neno mouse hurejelea panya, na kifaa
kinachotumika kwenye talakilishi. Aidha kitatizi kingine nicha saikolojia mtu
anakuwa anawaza mambo mengi kwa wakati mmoja. Mfano mtu anakuwa anashindwa
kuelewa kwamba hiyo ishara ina maanisha nini. Pia hata kwenye maamuzi mtu
anashindwa kuwa na kumbukumbu halisi kutokana na masuala ya kisaikolojia.
Tatumatatizo ya milango ya fahamu kama vile kutosikia vizuri husababisha mtu
kushindwa kusikia vizuri wakati wa mazungumzo yanapofanyika. Aidha tatizo la
kutoona vizuri linaweza kupelekea mtu kushindwa kuona vizuri na kupelekea mtu
asiweze kuziona ishara vizuri na kupelekea mawasiliano kukwama wakati wa
mazungumzo hayo.
Sita,
mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanaongozwa na kanuni
maalumu. Wood (2009:26), “Both Verbal
Communication and non verbal communication ar controlled by regurative
principles. For example traditional, in Asia home, the elder speak first while
youngster listen without interruption or contradiction.” Anaeleza kuwa
katika mazungumzo ya mdomo kuna kanuni inayoongoza mawasiliano. Mzungumzaji
huanza kuongea kisha msikilizaji humsikiliza na baada yakusikiliza hutoa jibu.
Pia katika ishara au mawasiliano yasiyo ya mdomo mmoja huanza kutoa ishara
ndipo mwingine anafuata. Wood (keshatajwa), anatoa mfano kuhusu utamaduni wa
watu wa bara la Asia ambapo mtu mwenye umri mkubwa huanza kuongea wakati mwenye
umri mdogo anakuwa anamsikiliza bila kumkatisha mazungumzo yake. Baada
yakumaliza mzungumzaji atampa nafasi msikilzaji kujibu.Hii haina tofauti sana
na utamaduni wa kwetu Afrika ambapo mawasiliano ya mdomo na yasiyo ya mdomo
huongozwa na kanuni/kaida. Ingawa mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya
mdomo yanafana lakini pia yanatofautiana.
Ingawa
mawasiliano yam domo na mawasiliano yasiyo ya mdomo yanafanana lakini pia yanatofautiana.
Zifuatazo ni tofauti kati ya mawasiliano ya mdomo na mawasiliano yasiyo ya
mdomo.
Mosi,
mawasiliano ya mdomo yanatumika kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mawasiliano
ya yasiyokuwa ya mdomo. Kwa mujibu wa Mehrabian (1983:29), “Approximately 55- 95 of communication is coontributed bynonverbal
communication.” Anaeleza kwamba inakadiriwa kuwa asilimia hamsini na tano
mpaka tisini na tano ya mawasiliano huchangiwa na mawasiliano yasiyokuwa ya
mdomo. Katika upashanaji habari mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanatumika kwa
asilimia kubwa ukilinganisha na mawasiliano ya mdomoambayo hutumika kwa kiasi kidogo.
Pili,
mawasiliano ya mdomo ni rahisi ukilinganisha na mawasiliano yasiyo ya mdomo.
Beardsley na wenzake (2003:29),Verbal communication are very easilycompeared to
Non verbal communication. Wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyo ya mdomo ni
magumu kueleweka ukilinganisha na mawasiliano ya mdomo. Beardsley na wenzake
(2003:29), wanaona kwamba mawasiliano yasiyo ya mdomo ni magumu kwasababu ya matumizi
ya ishara, picha na maandishi hivyo huwa ni vigumu kuvielewa pindi
vinavyotumika kuwasilishia ujumbe. Wakati mawasiliano ya mdomo yanahusisha
sauti ambayo ni rahisi kwa msikilizaji kufasiri taarifa au hisia
zinazowasilishwa.
Tatu,
mawasiliano yasiyo ya mdomo yanahusisha mchanganyiko wa tabia, saikolojia na
mwitiko wa mwingiliano wa watu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine,
wakati mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti. “Non verbal communication is the mixture of behaviour, response, interaction
of people from one person to anoooother person.” Beardsley na wenzake
(wameshatajwa), wanaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya mdomo yanahusisha
vitu vingi ikiwemo tabia, saikolojia ambavyo humsaidia kuelewa ishara, alama na
maandishi, wakati ambapo mawasiliano ya mdomo yanahusisha sauti peke yake.
Nne,
mawasiliano yasiyo ya mdomo huwa hayabadilikibadiliki wakati mawasiliano ya
mdomo yanabadilika. “Non verbal
communication is static unlike to vebal communication”. Boman (1969),
akinukuliwa na Beardsley (2003:29), anaeleza kwamba mawasiliano yasiyokuwa ya
mdomo hayabadiliki badiliki. Mfano maandishi, ishara na alama huwa hazibadiliki
kulingana na muktadha wa mawasiliano. Wakati mawasiliano ya mdomo yanabadilika
kulingana na hali ya msemaji na hali ya msemeshwaji.
Kwa
kuhitimisha, uanishaji wa aina za mawasiliano umekuwa na changamoto mbalimbali
katika kuzianisha kulingana na wataalamu. Hii inatokana na vyanzo
vinavyotumika. Lakini tunaona kwamba kigezo kizuri cha kutumia kuainisha aina
za mawasiliano ni jinsi au namna mawasiliano
yanavyotumika ambapo ndipo tulipopata aina mbili za mawasiliano.
MAREJELEO
Beardsley,
A (2003). Communcation Skills in pharmacy
practice. USA: Arizona State University.
Devito,
J. A(2009).Interpersonal Communication.
Newyork: Hunter college of the City University of New York.
Kacharava,
K (2016). Visual and Verbal
Communications. Europe: European Scientific Institute.
Massamba,
D.P.B (2009). Kamusi ya Isimu na falsafa
ya lugha. TUKI: Dar es salaam.
Mehrabian, A (1983). Significance of posture and position to the
Communication. Psychological
Bulletin.
Robert,
M (2003). Signalers and Receiver in
Communication. Philadelphia: University of Pennsylvania.
TUKI(2012).Kamusi ya Kiswahili na Kiingereza. Dar es
Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Triganda,
S. (2009).The Best of literarure Study
guides for your classes. Kompasiana: The University of Jakarta Publishers
limited.
Shannon,
E. C na Weaver,W (1948). Handbook of
Communication. Amazon: Atlantic Publishers Distribution.
Wood,
A. T (2009).Communication in our Lives.
Belmont, CA: Thomson Wadsworth.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com