Wataalamu
mbalimbali wamefasili maana ya isimu kama ifuatavyo
Richard
na wenzake wanasema Isimu ni mtaala ambao huchunguza lugha kama mfumo wa
mawasiliano ya mwanadamu.
TUKI(1990)
wanasema isimu ni sayansi ya lugha
Hartman(1972)
wanafasili isimu kama eneo maalumu la mtaala ambao lengo lake huwa kuchunguza
lugha.
Usayansi
wa Isimu.
Wataalamu
na wanaisimu hujiuliza ni kwa vipi isimu ni sayansi. Isimu ni sayansi kwa
sababu yam kabala ya kisayansi ambayo hutumiwa na wanaisimu wakati wanapofanya
shughuli zao za kuchunguza lugha.
Zifuatazo
ni sababu za isimu kuwa sayansi
Utoshelevu wa kiufafanuzi.
Sifa
hii huziilika wakati ule wanaisimu wanapofanikiwa kufafanua viwango vyote vya
lugha inayohusika. Viwango hivyo vya lugha ni pamoja na fonolojia, mofolojia,
semantiki, na sintaksia. Wakati mwanaisimu anapofafanua viwango anuai vya lugha
hulazimika kueleza umilisi walionao wazawa wa lugha hiyo katika viwango
mbalimbali vya lugha yao.
Uchechefu
Sifa
hii hubainika pale ambapo wanaisimu hufanikiwa kuzionesha tofauti zote zilizomo
katika kongoo linalochunguzwa na hatimaye katika lugha yote kwa ujumla.
Utoshelevu wa kiuteuzi
Sifa
hii hujitokeza pale mwanaisimu anapoweka msingi wa kiisimu ambao hudhiirisha
bayana uhalali wa kukiteua kiunzi fulani kitumike wakati wa uchunguzi wa
masuala fulani katika lugha fulani badala ya kuvitumia viunzi vingine
vinavyoweza kuwa na utoshelevu wa kiufafanuzi sawa na kiunzi kilichochaguliwa
kutumika.
Utoshelevu wa kiuchunguzi
Sifa
hii huzihilika wakati mwanaisimu anapofanikiwa kuyaeleza yote yale
yanayoonekana katika kongoo linalochunguzwa bila kuacha au kupuuza kitu
chochote katika kongoo hilo.
Uwazi.
Sifa
ya uwazi hubainika wakati ule wanaisimu wanapoeleza kwa uwazi kabisa mawanda ya
kanuni walizotumia katika ufafanuzi wao ili kuhakikisha kuwa kanuni hizo siyo
tata na wala hazipishani.
How can i download this document?
ReplyDelete