Flower
Flower

Wednesday, September 13, 2017

Dhana ya jamii na taifa

  

Jamii ni jumla ya mtu mmoja mmoja ambao kwa pamoja huunda jamii yenye matabaka na makundi ya watu mbalimbali (Mekacha 2000).
Matabaka na makundi ya watu katika jamii hutokana na vigezo anuwai kama umri, jinsia, kipato, aina ya kazi, viwango vya elimu, maeneo ya kuishi na kadhalika. Mekacha (2000) anaeleza kuwa jamii ni dhana changamano.

    Uhusiano baina ya lugha na jamii
Lengo la mwanaisimujamii ni kuchunguza na kufafanua uhusiano uliopo baina ya lugha na wazunguzaji wake. Lengo hili linalenga kuifahamu jamii kwa kuchambua lugha ya wazungumzaji wanayotumia. Kwa kuchambua lugha wanayotumia wazungumzaji, tunawezakutambua yafuatayo:-
ü  Kama jamii ina dini au imani ipi?
ü  Kujua jamii inayotumia lugha fulani iko maeneo gani ya nchi?
ü  Watu wanaotumia lugha fulani wapo maeneo gani ya nchi?
ü  Ni wanaume au wanawake, vijana au wazee, wasomi au wasiowasomi? n.k
Kwa kusikiliza mazungumzo ya watu mbalimbali utagundua kuwa kuna vibainishi vya lugha vinavyoonesha aina ya watu wanaozungumza. Vibainishi hivyo vyaweza kuwa vya kimofolojia, kifonolojia, kileksika n,k
Mfano mzungumzaji akisema
1.                  Umenunua wapi samaki nchanga?
2.                  Mtoto amefika apa sa ngapi?
Kwa kusikiliza matamshi katika sentensi ya kwanza utagundua kwamba mzungumzaji, ama kutokana na athari za kifonolojia zitokanazo na lugha yake ya asili au kwa sababu nyinginezo, ana mazoea ya kutamka baadhi ya maneno sanifu ya Kiswahili kulingana na matamshi ya lugha yake ya kwanza.  Badala ya kutamka mchanga anatamka nchanga. Kwa mujibu wa jamii za Tanzania, watu watu watamkao [nchanga] badala ya [mchanga] ni Wamakonde kutoka mkoa wa Mtwara.
Tunaweza pia kutambua aina ya wazunguzaji wenye imani au dini mbalimbali kwa kuchunguza lugha ya mazungumzo inayotumika na wahusika wakuu.
3.                  (a) Nataka mtoto wangu abatizwe jumapili ijayo, je inawezekana?
(b) Huyu mzee hakufunga Ramadhani kwa sababu alikuwa mgonjwa.
 (c) Kila mwaka baba huwa anakwenda kutambika kwenye milima yao.
            Kwa kuzingatia mifano yetu katika (3), unaweza kugundua kuwa katika mfano wa 3 (a)                        mzungumzaji ni wa dini ya kikristo, wakati mzee anayeongelewa katika 3 (b) ni wa dini    ya kiislamu.  Katika mfano 3(c), baba anayezungumziwa anaweza kuwa ni imani ya dini             ya jadi. Uteuzi ya maneno batiza, hakufunga ramadhani na tambika ni vibainishi ya      kileskika.


No comments:

Post a Comment

syliverymanyama@gmail.com

AddToAny