*1.4 Mifumo ya Lugha Asilia
Lugha asilia
zina tabia ya kuchangia baadhi ya sifa kwa kuwa zote zinachota sauti kutoka
katika bohari moja la sauti. Tofauti inatokea kwa kuwa kila lugha inachukua
sauti chache tu katika bohari hilo. Pia sauti zote za lugha hutolewa na viungo
vile vile vya mwili wa binadamu, kwa hiyo inawezekana kabisa sauti zinazotamkwa
na watamkaji wa lugha fulani zikatamkwa pia na watamkaji wa lugha nyingine
kwani na wao wana viungo vile vile isipokuwa tofauti ni katika namna ya mgusano
wa alasauti hizo katika kuzalisha sauti zinazoeleweka katika lugha hiyo. Lakini
pia zote ni lugha za binadamu. Hata hivyo, Sapir (1925:16-18) anasema kuwa
lugha mbili zinaweza kuwa na bohari sawa la kifonetiki lakini zikawa na
fonolojia mbili tofauti. Hapa inamaanisha jinsi sauti hizo zinavyofuatana ili
kuleta maana ikawa ni tofauti. Tofauti hii inatokana na mfumo wa mashartizuizi
(au kanuni) ya mfuatano sauti hizo katika kuunda maneno ya lugha husika. Kila
lugha ina mfumo wake asilia wa mfuatano wa sauti, na huu ndiyo unaitwa
‘fonolojia.
Katika lugha ya
Kiswahili, kwa mfano: Hakuna koda (*Koda), mfuatano wa konsonanti 3 halisi
haukubaliki (*KKK), Mfuatano wa kiyeyusho na konsonanti halisi haukubaliki
(*yK) au mfuatano wa *ty au *ky
1.5 Sifa Majumui za Lugha katika Fonolojia
Pamoja na kwamba
lugha zina fonolojia tofauti bado inaonekana kwamba kuna baadhi ya vipengele
vya kifonolojia vinavyopatikana karibu katika lugha zote duniani au katika
lugha nyingi duniani. Hivi ndivyo huitwa ‘sifa majumui za lugha katika fonolojia’.
Kuna aina kuu tatu za sifa majumui za lugha, ambazo ni:
- Sifa Majumui Halisi za lugha: Hizi ni zile sifa ambazo ni za kawaida katika lugha zote duniani. Kwa mfano kila lugha duniani ina irabu /a/, kila lugha ina utaratibu wa kuwa na irabu na konsonanti ingawa idadi hutofautiana, kila lugha ina utaratibu wa kuwa na silabi ingawa muundo wake unaweza kutofautiana, katika kila lugha zinapofuatana konsonanti na irabu, konsonanti huanza na kufuatiwa na irabu.
- Sifa Majumui Pana za lugha: Hizi ni sifa ambazo zinapatikana katika lugha nyingi duniani lakini si zote. Kwa mfano, lugha nyingi zina irabu 5 lakini baadhi zina irabu 3, 7, nk.; Katika lugha nyingi duniani inapokuwepo sauti yenye sifa fulani basi itakuwepo nyenziye nyingine yenye kupingana na hiyo katika sifa yake (ikiwepo [+ghuna] [d] basi ipo [-ghuna] [t], nk.
- Sifa Majumui Tabirifu za lugha: Hizi ni zile ambazo zinatabirika kuwepo katika lugha kwa misingi ya kutumia sifa nyingine zinazopatikana. Katika baadhi ya lugha unaweza kutabiri kuwepo kwa sauti fulani kutokana na kuwepo kwa sauti nyenziye ambayo ni ya msingi. [t,d], [p,b], nk
Sawa kaka tunashukuru
ReplyDeleteipo poa
ReplyDeleteUnafanya kazi nzuri. Fanya utafiti zaidi katika mada anuwai za Kiswahili. Hongera.
ReplyDeleteKazi nzuri ila ongeza mifano
Delete