Sosiolojia
ni taaluma inayoshughulikia uchunguzi na uchanganuzi wa matabaka na makundi ya watu
katika jamii. Mifano ya matabaka na makundi ya watu katika jamii ni kama vile:-
(a) Matabaka
ya watu wa kipato cha juu, watu wa kipato cha kati, na watu wa kipato cha
chini, pina kuna matabaka ya watawala na watawaliwa.
(b) Kuna
makundi ya wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, wasomi, wanafunzi, wazee,
vijana, wanawake n.k
Matabaka na makundi
haya ya watu, kwa kawaida huwa yanatumia aina ya lugha inayoelekea kufanana, na
inayotofautisha matabaka na makundi mengine ya watu katika jamii.
Sosiolojia ya lugha
inatakiwa ihusike na uchambuzi na ufafanuzi wa muundo wa jamii, hususani kama
unavyojidhihirisha kutokana na tofauti katika matumizi ya lugha. Lengo ni kujua
jamii na kuchambua lugha na ni kipengele kimojawapo miongoni mwa vipengele
vingi vya kusaidia kufikia lengo hilo. Kwa mtazamo huo sosiolojia ya lugha
inakuwa tawi la au mada ya sosiolojia na kila kipengele kinachochambuliwa
hufanywa hivyo kwa nia ya kuchangia katika kuielewa jamii au
Kwa nia ya kuboresha nadharia za
(sosiolojia) za kijamii. Vipengele hivyo, kwa maoni ya Trugdill (1983) ni kama
vile ulumbi, yaani hali ya kutumika
kwa lugha mbili au zaidi katika jamiilugha moja; diglosia, yaani hali ya lugha mbili zinatumika katika jamiilugha
moja kugawana uamilifu, hadhi na fahari; kubadili
msimbo; yaani matumizi ya lugha mbili tofauti katika mazungumzo hayo hayo;
kupanga sera ya lugha; mwelekeo kuhusu lugha, lugha katika elimu, na masuala
mengine yote yanayohusiana na kufafanua nani anasema lugha gani na nani.
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com