Flower
Flower

Saturday, October 21, 2017

NADHARIA YA NARATOLOJIA/USIMULIZI

misingi ya nadhalia
Kwamba binadamu ni kiumbe cha usimulizi.
Binadamu hufanya maamuzi yao kutokana na sababu za msingi kama historia, wasifu, tawasifu, mila na desturi na tabia ya mtu binafsi.
Urazini wa usimulizi hushikiliwa na mshikamano na usahihi wa hadithi zetu.
Dunia ni mkusanyiko wa hadithi tunazochambua

- Hadithi huumba upya maisha yetu.
Ktk usimulizi tunazingatia:
Msimulizi ktk sura zake zote
Msimulizi na Nafsi zake zote
Nafasi ya mwandishi na ya msimulizi
Nafasi ya Jamii ktk usimulizi
Wahusika ktk simulizi:
Wahusika watendaji
Wahusika wasio watendaji
Mhusika kama Msimulizi
Vifaa vya usimulizi???
Matini simulizi ni matini ambayo wakala hutueleza simulizi kwa njia maalumu kama vile lugha, taswira, sauti, majengo au vyote.
Simulizi ni fabula ambayo huwasilishwa kwa njia maalumu
Wakala ni msemaji anayemwakilisha mwandishi au jamii . Anaweza kuwa mtu, kitu au mnyama
Fabula ni mfuatano wenye mantiki wa matukio ambayo husababishwa au huelezewa na mtendaji/mpangilio kiwakati
Tukio ni badiliko lolote kutoka hali moja kwenda nyingine
Watendaji ni huelezea/huunganisha matukio
Utazamishwaji dhana inayotueleza uhusiano kati ya nani anaona nini na nini kinachoonwa
Simulizi ndani ya Simulizi/Mchezo ndani ya Mchezo--      
  i. Mashtaka
  ii) Utetezi wa wajumbe
      

No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny