Kuna nadharia
mbalimbali za chimbuko la fasihi kama ifuatavyo.
Chimbuko
la fasihi ni Mungu. Wataalamu wengi wanadai kwamba mungu
ndiye msanii mkuu kwani aliumba ulimwengu kwa usanii wa ajabu na mwanadamu ni
moja ya sanaa ya mungu. Hivyo mwanadamu kapewa uwezo na mungu kuweza kubuni
mambo mbalimbali. Inadaiwa kuwa uwepo wa dunia ni zao la Mungu, yeye ndiye
aliyeiumba dunia na kuumba binadamu pia. Wataalamu wanaounga mkono hoja hii ni
pamoja na Plato na Hesioid.
Chimbuko
la fasihi ni sanaa inayotokana na sihiri.
Sihiri ni imani ya kimuujiza, mathalani zamani wawindaji walipotaka kwenda
kuwinda walichora mchoro wa mnyama wanayehitaji kumuwinda kasha kuchoma mkuki
katika mnyama yule wakiamini wakienda kuwinda atamuua mnyama yule.
Chimbuko
la fasihi ni wigo au uigaji. Nadharia hii hudai kuwa mwanadamu
huiga mazingira yanayomzunguka na kuyaamishia kwenye maandishi, hivyo sanaa ya
mwanzo mara nyingi imejaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira.
Mathalani wanyama, mimea. Mito na kadharika. Nadharia hii imeenezwa na Plato na
Aristotle
No comments:
Post a Comment
syliverymanyama@gmail.com