Flower
Flower

Thursday, October 5, 2017

sarufi,

 kuna mikabala miwili
1) Sarufi kama taaluma inayoshughulika na uchambuzi wa lugha; fonolojia, mofolojia, sintaksia, na semantiki
2) Sarufi pia ni sheria, taratibu, kanuni zinazotawala viwango vinne vya lugha
Miundo ya sarufi
1) Sarufi mapokeo
Ndiyo sarufi kongwe kabisa, ilijishughulisha na uchambuzi wa sentensi sahili
Sentensi zilichanganuliwa kwa kuzingatia vipengele 3
Kiima- mtenda
Prediketa-tendo
Yambwa-mtendwa; vipashio hivyo vilijulikana km vipashio vya kikazi
Kwa mfano;
Mtoto anakula chakula
Awamu ya pili ilizingatia uchambuzi wa sentensi kwa kuangalia aina za maneno
Awamu ya tatu ilizingatia kiima kiarifu
Udhaifu wa mkabala huu ni kwamba haukuweka mipaka ya kikategoria kati ya neno moja na jingine.
2) Sarufi msonge
Sarifi hii iliibuka baada ya sarufi mapokeo kushindwa kuweka bayana mipaka ya kategoria za maneno ktk sentensi,
Hata hivyo bado ililkuwa na mahusiano na sarufi mapokeo
Ilitazama lg km mfumo mkuu ambao ndani yake kuna mifumo midogomidogo
Yaani; fonolojia, mofolojia nk.
Hivyo basi hata ktk kiwango cha sentensi waliainisha kuwa kuna vipashio vidogo vinavyounda sentensi;
Kwa mfano kiima- nomino, kivumishi
3) Sarufi miundo virai
Tungo imeundwa na viambajengo ambavyo vinatokana na maneno;
Waliainisha kanuni za uchambuzi wa sentensi km ifuatavyo;
1) Kugawanya sentensi kuu, mgawanyo huu unahusisha KN+KT
2) Kugawanya kirai kitenzi cha sentensi
Sarufi msonge iliitazama lugha km muundo mkuu ambao ndani yake kuna miundo midogo, kwa mfano; fonolojia ndani yake kuna irabu, konsonanti, toni shada nk.
Sarufi miundo kirai yenyewe ilichambua sentensi kwa kuchambua viambajengo vyake
5) Uchambuzi wa kirai nomino, kuainisha viambajengo vyake, kwa mfano ngeli za nomino husika, aina ya nomino.
Tanbihi,
Kama kuna yambwa ktk sentensi husika basi huainishwa km N2
6) Umbo la kivumishi
7) Kiwakilishi ktk kitenzi
8) Wakati ktk kitenzi
9) Tendo linalotendwa
Baadae mtaalamu wa isimu NOAM CHOMSKY alikuja na hoja kuwa sarufi mapokeo imeshindwa kuonesha uhusiano baina ya sentensi
Hivyo akaja na hoja ya SARUFI GEUZA MAUMBO ZALISHI – ambayo ilichunguza sentensi zilizofanana sana
Hivyo kukaibuka dhana ya, umbo la ndani na umbo la nje
Umbo la ndani la sentensi ni lile umbo ambalo halijafanyiwa badiliko lolote
Umbo la nje la sentensi ni lile umbo la neno ambalo limeshafanyiwa marekebisho

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny