(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA PILI YA MAOMBI YA UDAHILI
KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA
MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kufahamisha umma kuwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Udahili, awamu ya pili imefunguliwa kuanzia tarehe 18 Septemba, 2017 hadi tarehe 1 Octoba, 2017 kwa vyuo vyote ambavyo bado vina nafasi wazi za udahili.
Hivyo wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari wenye sifa za kujiunga na programu za Astashahada na Stashahada, walioomba na hawakufanikiwa kupata nafasi katika awamu ya kwanza na wale ambao hawajaomba hadi Udahili ulipofungwa tarehe 20 Agosti, 2017 watume maombi ya Udahili kwenye vyuo vya serikali na binafsi.
Kwa wanaotaka kuomba vyuo vya Serikali/Umma kwa fani za Ualimu na Afya watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz kwa kubonyeza kitufe cha Apply online (SAVS) kama ilivyokuwa awali. Kwa wale ambao wamekweisha fanya maombi kwenye mfumo na hawakuchaguliwa wanaweza kubadili machaguo yao kwa kurekebisha programu walizo chaguo au kada kwa kutumia kurasa (Profile) binafsi zao.
Baraza linatoa taarifa kuwa vyuo na kozi zilizodahili wanafunzi wa kutosha hazitaonekana tena wakati wa maombi ya awamu hii ya pili. Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kuwa wafanye maombi yao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho za kufunga dirisha la Uhakiki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 20/09/2017
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com